Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hakuna cha ajabu. Rais Samia atafanya yote atakayotakiwa kufanya. Kama ni kubusu pete, atafanya. Kama ni magoti atapiga.
Hata Papa akiingia msikitini, atavua viatu. Kule Saudi Arabia, aliendesha misa ndani ya msikiti.
Kwanza wale waislam wanaofuata kwa umakini mafundisho ya Mtume, katika msingi wa imani, Waislam hawapo mbali na ukristo:
Wote wanasema Mungu ni mmoja tu na ana uwezo wote. Tofauti ipo tu kwenye utatu mtakatifu, kitu ambacho waislam hawakubali.
Wote wanaamini Yesu mimba yake ilitungwa kwa muujiza, wote wanakubali Yesu alitenda miujiza mingi. Wote wanakubali kuwa Yesu atarudi tena Duniani siku za mwisho. Tofauti ni pale ambapo Wakristo wanaamini Yesu ni nafsi kamili ya Mungu, na kuwa alikufa msalabani na kufufuka. Waislam wanaamini Yesu (Isa) hakusulibiwa msalabani, siyo nafsi ya Mungu bali ni nabii wa ngazi ya juu. Mtume Muhamad anasema kuwa yeye ni mfuasi namba moja wa Nabii Isa bin Mariam. Lakini waislam wasioijua Kurani wanamtusi Yesu ambaye Muhamad anasema kuwa ni mfuasi wake namba moja.
Kule India kuna Kanisa ambalo linawapa nafasi waislam kulitumia kanisa hilo kwa swala siku ya Ijumaa. Na jamii nzima, wakristo na waislam, wote wanaliona kanisa hilo ni nyumba yao ya kumwabudia Mungu wao.