Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Kiukweli wenye Mamlaka ya kuurudisha mjadala Wa Richmond Bungeni ni Ccm maana wako wengi !

Lakini Watanzania hawajasahau kipindi kile wapinzani walileta hoja ya kurejesha Upya bungeni Lakini Ccm wakagoma !

Hata kama MTU alikuwa na makosa lakini ulituthibitishia baadhi ya watu muhimu hawakusikilizwa akiwemo Mh Lowassa!

Kwa maoni yangu Nitaiombea sana Nchi yangu , lakini sitaruhusu mtu acheze na akili yangu mpaka 2020 nitakapotumbukiza kura yangu .
 
Baadhi ya makamanda wa CHADEMA (hasa CHADEMA asilia) hawaitaki ndoa ya kisiasa kati ya Mbowe na Lowasa, sasa watoke vipi ni jinsi ya kuirudisha suala RICHMOND bungeni.
Hebu shirikisheni kidogo mbongo zenu. Mbali ya Lowassa kujiuzulu ni mapendekezo mangapi ya Kamati ile teuli ya bunge yalitekelezwa. Hata bila ya hoja kurudishwa Bungeni yeye Mwakyembe aseme ni nini walitekeleza kwenye mapendekezo ya kamati ile teule ambayo yeye alikuwa Mwenyekiti?
 
Ukitaka utukanwe humu jf, ligusie swala la RICHMOMD, DOWANS na MTUKUFU LOWASA. Siasa zetu zimejaa unafiki, upinzani kwa kipindi cha miaka nane walikuwa WANAICHUKIA NYAMA YA NGURUWE ALAFU MWISHO WA SIKU, WAKAAMUA WAUNYWE MCHUZI WAKE , kwa hiyo si shangai watu waliomtukana LOWASA kwa miaka nane na kwa vinywa vyao walisema walikuwa na ushahidi kwamba jamaa ni fisadi, bila kusahau series zile za Bw Kubenea na MWANAHALISI za kila siku kumchambua Lowasa juu ya ufisadi wa RICHMOMD na DOWANS na kama haitoshi akamtuhumu LOWASA na ROSTAM wanahusika ktk kumwekea sumu Mwakyembe , leo hii eti LOWASA mtakatifu si UNAFIKI huu. Wanasiasa wametugeuza kama SIGARA KALI, sijui wametuona sisi watoto wadogo, ila si shangai kwani hata huyu wanaemwita BASHITE, siku akiwa kwao watamwita KIJANA SHUJAA MH PAUL MAKONDA, ndio siasa zetu FULL UNAFIKI.
 
Amewashauri pelekeni hilo suala kule ili lishughulikiwe ninyi si kila siku mnaona ccm wanafiki?
Si mliunda Mahakama ya Mafisadi sasa mnashindwa nini kumshitaki ili hali mwenyewe alishasema mwenye ushahidi aende Mahakamani?
 
Amewashauri pelekeni hilo suala kule ili lishughulikiwe ninyi si kila siku mnaona ccm wanafiki?
Wanaipelekaje Bungeni. Wanaipeleka kama hoja mpya ama kama hoya ile ile ya zamani. Kwani hiyo Richmond bado ipo? Mitambo yake iliuzwa kwa Dowans na Serikali ikachukua kodi, na Dowans nao wakawauzia Symbion na serikali ikachukua kodi na mitambo hiyo inatumika kuwauzia TANESCO umeme na serikali inachokua kodi na tozo mbali mbali!!
 
Hebu shirikisheni kidogo mbongo zenu. Mbali ya Lowassa kujiuzulu ni mapendekezo mangapi ya Kamati ile teuli ya bunge yalitekelezwa. Hata bila ya hoja kurudishwa Bungeni yeye Mwakyembe aseme ni nini walitekeleza kwenye mapendekezo ya kamati ile teule ambayo yeye alikuwa Mwenyekiti?
Kwa kulirejesha tena bungeni, nadhani hataishia kuhusu uhusika wa Lowasa, bali pia kupitia utekelezaji wa maamuzi ya Bunge.
 
Mwakyembe sema ukweli , tunazo taarifa zote kuhusu safari yako ya Marekani , tunawafahamu hata waliokuwa wanakutembeza , walipogundua uongo wako wakakushiti , ulitumwa kufunika kombe , UNABISHA , NIFUKUE MAKABURI ? tena aliyekuwa anakuzungusha ni mlokole mmoja mwenye asili ya kiafrica , natoa wito kwa wabunge wa Chadema kuirudisha bungeni hoja hii , Mwakyembe atakimbia .
 
Wairudishe tu ................... tena wasiishie hapo. Wazirudishe zote i.e. Escrow, EPA, Meremeta na Kangoda ili tuone kama kweli awamu ya 5 ipo kazini au same story!!
 
Richmond ikirudi bungeni.....mahakama ya mafisadi itawahusu akina JK, EL, JPM na cabinet yote iliyoidhinisha yale manunuzi wakati ule!
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!
0bfc1bc264eaf8714b1f1f9e717fad6b.jpg

Huko si kuwatega. Ninaomba hoja hii ya Richmond, irudishwe bungeni, mzee wa watu apumzike.

Siyo Richmond tu. Ninaomba maufisadi yote hata aliyoyasema juzi CAG, yote yajadiliwe bungine kieleweke mafisadi wako wapi kati ya CCM na upinzani.

Na isiwe mijadala ya kupoteza muda. Maazimion mazito yafikiwe ikiwemo kurudishwa kwa fedha zilizokwibwa na adhabu zingine wastahlizo majizi.

Tumechoka na ngonjera za hawa ccm.
 
Kwa kulirejesha tena bungeni, nadhani hataishia kuhusu uhusika wa Lowasa, bali pia kupitia utekelezaji wa maamuzi ya Bunge.
Wanairejeshaje. Kama hoja mpya ama kama ni hoja ile ile ambayo Mwakyembe alisema wameficha mengine kuzuia serikali isianguke? Na serikali ni nani kama waziri Mkuu walitaka ajipime? Unapotaka kurudisha hoja ile Bungeni ni lazima na Kikwete arudi tena madarakani, ili ukweli wote usemwe na tuone kama serikali itaanguka ama itapona!!
 
Upuuzi halafu watu wanashangilia....ni serikali gani ilikuwepo wakati huo na sasa ni serikali ya chama gani.....
Waziri anaongea upuuzi watu sababu ya ushabiki wa vyama.
Upuuzi kabisa
 
Mara hii Mwakyembe anawalaza watu na viatu ...yaani ni bampa tu bampa!
Hivi kwa swala la Richmond aibu ni ya nani ?! Siyo serikali (CCM) iliyoshindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa ?! Wenye dola ni CDM kweli ?! au huyu Mwakyembe mi ndiyo simuelewi !!! Nchi ikiwa viongozi wasanii aina hii maendeleo ni ndoto
 
MH Dr mwakyembe unataka upande wetu mafuliko yapungue 2020
Kanali hii hoja ni ya kitoto kabisa. Yaani mtu alipewa nafasi ya kusema kila alichokijua na hakusema halafu anakuja miaka 9 baadaye anasema anataka kusema na watu wanamshangilia. Hivi vichwa vyetu vimebeba nini ndani yake!?

Kuna ulazima gani wa kusema mpaka hoja irudishwe bungeni? Sia aseme tu anachokijua na watu watamsikia. Kwani wakati anasema kalishwa sumu alisubiri kusemea bungeni?
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!
0bfc1bc264eaf8714b1f1f9e717fad6b.jpg

Nilijua serikali itampeleka kwenye mahakama ya mafisadi.
 
Back
Top Bottom