Mwalimu aliyetoweka Simiyu akutwa amefariki Musoma

Mwalimu aliyetoweka Simiyu akutwa amefariki Musoma

Acha yafe, hayajielewi ni maoga ukiwaambia yaandamane ya naogopa kufa nakati kifo ni Natural death, sasa Mungu anaamua kujibu Kwa vitendo nawatapukutika
wewe umeandamana? Au kazi kung'ang'aniza wengine. Kazi ya CHADEMA ni kuwatumia wengine kwa kazi zao chafu. Ndiyo maana hamtafanikiwa, mkiwa na uchungu wa kweli waambie wanachama wenu waandamane. Siko tayari kuumia kwa sababu ya CHADEMA kupata madaraka. Waandamane wenyewe, siyo kazi kushawishi huku watoto wao wamewaficha Ulaya/Dubai. Wakisha pata madaraka wataiwaita watototowao wawepe ulaji.
 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Monica Patrick (31) aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa ameuwawa na mwili wake kutelekezwa kichakani mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mara, Agostino Magere amethibitisha mwili huo kuopolewa kutoka kwenye kichaka kilichoko ndani ya maji pembezoni mwa Ziwa Victoria.

“Februari 19, 2023, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara tulipokea taarifa ya mwili wa mtu kuonekana ikielea juu ya maji kwenye kichakani kilichopo mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma na kweli tullipofika tuliukuta na kuuopoa ukiwa umeharibika.

“Marehemu ametambulika kwa jina la Monica Patrick aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya msingi mkoani Simiyu,” amesema Kamanda Magere

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Februari 20, 2023, Kamanda huyo wa Zimamoto na Uokoaji amesema mwili wa Mwalimu Monica umekabidhiwa kwa wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi kubaini chanzo cha kifo chake.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyang’wena, Selemani Makanja amesema taarifa za awali zinadai Mwalimu Monica ambaye ndugu zake wametoa tangazo la kutoweka kwake kupitia njia ya mitandao ya kijamii alifariki dunia baada ya kunyweshwa dawa na mtu anayeaminika kuwa ni mganga wa kienyeji kwa lengo la kufanikiwa kibiashara.

“Inasemekana marehemu ambaye pia tumeelezwa kwamba ni mwalimu huko mkoani Simiyu alikwenda kwa mganga huyo kwa lengo la kuaguliwa ili afanikiwe katika biashara yake ya madini. Tunasubiri taarifa za uchunguzi kujua chanzo cha kifo,” amesema.

Amesema mwili wa merehemu Monica umekutwa eneo la mradi wa majitaka ambao haujakamilika, huku akiiomba Serikali kukamilisha mradi huo kuondoa kichaka ambacho kimegeuka kuwa

Kupitia mitandao ya kijamii, familia ya Mwalimu Herman Mlale wa Sanya Juu Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ilitangaza kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa mtoto wao Monica Patrick, ikiomba mwenye taarifa ama kuwasiliana na familia hiyo kupitia namba tatu za simu zilizoambatana na tangazo hilo au kituo chochote cha polisi.

Taarifa zilizoifikia Mwananchi zinaeleza kuwa mwili wa Mwalimu Monica tayari umewasili nyumbani kwao Sanya Juu ambako mazishi yanatarajiwa kufanyika leo kutokana kuharibika.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai mwalimu Monica ambaye haijajulikana iwapo alikuwa akijihusisha ba biashara ya madini kama inavyoelezwa baada ya kifo chake, alitoweka muda mfupi baada ya kupokea fedha za mkopo kiasi cha Sh5 milioni kutoka katika moja ya taasisi za fedha mkoani Simiyu.

Chanzo: Mwananchi
Inasemekana marehemu ambaye pia tumeelezwa kwamba ni mwalimu huko mkoani Simiyu alikwenda kwa mganga huyo kwa lengo la kuaguliwa ili afanikiwe katika biashara yake ya madini. Tunasubiri taarifa za uchunguzi kujua chanzo cha kifo,” amesema.
 
Nipo hospital ya mkapa apa dodoma
Nikupe pole tena nakupa pole, pesa ninayo ingiza hapa Kariakoo kwenye biashara yangu ya makapeti na mapazia ya nyumbani ni zaidi ya million saba Kwa mwezi hiyo sio profit ni NET PROFIT
Hapa umeniacha njia panda CHIEF, ni kwamba unapiga kaz hospital dom na huku kariakoo unauza makapeti?
 
Mwl. Shule ya Msingi iliyopo Wilaya ya Itimila huko mkoani Simiyu.......

Naomba kuuliza kwani mwanadamu ukiridhika unapungukiwa na nini??? Mpaka kwa Mganga, halooo wachagga bado wana hii tabia.

R.I.P MWL. MONICA PATRICK.
 
Wengi tuliocomment kwenye huu uzi ni walimu
Waalimu mliomo humu naomba mjibu mpyayangu village ki hoja kwa kuonyesha umahili wenu, kurushiana matusi sio jibu, hapo mtakua mnafanana, yeye kama yeye tuhuma zake kwake zina ukweli na mashiko kwa% fulani, nyie ni wasomi tena waalimu counter- challenge him, sio kulilia mod kufuta uzi, naona huo ni udhaifu kwa upande wa waalimu, teteeni mwenzenu kwa hoja.
 
Maiti ipo kwenye maji. Pia umefupisha kulitaja kwa kirefu linaitwa jeshi la zimamoto na uokoaji
Wakishaopoa mwili ni kazi ya jeshi la polisi kufanya logistics zake kwa sababu kuna mambo kadhaa yanayohusu scemario na kuchukua maelezo ya awali na kwenda kusimamia postmoterm....
 
Waalimu mliomo humu naomba mjibu mpyayangu village ki hoja kwa kuonyesha umahili wenu, kurushiana matusi sio jibu, hapo mtakua mnafanana, yeye kama yeye tuhuma zake kwake zina ukweli na mashiko kwa% fulani, nyie ni wasomi tena waalimu counter- challenge him, sio kulilia mod kufuta uzi, naona huo ni udhaifu kwa upande wa waalimu, teteeni mwenzenu kwa hoja.
Angekuwa analeta hoja angejibiwa, wewe nawe unaonekana tuu chuki moja na mtoa mada, yaani kwa akili yako unaona kabisa anatoa hoja? Hujiulizi kwanini kila mtu anamlalamikia? If possible update your IQ brother, huu upumbavu
 
Hii taarifa imeniumiza sana,Monica ni classmate wangu wa Olevel,alikuwa ni yatima pia.Ameacha simanzi kwa mtoto wake ambae ni mdogo sana na familia pia.Sijui nini kimekukuta Monica lakini hata kwenye group letu la whtasaap la Oleve tutakumiss pia maana ulikuwa active member.

Rest well mate
 
Back
Top Bottom