Mkuu mimi naeleza mawazo yangu, kwahiyo kama wewe unaona ni sawa kuwaamini basi sawaWapinzani hawatuchezei akili acha kuwasingizia. Wanaotuchezea akili ni wale ambao tumewapa ridhaa ya kutuongoza na kuhakikisha kila mtu anatendewa kwa haki, na hawafanyi hivyo. Acha kuwapandisha hadhi wapinzani kwenye mambo ya ovyo. Put the blame where it belongs.
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.
Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!
Dk Mwakyembe, Nassari wapimana
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.
Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.
Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”
Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.
“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.
Chanzo: Mwananchi
Mkuu mimi naeleza mawazo yangu, kwahiyo kama wewe unaona ni sawa kuwaamini basi sawa
Na wewe pia tumia akili!Kwani kwa akili yako ni nani waliofanya figisu ambao huyo Mwakayembe anawaambia warudishe suala Bungeni?? Kwa nini hajaomba suala ya ESCROW lirudishwe pia???? au lenyewe halikuwa na figisu? Tumia akili kidogo tuu, hii siyo wala rocket science.
Kwani selikali haikuanguka? Lowasa alijiuzulu u pm, ndio kusema sekikali iliangukaSi ni huyu huyu Mwakyembe aliyesema kwamba angesoma report your Serikali ingeanguka?
Alikuwa anaficha nini,sasa anapata wapi guts now?
Kama ushahidi upon wampeleke mahakamani tujue mbivu na mbichi...lakini so kutaka kuhamisha mijadala ya binge kwa sasa wakati serikali inafail
Sasa fikiri bashite aje huko chadema alafu mmpe VIP treatment! Si mtakuwa wajinga wakutupwa?Hata leo tunawaambia kuna mtu anaitwa Daudi Bashite anafanya kazi kwa kutumia "mavyeti" feki, but they never do anything or take any action as usual. Wanasubiri Bashite ahame chama chao ndio waanze nao kumwandama kwa vyeti feki???? You cannot be a reasonable ruling party by doing all the wrong things...Ni lazima tuwaambie ukweli hata kama unauma.
Na wewe pia tumia akili!
Nasari hakuhoji ishu ya escrow, alihoji suala la richmond akionesha kwamba Lowassa alionewa ndio maana mwakyembe akamjibu hivyo!
Fuatilia mambo kwa umakini.
Sasa fikiri bashite aje huko chadema alafu mmpe VIP treatment! Si mtakuwa wajinga wakutupwa?
Huyo Mwakyembe kichwa chake kilishaharibika yupo yupo tu. Ni mgonjwa huyo. Kipindi cha Richmond yeye ndie alikuwa mwenyekiti wa kamati alishindwa nini kueleza yote. Leo anatujia na porojo za alfu lelaulela. Mwakyembe anayotamaa ya madaraka tangu kipindi cha Richmond aliaidiwa uwaziri akashindwa kutoa ripoti akachapiachapia. Leo anatujia na mafangas yake eti rudisheni Richmond. Miaka 20 inaenda alikuwa wapi kueleza. Umewadhalilisha sana wanyakyusa unapenda madaraka huwezi kusimamia ukweli unapinda kama benderaWaziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.
Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!
Dk Mwakyembe, Nassari wapimana
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.
Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.
Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”
Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.
“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.
Chanzo: Mwananchi
Mkuu hao ndio wanasiasa wa siasa majitaka tulionao nchi hii!mimi nafikiri ili swala sio la chadema ni la nchi mwakyembe amekua waziri wa katiba na sheria lakini hakuwahi ongelea swala la richmond sasahivi kabwana na ansad ndo anaanza kusema kama chadema wana ushahidi warudishe swalala richmond mezani swali kwanini mwakyembe mwenyewe asirudishe swala la richmond kama anaona lowasa alitakiwa kushughulikiwa na aliachwa pili kwa nini serikali isifungue kesi dhiidi ya lowasa kuhusu richmond ilo ndo swala lamsingi kwenye mahakama ya mafisadi mwakyembe alisema hakuna fisadi sasa tunakuomba mwakyembe ufungue mashtaka mahakamani ili lowasa akikutwa na ushahidi afungwe kabisa
mwakyembe bunge sio mahakama na haliwezi kumfunga lowasa kwakua ww nimwanasheria mahiri fungua kesi ya richmond hapoi utakua umelitendea haki taifa tumechoka maneno ya kisiasa tunataka action kamanikufungwa basi afungwe sio mnaleta maneno maneno hayana mana
Aloufungua mjadala huo ni nasari uyo mbunge kijanaHii serikali ijiuzulu tu.
Yaani wao ndio wameshika dola na wao ndio waliofunga huo mjadala Bungeni alafu leo ndio wanaowataka wapinzani waibue swala hilo badala ya kutekeleza maazimio ya Bunge au kufungua kesi Mahakamani.
Pathetic!
vigeu geu kama kinyonga, lowasa hasafishiki, wewe ulitaka alete hoja ipi ili uione inamashikoKha! Ndo mnamuita Dr huyo, mbona hoja zake hazina mashiko na hazistahili kuongelewa na mtu mwenye hadhi-cheti cha PHD achilia mbali nafasi aliyonayo ya uwaziri.
Hivi unajua tunachojadili hapa?That is the problem, you don't think outside the box. You narrow your thinking and fit yourself into Chadema's patter of doing things. Unataka nikukumbushe kwamba Chadema hawana nchi wanayoitawala katika Afrika au utajiongeza mwenyewe baadaye???
Inamana huyo Dr alilidanganya bunge na taifa!?vigeu geu kama kinyonga, lowasa hasafishiki, wewe ulitaka alete hoja ipi ili uione inamashiko
Una maana gani mkuu kwa hili neno lair!????? Nijuavyo mimi maana ya hili neno ni mahali ambapo wanyama wa porini wanaishi sasa sijui unaunganishaje na Mwakyembe na mnyama wa porini????? Ungeamua kutumia lugha moja tu ambayo unayoielewa kamili iwe kidhungu ama kimang'ati usingejichanganya namna hii. Usiwe kama ma surrogate wa Donald Fred Trump wakibanwa wanarudisha habari za Obama. Hapa kaulizwa juu ya Richmond wewe unataka ajibu kuhusu ESCROW halafu unataka kudharau IQ za wenzako wakati wewe IQ ya kwako ni questionable.This guy is a lair! Anaomba kesi ya Richmond kwa sababu anataka kufanya siasa. Ni chama chake mwenyewe ndicho kilichoiua hoja hiyo Bungeni wakati ule, and he should be ashamed of what he is saying. Kwa nini asililie kesi ya ESCROW ambayo ni ya juzi tu, akarudishwa Bungeni ili aonyeshe ushujaa wake??? we say it everyday... ukiwa kwenye hiki chama unakumbwa na tatizo la IQ yako kushuka kila siku....