Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Uongo wa mwanaume tena msomi ni hatari sana!Hili jamaa liongo balaa!Yaani hata aibu hana,anaomba hoja ya Richmond irudishwe?Ama anatuona sisi watoto wadogo ama tuna mtindio wa akili???!!!Tafadhali,ni bora ukaheshimu wananchi kama walikunyamazia
 
Ujasiri wa kusema wameficha baadhi ya taarifa kwenye report kuilinda serikali?
HAKUNA ALIYECHUKIA UFISADI THAT TIME BILA YA KUMSIFIA MWAKYEMBE KWA ILE REPOTI.
WOTE TULIOKUWA UPINZANI TULIMUITA SHUJAA NA HATA ALIPOPATA LILE SUALA LA KUWEKEWA SUMU TULIILAUMU SERIKALI NA KUMSIFIA MWAKYEMBE.
Alipojiuzuru Lowassa ndiyo kaiokoa SERIKALI NA si kuficha hiyo ripoti.
 
Hii ni kuonyesha umbumbu wake Katika sheria ijapokuwa anajitambulisha kama mwanasheria.
 
Tuliwaambia Chadema ....hata wapige sarakasi gani ...huu mzimu wa usaliti utawafata hadi watubu hadharani ....
 
Usipanic sasa [emoji16][emoji16][emoji16]

Hiyo si lugha ya kupanic kutoka kwangu, ila nimeshindwa kujizuia kukujibu kwa lugha uliyoizoea.

Ukitaka kuheshimika nawe waheshimu binadamu wenzio na siyo kila kukicha unajadili na kubandika hoja za kejeli, dharau na ujuaji.

Niamini tu hayo ndiyo maisha yako ya kila siku ya umbea na ati unajiita Daudi Mchambuzi, kumbe uchambuzi wa kijiweni.

Acha maneno, tumia lugha staha.
 
Cdm wametoka nduki kama trump
Mmmhhh kumbe wenye uchungu ni chadema tu,kama ukweli upo kwa nini ccm hawaileti hiyo hoja tena,ili wampate muhusika wa kweli wa Richmond, Mwakyembe acha unafiki wewe baba umekubali demotion basi vimilia hivyo hivyo uendelee kutumika
 
Warudishe ile hoja bungeni tutajua mwenye ugonjwa, mwenye PHD na mwenye Bachelor Degree ya kucheza ngoma jukwaani na manyanga miguuni. Wekeni mziki acheni maneno...
Kwani ile mahakama ya mafisadi inafanya kazi gani, au unajitoa ufahamu mkuu?
 
Mmmhhh kumbe wenye uchungu ni chadema tu,kama ukweli upo kwa nini ccm hawaileti hiyo hoja tena,ili wampate muhusika wa kweli wa Richmond, Mwakyembe acha unafiki wewe baba umekubali demotion basi vimilia hivyo hivyo uendelee kutumika

Wabunge wa Chadema ndio walileta hoja ya ku challenge report ya Richmond sio CCM!
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!

Mwakyembe aliongoza Kamati ya Richmond na mpaka leo anadai Lowassa ni fisadi. Mbona alipokuwa Waziri wa Katiba na Sheria hakumshitaki? Yeye si ndiye alikuwa akisimamia mahakama ya mafisadi?
Hata akiibua hoja hiyo leo, itasaidia nini kama fisadi hashitakiwi? Huu wote ni unafiki tu unamtafuna
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!

Hivi yeye si yuko serikalini? Kama kuna ufisadi anasubiri mpaka hoja iletwe badala ya kumpeleka kwenye ile mahakama yao waliyo anzisha?
 
Tuliwaambia Chadema ....hata wapige sarakasi gani ...huu mzimu wa usaliti utawafata hadi watubu hadharani ....

..Wabunge wa upinzani wanataka Mwakyembe ashughulikie suala la Makonda kwa mtindo uleule alioutumia kushughulikia kashfa ya Richmond.

..kama Mwakyembe aliweza kuhitimisha suala lile bila kumhoji Lowassa kwanini anashindwa kuhitimisha suala la kuvamiwa clouds bila kumhoji Makonda?

..hoja haipaswi kuwa Lowassa alionewa or not. Kwa maoni yangu hakuonewa.

..hoja ni kwamba Mwakyembe alitengeneza precedence ya kutoa hukumu bila kulazimika kumhoji mtuhumiwa namba moja. Precedence hiyo ndiyo wabunge wanataka Mwakyembe aitumie kwenye shauri la Makonda vs Clouds ambapo kuna ushahidi wa video.

..lingine ni kwamba Mwakyembe alikuwa waziri wa sheria. Sasa nini kilimzuia kipindi hicho kumfungulia mashtaka Edward Lowassa?

..tena Mwakyembe alikuwa akijitapa wakati wa kampeni kwamba jinai haifutiki. Kwamba Lowassa alitenda jinai hivyo ana kesi inamsubiri.

..kwa hiyo MWAKYEMBE kudai suala la richmond lirudi bungeni ni ULAGHAI tu. Suala hilo lilishamalizika bungeni na linapaswa kwenda Mahakamani.
 
Kama kuna lilofichika kwa hoja liludishwe Bungeni ili ukweli uwe bayana na mwenye hatia aliyeisababishia Hasara Nchi yetu kwanza mali zake zitiwe tanzi kufidia hasara pamoja na waliohusika wote na sakata hili wasionewe haya
 
Back
Top Bottom