Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Kuna mwaka nilijipanga kununua flat screen mpya ya nyumbani. Nikaingia mtandaoni na kuongea na muuza mali kwa njia ya simu. Akanielekeza mpaka dukani nikafika. Nikapokelewa na kijana wa kiarabu nahisi alikuwa O level. Kilikuwa kipindi cha likizo za shule. Akanipeleka kwenye sectiona ya flat screen kwenye duka na kunipa kila sifa ya TV iliokuwa mbele ya macho yangu. Mimi nilikuwa na ingia google na kuandika model namba ya TV na specs zake zipo kama dogo alivyosema. Nilikuwa na budget ya 1M, ila dogo kanishawishi kununua TV ya 1.5 M yenyewe warranty ya miaka 2. Kaniitia mtu wa usafiri na bei kambana na kumshusha. Mali ilifika salama na haijapata tatizo lolote huu mwaka ushapita. Baada ya siku kadhaa ya kununua ile TV, nilipigiwa simu na yule dogo na aliniulizia ufanisi ya TV.

Wenzetu biashara wana wazoesha watoto wao tangia mashuleni. Wakati sisi waswahili kipindi cha likizo tukienda tuisheni mchikichini ili kupanga mabanda mitihani ya taifa. Waswahili tukimaliza vyuoni ndo tuna tembeza CVs na mavyeti.

Na bado hatujashtuka!
Uko sahihi, inawezekana maandalizi ikawa changamoto; ndio maana mzazi kama ameajiriwa, atataka na mtoto wake aajiriwe n.k
 
Nitajie kipimio sahihi ulichonacho
Nadhani kipimio sahihi cha mafanikio ya mtu ni yeye mwenyewe, KWa sababu KILA mtu ana malengo na mipango yake.... KWa sababu kuna mwingine yeye ana amini kuwa ataendesha maisha yake vyema katika kujiajiri na mwingine kuajiriwa.... Eti sijui kauli za mtu aliye ajiriwa ni mtumwa ni kauli za kishamba... Na hivyo vitu ni asili ya dunia.... Ili kuwe na usawaziko lazima wengine waajiriwe na wengine wajiajiri.... Achaneni na braabraa za wabinafsi na wachoyo.... Na nakwambia ukweli..."mijitu inayo toa hizo kauli sijui za AJIRA utumwa Mingi imeajiriwa" na hakuna mfanyabiashara au mmajilia mali wa kweli anaye kejeli muajiriwa..."
 
Tatizo ni nini, elimu au kuna kingine?
Mifumo mibaya ya govt katika biashara

Mfano...Unamkadiliaje kodi mtu anayeanza biashara how it comes? Sawa unaweza ukaweka constant tax kwa biashara flan kutokana na level za mtaji....je kwa biashara za bidhaa ambazo ziko imported..mtu wa dar atakuwa sawa na kigoma ...maana akiupokea bandarini gharama za kusafirisha..ushuru wa vibali
Ingependeza watu wapewe muda flan baada ya kuanza biashara ndio alipe baada ya kutoa running cost profit ndio wagawane..

Pili serikali km yenyewe kwa yenyewe haina communication unakuta sehemu km machinga complex,kariakoo kila siku wafanyabiashara wanatozwa kodi ilo eneo then ghafla bin vuu mtu siku anasimama anasema wamevamia sehemu je izo kodi zinavochukuliwa hawakuziona? Unavunja mabanda bila kuwalipa watu

Tatu mashart ya mikopo pia magumu mtu km hana kitu hakopesheki? Na riba yake ni kubwa Seriously km kuna fungu la vijana,wanawake wanapewa bila hayo mashart ...kwann mtu asikopeshwe kwa mashart nafuu na riba kidogo

Nne...Kuwe na TAWA TRA ya elimu ya ujasiriamali(finencial education) sio tu kukusanya kodi...hii ni sawa mwalimu asiyemfundisha mwanafunzi ila anampa mtihani akimsubiri afeli amuadhibu

MIMI YANGU NI HAYO TU MWENYE USHAURI AONGEZEE
 
Nini kifanyike ili tuweze kujiajiri
 
Lakini wapo waliopiga hatua kama kuanzisha kampuni mbalimbali; je hawa wamefanikiwaje?
 
Jambo kubwa ni uoga wa wasomi kujiajiri kwa sababu wana option ya kuajiriwa, wengi waliojiajiri wanakuwa na plan A tu.
Tatizo kubwa ni watu kuogopa kulipa gharama katika kujiajiri.
Kuajiriwa ni utumwa mkubwa sana.
Maisha mazuri ni kujiajiri, kila jambo kubwa linahitaji muda, kujitoa, kusimamia.
Tujiulize ni lini uliona mhundi ameajiriwa serikalini hapa nchini kwetu.
 
Ukijiajiri utatumwa na clients wako au soko. Tabu ipo pale pale

I'd argue wafanyakazi Wana a balanced life style kuliko waliojiajiri. Hii notion kwamba ajira ni mbaya na kila mtu inabidi ajiajiri as though self-employed wote wamefanikiwa is nonsense.
Levels mzee, kuna vibarua, wafanyakazi na waajiriwa.

Ukiwa kwenye makundi mawili ya kwanza hayo ni vizuri ukapambana kujiajiri tu.

1.Vibarua hawana mikataba rasmi hawa boss akinuna akasema usije ujue ni mateso bila chuki. Mara nyingi vipato vyao havitoboi laki 3 kwa mwezi mzima. Hamna muda maalum wa kutoka kazini ila saa 12 asubuhi lazma uwepo eneo la kazi 😂😂😂 na mazingira ya kazi ni magumu.

2. Wafanyakazi hawa hawana tofauti sana na vibarua isipokuwa muda wa kuripoti wengi huwa saa 2 asubuhi na kutoka saa 11 jioni na wanaenda hadi siku ya Jumamosi. Kipato chao range ni laki 5 mpaka 2M kwa waliobahatika kupata ofisi nzuri. Hawa sifa yao kuu ni kudaiwa kila kona mikopo mikopo tu alimradi. Wapo wanajitutumua na vimikebe vya mtumba toka japani na kujiona wamewin sana ila hamna kitu wanatubu sana kitaa.😂

3. Wenye ajira, kiukweli ukiskia kijana amepata ajira jua tu kwamba amefanikiwa kuukimbia umaskini kwa ghafla mno kama mwanga wa radi. Hawa wengi unakuta wako kwenye Taasisi nyeti kama TCRA, TPDC, Mifuko ya hifadhi ya jamii ambako level ya mshahara si chini ya 4M kwa kuanzia tu na safari nyingi zenye per diem mlima na dili nyingi za mkwanja mrefu, hali kadhalika makampuni makubwa ya binafsi kama GGM au Barrick Gold ambako watu wanalamba 8 figures za madafu. Hawa ofisini huwa ni saa 3 mpaka saa 9 wanafunga siku😀 na benefits zote hupewa kuanzia bima kubwa ya familia, transport, communication na hata schoolfees za watoto. Hawa waajiriwa wengi ndio husukuma vyuma vya kibabe kwa 0kms na ndo juzi kwenye speech mzee wetu Jenerali ulimwengu aliwagusia kama huna disposable income walau ya 5M kwa mwezi usijitwishe gari litakutesa.

Kwahio tujichekeche tu ndugu zangu. Maswala ya kujiajiri yana mantiki kwa vibarua na wafanyakazi. Walioko kwenye level ya ajira wanaweza ku make it in life easily kuliko hata wanao hustle kupambana na kero za TRA,OSHA,FIRE, Manispaa na wengineo wengi.
 
Elimu ya darasani hasa inayopatikana kwa nchi zetu za kiafrica haimjengei mtu uwezo wa kujiajiri. Unahitaji kutumia akili ya ziada kuweza kujiajiri. Ila, ukitaka kutumia akili ya shule kujajiri kamwe hutakaa ujiajiri.
 
Nakubaliana na hoja yako hasa kwa wale wanaolenga pesa tu, ila msukumo wa mtu kujiajiri sio pesa tu; kuna vitu vingi
 
Bongo watoto wakienda shule wanatoka nyumbani nyumbani kwao si nyumba ya kupanga na asubuhi wakanywa chai na kipolo cha wali maharage, na ukaweza wapatia matibabu, na ukaweza kuwanunulia kifurushi cha azam cha elfu 25 kwa mwezi, na wakapata uhakika wa matibabu wewe umetoboa haijairishi umejiajiri au umeajiriwa sababu duniani tunapitaw ewe tayali umetusua hizo nyingine mbwebwe gari si kuna bajaji kuna uber kuna bodada nini sasa unataka kama siyo kihelele na mawazo ya kitoto

NB
Kibongo bongo ukiweza timiza hayo juu unatakiwa ukaze sana tena sana ingawa vijana mtachukulia pouwa
 
Elimu ya darasani hasa inayopatikana kwa nchi zetu za kiafrica haimjengei mtu uwezo wa kujiajiri. Unahitaji kutumia akili ya ziada kuweza kujiajiri. Ila, ukitaka kutumia akili ya shule kujajiri kamwe hutakaa ujiajiri.
Inawezekana ikawa ndio sababu
 
Shida kubwa ni Elimu yetu inatulaza usingizi sana, yaani Mtu unatumia miaka mingi kuwaza namna ya ku-score A's tu katika masomo, ukirudi likizo tusheni, nyumbani homework ya masomo ya darasani. habari za ujasiliamali hujishughulishi nazo.

Na hayo masomo bora hata yawe yanalenga ktk ubunifu, kupata pesa na kutengeneza faida kupitia hiyo pesa, kukuza uchumi unakuta ni nadharia fulani za kukaririshana tu basi mtu anazidi kuwa mgeni na mazingira halisi.

Kwangu Mimi shida kubwa ni mifumo yetu ya elimu inalaza watu usingizi.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom