Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Fumbo mfumbie mjinga mwerevu hung'amua.

Baadhi ya makamanda wa CHADEMA (hasa CHADEMA asilia) hawaitaki ndoa ya kisiasa kati ya Mbowe na Lowasa, sasa watoke vipi ni jinsi ya kuirudisha suala RICHMOND bungeni.

Mwakyembe naye kawatega waingie vichwa vichwa. Likiachwa kurudishwa bungeni, basi yatosha CHADEMA kuthibitishiwa kuwa waliyekuwa wakimtuhumu, kwenye majukwaa kuwa ni fisadi, kweli ni fisadi.

Hivyo hoja yao, ya kila siku kila akitajwa kuhusika na ufisadi, ati mwenye ushahidi atoe afikishwe mahakamani, haitakuwa na nguvu tena. Kwanza, kwa yeye kujiuzuru Uwaziri Mkuu, ilikuwa adhabu tosha kwa mtu mwenye uchu wa madaraka, kama yeye.
Mkuu kuna kitu sikielewi hivi ina maana serikali inashindwa yenyewe binafsi kumburuza lowassa mahakamani mpaka upinzani eti wairudishe bungeni?? Kma lowasa ana machafu kafanya basi sheria ichukue mkondo wake ssa hivi vitisho toka 2015 mara ooh mahakama ya mafisadi sijui fisadi papa huku mahakama na polisi ni yenu ssa kumkamata mnaogopa nni???
 
Ukitaka utukanwe humu jf, ligusie swala la RICHMOMD, DOWANS na MTUKUFU LOWASA. Siasa zetu zimejaa unafiki, upinzani kwa kipindi cha miaka nane walikuwa WANAICHUKIA NYAMA YA NGURUWE ALAFU MWISHO WA SIKU, WAKAAMUA WAUNYWE MCHUZI WAKE , kwa hiyo si shangai watu waliomtukana LOWASA kwa miaka nane na kwa vinywa vyao walisema walikuwa na ushahidi kwamba jamaa ni fisadi, bila kusahau series zile za Bw Kubenea na MWANAHALISI za kila siku kumchambua Lowasa juu ya ufisadi wa RICHMOMD na DOWANS na kama haitoshi akamtuhumu LOWASA na ROSTAM wanahusika ktk kumwekea sumu Mwakyembe , leo hii eti LOWASA mtakatifu si UNAFIKI huu. Wanasiasa wametugeuza kama SIGARA KALI, sijui wametuona sisi watoto wadogo, ila si shangai kwani hata huyu wanaemwita BASHITE, siku akiwa kwao watamwita KIJANA SHUJAA MH PAUL MAKONDA, ndio siasa zetu FULL UNAFIKI.

Mpelekeni kwenye mahakama ya mafisadi. Mahakama imekaa bure tu.
 
Kha! Ndo mnamuita Dr huyo, mbona hoja zake hazina mashiko na hazistahili kuongelewa na mtu mwenye hadhi-cheti cha PHD achilia mbali nafasi aliyonayo ya uwaziri.

My take: Atumwe India kwa matibabu haraka sana, mana naona ile sumu imekula kaubongo kaliko kabakia kazima kale daaah
Tanzania pekee ndo diploma holder na degree holder wana kiburi cha kutukana pHd holder ...mnataka msikie kitu mnachokipenda mazezeta akili zenu zipo matakoni hama.
 
Si mliunda Mahakama ya Mafisadi sasa mnashindwa nini kumshitaki ili hali mwenyewe alishasema mwenye ushahidi aende Mahakamani?
Kwa hivo chadema hawakuwa na ushahid wa ufisadi wake?
 
Ukitaka utukanwe humu jf, ligusie swala la RICHMOMD, DOWANS na MTUKUFU LOWASA. Siasa zetu zimejaa unafiki, upinzani kwa kipindi cha miaka nane walikuwa WANAICHUKIA NYAMA YA NGURUWE ALAFU MWISHO WA SIKU, WAKAAMUA WAUNYWE MCHUZI WAKE , kwa hiyo si shangai watu waliomtukana LOWASA kwa miaka nane na kwa vinywa vyao walisema walikuwa na ushahidi kwamba jamaa ni fisadi, bila kusahau series zile za Bw Kubenea na MWANAHALISI za kila siku kumchambua Lowasa juu ya ufisadi wa RICHMOMD na DOWANS na kama haitoshi akamtuhumu LOWASA na ROSTAM wanahusika ktk kumwekea sumu Mwakyembe , leo hii eti LOWASA mtakatifu si UNAFIKI huu. Wanasiasa wametugeuza kama SIGARA KALI, sijui wametuona sisi watoto wadogo, ila si shangai kwani hata huyu wanaemwita BASHITE, siku akiwa kwao watamwita KIJANA SHUJAA MH PAUL MAKONDA, ndio siasa zetu FULL UNAFIKI.
Hahah mkuu haupo siriaz, Bashite aende ukawa alafu aitwe shujaa!!?? Nadhani mkuu haupo sawa
 
Mbona ukweli unajulikana toka zamani kuwa ukweli wa ufasadi wa Richmond ungetolewa kama inavyotakiwa,Lowassa asingekuwa mbuzi wa kafara wenye Richmond wangeweza kuwajibika na Richmond Yao.
 
Hii kali, safi sana Waziri unajua awamu hii itanyoosha tu na wanajua

Natega sikio kusikilizia na kukodoa macho nione watajibuje au ndio watakaa kimyaaa

Ha ha ha haaaaaa

Hapa kazi tu
 
Mwakyembe sema ukweli , tunazo taarifa zote kuhusu safari yako ya Marekani , tunawafahamu hata waliokuwa wanakutembeza , walipogundua uongo wako wakakushiti , ulitumwa kufunika kombe , UNABISHA , NIFUKUE MAKABURI ? tena aliyekuwa anakuzungusha ni mlokole mmoja mwenye asili ya kiafrica , natoa wito kwa wabunge wa Chadema kuirudisha bungeni hoja hii , Mwakyembe atakimbia .
Teh, naona unataka ndoa ya chadema na lowassa ife
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!
0bfc1bc264eaf8714b1f1f9e717fad6b.jpg
Kwani Mahakama.ya mafisadi imefutwa?
 
Huu upuuzi wa wanasiasa uchwara wa kucheza na Akili za wadanganyika naona unazidi kukita mizizi kwa viongozi wa serikali ya awamu hii! Yaani badala ya kuishauri serikali suala la Richmond lipelekwa mahakami yeye analeta upuuzi wa siasa za majitaka eti lipelekwe tena bungeni!!!!
 
Kwa mara ya kwanza Chadema wataanza kuitetea Richmond...
Mkuu ulisoma hotuba ya waziri kivuli mnyika kuhusu maazimio ya bunge kuhusu richmond??? Hivi na wwe unaamini chadema wangemchukua lowassa kama wanajua mwisho wa siku HE IS A CRIMINAL na atakamatwa??? R they that dumb???

Najua humkubali lowassa ila ukiweka ushabiki pembeni na ukiangalia kwa picha kubwa utagundua ukweli wa mambo
 
Inamaana mahakama ya mafisadi mtafugia popo mpaka lini??

Mwakyembe akili yake ilinyonyoka na zile nyusi kipindi kilee.
Ubongo ulitikiswa kidogo kha maana haya majibu ndivyo sivyo. Arudishe Richmond kama Lowassa atakutwa na hatia sheria ichukue mkondo wake sio kufichiana maovu. Bashite likewise!
 
Huu upuuzi wa wanasiasa uchwara wa kucheza na Akili za wadanganyika naona unazidi kukita mizizi kwa viongozi wa serikali ya awamu hii! Yaani badala ya kuishauri serikali suala la Richmond lipelekwa mahakami yeye analeta upuuzi wa siasa za majitaka eti lipelekwe tena bungeni!!!!
Acha hasira! Rudisheni hoja bungeni vinginevyo ninyi ni ndumi la kuwili.
 
Yaani wakati Lowassa yupo Bungeni alisema mambo nusunusu, leo Lowassa hayupo Bungeni anajidai jambo lirudishwe Bungeni. Hivi alipokuwa Waziri wa Sheria si ndiyo ilikuwa nafasi yake ya kulimaliza suala hilo kwenye Mahakama ya Mafisadi ambako ndiko na Lowassa angepata nafasi ya kujitetea?
 
Back
Top Bottom