Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe binafsi nakukubali sana kwa umahiri wako wa sheria na hasa nilikukubali zaidi kwa namna ulivyoiandaa ripoti ya Richmond iliyomng'oa Edward Lowassa kwenye uwaziri mkuu.
Tuwe wawazi jamani, ni nani ndani ya Chadema atakayekubali sakata hilo lirudi bungeni tena? Wako wanachama ndani ya chadema ambao mpaka sasa hawakubaliani na ujio wa Lowassa katika chama kwa kuwa kimepoteza agenda na hakitamaniki tena kwa wananchi kwa kuonyesha undumilakuwili wao. Lakini wanachama hao watafanyaje ili hali mwenyekiti wa kudumu wa chadema anamkubali Lowassa kwa maslahi yake binafsi? Nani ndani ya chadema atabetua mdomo saivi kupingana na mwenyekiti wa kudumu? Mnakumbuka mwanahalisi ilivyokuwa ikiichambua Richmond na mshirika wake Lowassa? Leo kubenea ataweza kuandika tena?
Ile muvi ya Richmond bungeni ilikuwa tamu sana na ninaomba irudishwe bungeni na watuwekee bunge mubashara wakati wote wa kuijadili Richmond hadi watakapomaliza.
Wapi Selelii jamani
Ngoja nikamate popcorn zangu nivute na kiti muvi ndo hiyooooo
Chonde chonde jamani chadema ileteni Richmond bungeni
Naanza kupasua chupa nipate vipande vya kunyolea
 
..Tuwe wawazi jamani, ni nani ndani ya Chadema atakayekubali sakata hilo lirudi bungeni tena?

Hili Sakata linapaswa kupelekwa kwenye ''Mahakama ya Mafisadi'', kama ipo, badala ya kuleta ngojera na ''kutishia'' kulileta Bungeni.
 
Hivi kumpeleka mtu mahakamani inahitaji maombi kwa wabunge wapeleke hoja bungeni??

Hiyo mahakama ya mafisadi mlijenga kama urembo???
 
Nimemtukana nani??Mie duka langu linaendelea vizuri,nalipa kodi na ninapata chakula kwa watoto na familia yangu
Watoto na familia yako wao hujawafunza kulalamika mitandaoni 24/7
 
Watoto na familia yako wao hujawafunza kulalamika mitandaoni 24/7

KOsa la kwanza mlilonalo UVCCM ni kuingiza familia ya mtu kwenye mambo ya mitandaoni.Naoma watoto wangu na familia yangu iache,nituhumu mimi,vinginevyo huna hoja kaa kimya funika bakuli
 
KOsa la kwanza mlilonalo UVCCM ni kuingiza familia ya mtu kwenye mambo ya mitandaoni.Naoma watoto wangu na familia yangu iache,nituhumu mimi,vinginevyo huna hoja kaa kimya funika bakuli
Sawa mangi, utagombea uenyekiti BAWACHA ?
 
Sidhani kama Chadema wapo Tayari kufukua kaburi ambalo Tayari walilifukia kwa kumteua Lowasa kuwa mbombea wa Urais Kupitia Chama chao.
 
Mkuu hata kagame alituaminisha watu kuwa watutsi million 1 waliuawa 1994 yaani mauaji ya kimbari yalikuwa ni mauji dhidi ya watutsi kwa miaka 20 katuaminisha hivyo ila recently mambo yamekuwa wazi kuwa rwanda haikuwa na watutsi zaidi ya 200,000 ssa inakuwaje waseme walikufa watutsi million 1??? The whole world now knows the truth

Kwahyo hta ccm ilituaminisha watanzania wote kupitia ripoti ya mwakyembe kuwa yye ndo fisadi wa richmond ila with tym ukweli umejulikana ssa lowasa kasema yye hakuna alilofanya kikwete hakujua so whatever ushahidi chadema waliokuwa nao yeye simply "ALITUMIWA" ssa ndio unataka tuendelee kushkilia msimamo huo huo wa kuwa lowassa ni fisadi?? While the chain of command was clarified???
we jamaa una akili fupi sana CHADEMA ndio waliosambaza habari za ufisadi wa Lowasa kwa miaka nane kuhusu Richmond...na tume ya Mwakyembe ikadhibitisha ufisadi wa Lowasa.......sasa hiyo ya kusema Lowasa hausiki na Richmond ushahidi wake uko wapi?
 
chadema tuko tayari lowassa ahojiwe kwetu sio issue maana ukweli tunaujua
 
Kwahiyo wale watanzania wooote qliokuwa naahaba nae hadi wakati wa kampeni wengine wakawa wanazimia kwa kukosa hewa kwa sababu tu ya kumuna na kumsikiliza Lowasa hawana akili? Na kama hakuna mtanzania mwenye akili anayemuunga mkono Lowasa mbona aliwasumbua sana mwaka 2005? Hizo asilimia 56 za kura alizopata ilikuwa ni miti iliyomuunga mkono na sio watu? Na pia kama nyinyi mnajiamini kuwa hakuna mtu mwenye akili anayemuunga mkono Lowasa, mwambie mkuu aruhusu mikutano ya vyama vya siasa just for one week then uone kati yako na watanzania wengi ni nani hana akili!!!
mbona Lema huku Arusha kila siku anafanya mikutano ya hadhara mkuu hiyo mikutano imezuiwa wapi?
 
Wewe umeharibiwa na nini?Viroba au MAsogange??Hivi kuna FISADI zaidi ya Paul Makonda?Aliyekwapua Bilion nane za kivuko kibovu ni Lowassa au ni JPM??

Wa barabara mbovu je?Aliyejengewa hotel maneo fulani kama asante toka kwa mkandarasi ni Lowassa??

Kama umelewa Masogange ni juu yako
ukweli utabaki ukweli hata kama CCM kuna mafisadi hata Lowasa nae ni fisadi
 
Wale wanachama, wafurukutwa, wakereketwa na wapenzi wa CDM mliomtangaza Lowassa kwa miaka 8 kuwa Fisadi na baadaye mkarubuniwa kuwa ni Malaika kupitia kwa Mwenyekiti wenu, sasa mnakaribishwa Bungeni ili mtuthibitishie Umalaika wa Lowassa aliyekosa sifa za Urais CCM nanyi mkamchukua kwa kuingizwa mjini( "kubadili gia angani"). Mnao wabunge wenu mahiri wafufue sasa Richmond tujue mbivu na mbichi ili iwasaidie angalau kumpatia Lowassa uenyekiti wa Chama chenu kinachokufa! Inafahamika wazi kwamba Urais ndio asahau milele hiyo MTU wenu!! Karibuni mje na dawa za kutosha kumsafisha!!
 
Acha maneno mengi lowassa is the hero.
 
tena richmond ina watu wengi wengine ni marais wastaafu na wengi wako ccm mtaaibika bure
 
Chadema hawana huo uwezo, watabaki kupiga kelele tu lakini si kupeleka hoja bungeni officially.
 
Back
Top Bottom