Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela hatotakiwa kujishughulisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi kwa nia ya kuwachochea mashabiki wa Yanga dhidi ya vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu nchini
Maamuzi hayo yamefikiwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kupokea malalamiko yaliyotolewa Februari 19 alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo alisema TFF na TPLB vinaihujumu Yanga
Mwakalebela amemtozwa faini ya Tsh. Milioni 5 kwa kosa la maadili. Pia ametozwa Tsh milioni 2 kwa kosa la kuta taarifa za uongo juu ya mkataba kati ya mchezaji Bernad Morrison na klabu ya Simba
View attachment 1741073