Fumbo mfumbie mjinga mwerevu hung'amua.
Baadhi ya makamanda wa CHADEMA (hasa CHADEMA asilia) hawaitaki ndoa ya kisiasa kati ya Mbowe na Lowasa, sasa watoke vipi ni jinsi ya kuirudisha suala RICHMOND bungeni.
Mwakyembe naye kawatega waingie vichwa vichwa. Likiachwa kurudishwa bungeni, basi yatosha CHADEMA kuthibitishiwa kuwa waliyekuwa wakimtuhumu, kwenye majukwaa kuwa ni fisadi, kweli ni fisadi.
Hivyo hoja yao, ya kila siku kila akitajwa kuhusika na ufisadi, ati mwenye ushahidi atoe afikishwe mahakamani, haitakuwa na nguvu tena. Kwanza, kwa yeye kujiuzuru Uwaziri Mkuu, ilikuwa adhabu tosha kwa mtu mwenye uchu wa madaraka, kama yeye.