Imagine katika mazingira ya aina hiyo, halafu mtu analeta taarifa huku akikejeli. Kisa tu huyo marehemu alikuwa ni mwalimu. This is totally unfair.Hii taarifa imeniumiza sana,Monica ni classmate wangu wa Olevel,alikuwa ni yatima pia.Ameacha simanzi kwa mtoto wake ambae ni mdogo sana na familia pia.Sijui nini kimekukuta Monica lakini hata kwenye group letu la whtasaap la Oleve tutakumiss pia maana ulikuwa active member.
Rest well mate
Mualimu kuna rafiki yangu iko shule moja inaitwa mputwa mkoa Lindi Dc, uko ni wapi? natamani kuenda kumtembelea kwasbb ni mda nasikia hamna mawasiliano uko.Mimi pia mwalimu,nafundisha shule ya msingi Mpigamiti Liwale-Lindi
Mkuu mbona mimi sina chuki na mualimu Baba angu alikua mualimu japo aliacha mapema Mjoba angu ni mualimu secondary,.... mimi nacho semea nyie waalimu mlimesoma mambo mengi kama saikolojia tumiani hiyo saikolojia mlio soma kumjibu huyu, bila kutumia matusi kama yeye.Angekuwa analeta hoja angejibiwa, wewe nawe unaonekana tuu chuki moja na mtoa mada, yaani kwa akili yako unaona kabisa anatoa hoja? Hujiulizi kwanini kila mtu anamlalamikia? If possible update your IQ brother, huu upumbavu
Duh Mimi Niko liwale mkuu,ni mbali kwenda lindi DCMualimu kuna rafiki yangu iko shule moja inaitwa mputwa mkoa Lindi Dc, uko ni wapi? natamani kuenda kumtembelea kwasbb ni mda nasikia hamna mawasiliano uko.
Loh!! kwahiyo una nishauri je? Niachana nae au nikija na ka baby walker kangu katamudu njia za huku, nasikia serikali ilisha wasahau sana uko kimaendeleo barabara na miundombinu zingine.Duh Mimi Niko liwale mkuu,ni mbali kwenda lindi DC
Inaumiza sana mkuu,kwake yeye marehemu alikuwa Mwal lakini kwangu Monica ni zaidi ya MwalImagine katika mazingira ya aina hiyo, halafu mtu analeta taarifa huku akikejeli. Kisa tu huyo marehemu alikuwa ni mwalimu. This is totally unfair.
Huyu dogo Mwenyezi Mungu amrehemu.
Ndiyo,mgomo unaweza kuleta mabadiliko lkn Mwl akiangalia watu walioko nyuma yake,hapo bado Chama cha Wanyonyaji Tanzania (CWT) akijafanya njama zake za uwakala wa kuwafitinisha na Serikali,ebu vaa uhusika alafu ulete majibu.Kwanini wasifanye mgomo na kuandamana ili wadai haki zao waachane na Roho za uoga
Ameathirika kisaikolojia hata kwa mtu ambae hujasoma saikolojia unaliona hiliAmekuwa na upumbavu na ujuha flani nadhani kuna watu walimsifia before. Imekuwa too much sasa. Anakosa heshima kabisa na kuonesha jinsi ambavyo ni mweupe kichwani. Sielewi anapitia changamoto gani kisaikolojia. Mimi amefikia hatua naona anakuwa kama ameathirika kiakili ana msongo wa mawazo n.k
Mimi wala sina shida na Mpwayungu maana anayoyasema ni ya kweliWaalimu mliomo humu naomba mjibu mpyayangu village ki hoja kwa kuonyesha umahili wenu, kurushiana matusi sio jibu, hapo mtakua mnafanana, yeye kama yeye tuhuma zake kwake zina ukweli na mashiko kwa% fulani, nyie ni wasomi tena waalimu counter- challenge him, sio kulilia mod kufuta uzi, naona huo ni udhaifu kwa upande wa waalimu, teteeni mwenzenu kwa hoja.
Shida ipo tena kubwa sana.Moyo wake umejaa hasira na hana pa kuzitolea zaidi ya kuja hapa Jukwaani na kuanza bullying na bahati mbaya sana Walimu ndiyo wamekuwa wahanga wa depression aliyo nayo.Ameathirika kisaikolojia hata kwa mtu ambae hujasoma saikolojia unaliona hili
Jamaa ana shida kubwa ni kama kuna laana flani ameipata.Ameathirika kisaikolojia hata kwa mtu ambae hujasoma saikolojia unaliona hili
Jamaa ana shida kubwa ni kama kuna laana flani ameipata.Ameathirika kisaikolojia hata kwa mtu ambae hujasoma saikolojia unaliona hili
Acha kiburi cha uzima!!!!Hali ngumu kwako, mm nina Prado mpyaa namba E Nina nyumba pesa za kutosha
Sijui kwa nini dunia haina ubinadamuMwalimu wa Shule ya Msingi Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Monica Patrick (31) aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa ameuwawa na mwili wake kutelekezwa kichakani mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mara, Agostino Magere amethibitisha mwili huo kuopolewa kutoka kwenye kichaka kilichoko ndani ya maji pembezoni mwa Ziwa Victoria.
“Februari 19, 2023, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara tulipokea taarifa ya mwili wa mtu kuonekana ikielea juu ya maji kwenye kichakani kilichopo mtaa wa Nyang’wena Manispaa ya Musoma na kweli tullipofika tuliukuta na kuuopoa ukiwa umeharibika.
“Marehemu ametambulika kwa jina la Monica Patrick aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya msingi mkoani Simiyu,” amesema Kamanda Magere
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Februari 20, 2023, Kamanda huyo wa Zimamoto na Uokoaji amesema mwili wa Mwalimu Monica umekabidhiwa kwa wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi kubaini chanzo cha kifo chake.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyang’wena, Selemani Makanja amesema taarifa za awali zinadai Mwalimu Monica ambaye ndugu zake wametoa tangazo la kutoweka kwake kupitia njia ya mitandao ya kijamii alifariki dunia baada ya kunyweshwa dawa na mtu anayeaminika kuwa ni mganga wa kienyeji kwa lengo la kufanikiwa kibiashara.
“Inasemekana marehemu ambaye pia tumeelezwa kwamba ni mwalimu huko mkoani Simiyu alikwenda kwa mganga huyo kwa lengo la kuaguliwa ili afanikiwe katika biashara yake ya madini. Tunasubiri taarifa za uchunguzi kujua chanzo cha kifo,” amesema.
Amesema mwili wa merehemu Monica umekutwa eneo la mradi wa majitaka ambao haujakamilika, huku akiiomba Serikali kukamilisha mradi huo kuondoa kichaka ambacho kimegeuka kuwa
Kupitia mitandao ya kijamii, familia ya Mwalimu Herman Mlale wa Sanya Juu Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ilitangaza kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwa mtoto wao Monica Patrick, ikiomba mwenye taarifa ama kuwasiliana na familia hiyo kupitia namba tatu za simu zilizoambatana na tangazo hilo au kituo chochote cha polisi.
Taarifa zilizoifikia Mwananchi zinaeleza kuwa mwili wa Mwalimu Monica tayari umewasili nyumbani kwao Sanya Juu ambako mazishi yanatarajiwa kufanyika leo kutokana kuharibika.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai mwalimu Monica ambaye haijajulikana iwapo alikuwa akijihusisha ba biashara ya madini kama inavyoelezwa baada ya kifo chake, alitoweka muda mfupi baada ya kupokea fedha za mkopo kiasi cha Sh5 milioni kutoka katika moja ya taasisi za fedha mkoani Simiyu.
Chanzo: Mwananchi
Duu....mkuu nikaribishe nami huko nipigemiti kisawasawa.Mimi pia mwalimu,nafundisha shule ya msingi Mpigamiti Liwale-Lindi