Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Wabunge wavae Uzalendo,waipekeke ili nasi tufahamu ukweli ni nani mwenye Richmond! Wasisubiri hadhi watangulie mbele za haki ndipo wanasema ukweli,inaumiza kwa sababu Marehemu hana pumzi ya kusema ili kujitetea!
 
Hii serikali ijiuzulu tu.

Yaani wao ndio wameshika dola na wao ndio waliofunga huo mjadala Bungeni alafu leo ndio wanaowataka wapinzani waibue swala hilo badala ya kutekeleza maazimio ya Bunge au kufungua kesi Mahakamani.

Pathetic!
Kama wamejua hoja imefungwa hao akina Kubenea and Co mbn kila siku kwenye magazeti yao na nasari kurudia jana, waambie wairudishe tena
 
Hapo amewaweza vibaya sana, na hatutasikia lolote toka upinzani.
 
Wanaipelekaje Bungeni. Wanaipeleka kama hoja mpya ama kama hoya ile ile ya zamani. Kwani hiyo Richmond bado ipo? Mitambo yake iliuzwa kwa Dowans na Serikali ikachukua kodi, na Dowans nao wakawauzia Symbion na serikali ikachukua kodi na mitambo hiyo inatumika kuwauzia TANESCO umeme na serikali inachokua kodi na tozo mbali mbali!!
Kanuni si zipo watatumia hizo hizo
 
mkulu kipindi kile alituambia mmiliki hamjui sasa Le Dr Alimjua vipi wakati boss wake hamjui???
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!

Hakuna mtu yeyote mwenye akili nzuri ambaye anamuunga mkono Lowassa ambaye anaweza kuthubutu hata ndotoni kuleta tena hoja ya Richmond; hii changamoto imetolewa mara nyingi na hakuna aliyethubutu kuichukua. Lowassa alipewa nafasi ya kujitetea mbele ya wabunge wote na mbele ya taifa lote lakini kwa hasira aliamua kuzira uwaziri mkuu kupitia ile hotuba yake maarufu ya "nimedhalilishwa sana".
 
. Mzee mwanakijiji we unaamini ni yake? Na je siku ukiambiwa labda ni ya mama Clinton utakubali kwa mfano lakini?hama ya Obama hivi?
 
Kha! Ndo mnamuita Dr huyo, mbona hoja zake hazina mashiko na hazistahili kuongelewa na mtu mwenye hadhi-cheti cha PHD achilia mbali nafasi aliyonayo ya uwaziri.

My take: Atumwe India kwa matibabu haraka sana, mana naona ile sumu imekula kaubongo kaliko kabakia kazima kale daaah
Du inawezekana?Si alisema angeeleza yote serikali ingeanguka? Alikuwa akimaanisha nini? Wana siasa msituchezee tumeshanyooshwa tayari ile migongo iliyopinda
 
Aliekua waziri wa katiba na sheria na akashindwa kumfunga Fisadi Lowassa.
Naamini unajua maana ya 'Natural Justice'. Kwamba mtu hapewi adhabu mbili kwa kosa hilohilo. Lowasa adhabu yake ya kukubali kujiuzuru ilimpa nafuu ya kutoendeleza mjadala bungeni, wakati huo na kuzua makibwa ambayo yangepelekea kufikishwa mahakamani, na leo mjadala ungekuwa haupo labda na upinzani wanatawala nchi hii.

Naamini umemsikia na kumwelewa Dr Mwakyembe alivyosema kuhusu hilo suala. Kwamba, wabunge wa upinzani wanalichokonoa suala lililokwisha fungwa lakiri.

kisu cha ngariba: kwa jina la ID yako umekuwa ukijadili au kuleta hoja za udaku mtupu. Nina uhakika hata maisha yako ni ya kingaribangariba (kukatakata tu, pasipo mpangilio).
 
Sasa kama ana ukweli mwingine tofauti na ule aliousoma bungeni wakati ule maana yake nini?
Kwani kasema ana ukweli mwingine? Hana mwingine bali kwa wale wasio ridhika may b hawakufuatilia n.k 2006 mpk leo ni miaka 11 wengi walikuwa wadogo.
 
Anashindwa nini kuifufua yeye ambaye anayo mengine aliyoyaacha kwa faida ya chama chake? Amekuwa waziri wa sheria kwa nini asimpeleke edo kwenye mahakama ya mafisadi? Msituvuruge mapema ngojeni 2020 tuwanyowe kwa chupa
 
Kha! Ndo mnamuita Dr huyo, mbona hoja zake hazina mashiko na hazistahili kuongelewa na mtu mwenye hadhi-cheti cha PHD achilia mbali nafasi aliyonayo ya uwaziri.
Huyu Bwana mwakyembe (Nakataa muita Dr) kajivua nguo sana kwenye hili. PhD holder wa sheria anasema hakuna haja ya kutimiza shart la Natural Justice kwa kuskiliza mtuhumiwa Kisa amehoji watu wengi. Is he really serious? Halafu anataka kutubabaishia na cjui investigation kitu gani. Tumbavu!

Nadhani ukiwa CCM unakuwa Zamwamwa automatically. Mana huwezi kujua nani Dr. Prof au Std 7. Bashite tupu
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!

Je yupo tayari kueleza yale aliyo acha ili serikali isianguke?
 
Back
Top Bottom