Kwahiyo kosa la Kiduku ni nini? Kuomba pambano na champion?[emoji23][emoji23], Sasa usipoomba pambano na champion unataka aombe na nani? Ni kawaida kwenye masumbwi bondia yeyote mwenye lengo la kufika on top lazima apigane na wa juu yake ili aipate hiyo nafasi, hata kina Antony Joshua tunaowajua wasingepata majina kama wasingepigana na 'matop' kina Klitschko na kuwapiga, Andy Ruiz dunia haikuwa inamtambua hadi alipompiga AJ. Na juzi hapa nimemuona bondia no1 one pound for pound anaitwa Crawford alipompiga Kelly Brook na alipoulizwa yupi unamtaka next, akajibu anamtaka Man Pacquiao, Je jiulize kwanini anamtaka zaidi Man Pacquiao wakati kuna mabondia wazuri wengi kwenye division yake kama Errol Spence Jr, Keith Thurman, Shawn Porter, Garcia, n.k. Jibu; anamtaka zaidi Pacquiao kwakuwa 1. Ana mkanda 2. Ni maarufu zaidi (so kibiashara anatarajia kupiga hela zaidi) 3. Ni legend tayari (Ukimpiga legend cv yako inakuwa kubwa zaidi) 4. Kujiongezea fanbase (kwakuwa Pac ana mashabiki wengi hivyo sikuhiyo anauhakika wa kupata mashabiki wengi wapya endapo akiperfom vizuri hivyo kumuweka vizuri zaidi kibiashara). Hivyo Mwakinyo akiombwa pambano na Kiduku asipanic, inapaswa awe proud kwamba yeye ni mkubwa tayari ndio maana mabondia wengine wakubwa wako interested naye ili na wao wafike hapo juu alipo, hata kama anakataa pambano atafute sababu za kukataa zenye mashiko maana sio lazima akubali (pambano la lazima ni la mandatory tu ila haya mengine ana hiyari ya kukubali au kukataa), ila anachoboa watu ni ile mipasho yake na dharau zisizo na maana, angekuwa anakataa kistaarabu tungemuelewa tu. Na sio kusema huwezi kupigana na bondia wa Moro, wakati baada ya kutoka Uingereza alipigana na bondia mchovu kabisa wa Tanga anaitwa Said Yazidu, that's NONSENSE [emoji23][emoji23]