Namshauri AACHE Tabia yake ya kubebwa na marefa,,la iko siku atakuja fia ulingoni
Ndio maana anamkacha Twaha kiduku
View attachment 1923505
Kwa tunaoijua boxing, mwamuzi wa katikati ali-mess up kidogo. Maamuzi yake ya kumaliza pambano mapema vile, mmh, ni walakini. Indongo alionesha bado kuwa na uwezo wa kuendelea na pambano na hata kushinda, haiyumkiniki.
Mwamuzi yule mzee naweza sema alikatisha pambano prematurely. Pambano la Tony na Mahlangu linatupa mwanga kidogo kuhusiana na situation hii. Mahlangu alionekana kuzidiwa tangu round ya kwanza lakini mwamuzi hakukatisha pambano. Tukashuhudia aliyepigwa round zote ndiyo kampiga kwa KO mpinzani wake. Yeah, that's boxing. It's a fight or die game!
Kuna bout hupenda kuitazama titled "Greatest Comeback in boxing History" kati ya Diego Corrales dhidi ya Jose Luis Castillo. Mwamuzi kama wa jana angemaliza fight mapema kwa kumpatia Jose ushindi kwani mpinzani wake Diego alionekana wazi kuzidiwa na alikuwa ameumizwa hata hawezi kuona vizuri. Lakini, mnamo round ya mwisho, miraculously, Diego aliamka kutoka "ndotoni" (Twaha Kiduku) akaushangaza ulimwengu wa ndondi. Waamuzi wafuate sheria. Wataharibu ladha ya mchezo huu ambao umeanza kupendwa tena.
Hata hivyo, hongera sana Hassan. Ulicheza vizuri na ulionesha uwezo dhidi ya mpinzani wako. Naamini Mwalimu wako atafanya corrections kwenye maeneo machache kadhaa, ikiwemo, speed, feetwork, target, nk.
Naamini, una nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa dunia. Hongera sana.