Mwalimu aliyetoweka Simiyu akutwa amefariki Musoma

Mwalimu aliyetoweka Simiyu akutwa amefariki Musoma

Hii taarifa imeniumiza sana,Monica ni classmate wangu wa Olevel,alikuwa ni yatima pia.Ameacha simanzi kwa mtoto wake ambae ni mdogo sana na familia pia.Sijui nini kimekukuta Monica lakini hata kwenye group letu la whtasaap la Oleve tutakumiss pia maana ulikuwa active member.

Rest well mate
Imagine katika mazingira ya aina hiyo, halafu mtu analeta taarifa huku akikejeli. Kisa tu huyo marehemu alikuwa ni mwalimu. This is totally unfair.

Huyu dogo Mwenyezi Mungu amrehemu.
 
Angekuwa analeta hoja angejibiwa, wewe nawe unaonekana tuu chuki moja na mtoa mada, yaani kwa akili yako unaona kabisa anatoa hoja? Hujiulizi kwanini kila mtu anamlalamikia? If possible update your IQ brother, huu upumbavu
Mkuu mbona mimi sina chuki na mualimu Baba angu alikua mualimu japo aliacha mapema Mjoba angu ni mualimu secondary,.... mimi nacho semea nyie waalimu mlimesoma mambo mengi kama saikolojia tumiani hiyo saikolojia mlio soma kumjibu huyu, bila kutumia matusi kama yeye.
 
Amekuwa na upumbavu na ujuha flani nadhani kuna watu walimsifia before. Imekuwa too much sasa. Anakosa heshima kabisa na kuonesha jinsi ambavyo ni mweupe kichwani. Sielewi anapitia changamoto gani kisaikolojia. Mimi amefikia hatua naona anakuwa kama ameathirika kiakili ana msongo wa mawazo n.k
Ameathirika kisaikolojia hata kwa mtu ambae hujasoma saikolojia unaliona hili
 
Waalimu mliomo humu naomba mjibu mpyayangu village ki hoja kwa kuonyesha umahili wenu, kurushiana matusi sio jibu, hapo mtakua mnafanana, yeye kama yeye tuhuma zake kwake zina ukweli na mashiko kwa% fulani, nyie ni wasomi tena waalimu counter- challenge him, sio kulilia mod kufuta uzi, naona huo ni udhaifu kwa upande wa waalimu, teteeni mwenzenu kwa hoja.
Mimi wala sina shida na Mpwayungu maana anayoyasema ni ya kweli
 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Monica Patrick (31) aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa ameuwawa na mwili wake kutelekezwa kichakani mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mara, Agostino Magere amethibitisha mwili huo kuopolewa kutoka kwenye kichaka kilichoko ndani ya maji pembezoni mwa Ziwa Victoria.

“Februari 19, 2023, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara tulipokea taarifa ya mwili wa mtu kuonekana ikielea juu ya maji kwenye kichakani kilichopo mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma na kweli tullipofika tuliukuta na kuuopoa ukiwa umeharibika.

“Marehemu ametambulika kwa jina la Monica Patrick aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya msingi mkoani Simiyu,” amesema Kamanda Magere

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Februari 20, 2023, Kamanda huyo wa Zimamoto na Uokoaji amesema mwili wa Mwalimu Monica umekabidhiwa kwa wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi kubaini chanzo cha kifo chake.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyang’wena, Selemani Makanja amesema taarifa za awali zinadai Mwalimu Monica ambaye ndugu zake wametoa tangazo la kutoweka kwake kupitia njia ya mitandao ya kijamii alifariki dunia baada ya kunyweshwa dawa na mtu anayeaminika kuwa ni mganga wa kienyeji kwa lengo la kufanikiwa kibiashara.

“Inasemekana marehemu ambaye pia tumeelezwa kwamba ni mwalimu huko mkoani Simiyu alikwenda kwa mganga huyo kwa lengo la kuaguliwa ili afanikiwe katika biashara yake ya madini. Tunasubiri taarifa za uchunguzi kujua chanzo cha kifo,” amesema.

Amesema mwili wa merehemu Monica umekutwa eneo la mradi wa majitaka ambao haujakamilika, huku akiiomba Serikali kukamilisha mradi huo kuondoa kichaka ambacho kimegeuka kuwa

Kupitia mitandao ya kijamii, familia ya Mwalimu Herman Mlale wa Sanya Juu Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ilitangaza kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa mtoto wao Monica Patrick, ikiomba mwenye taarifa ama kuwasiliana na familia hiyo kupitia namba tatu za simu zilizoambatana na tangazo hilo au kituo chochote cha polisi.

Taarifa zilizoifikia Mwananchi zinaeleza kuwa mwili wa Mwalimu Monica tayari umewasili nyumbani kwao Sanya Juu ambako mazishi yanatarajiwa kufanyika leo kutokana kuharibika.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai mwalimu Monica ambaye haijajulikana iwapo alikuwa akijihusisha ba biashara ya madini kama inavyoelezwa baada ya kifo chake, alitoweka muda mfupi baada ya kupokea fedha za mkopo kiasi cha Sh5 milioni kutoka katika moja ya taasisi za fedha mkoani Simiyu.

Chanzo: Mwananchi
Sijui kwa nini dunia haina ubinadamu
 
Na huyu jamaa Mpwayungu village na kejeli zote Kwa walimu ila siku mtoto wake akifika umri wa kwenda shule ataenda kumkabidhi mtoto wake wa walimu hao hao anaowaita mapoyoyo.

Na aje hapa atambe kuwa haitatokea hata siku Moja mtoto wake atakuwa chin ya uangalizi wa hao walimu anaowatukana Kila siku. It's obvious huyu jamaa ana Shida kubwa na bahati mbaya sana kwake hajui kama ana Shida.

Kale kautafiti kaliko sema katika Kila watz 4 mmoja ana kichaa Mpwayungu yupo next level huyu anabeba watu 18.😂😂😂
 
Back
Top Bottom