Mwalimu aliyewahi kunyanyaswa na Mkurugenzi wa Tanga Jiji amefariki dunia

11 Juni 2021
Dodoma, Tanzania

'Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania'

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM anayehusika na uhusiano wa kimataifa, kanali (mstaafu) Ngemela Lubinga wakati akifunga semina ya uongozi kwa jukwaa la walimu wazalendo Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya chama

Waalimu nchini wameaswa na kada huyo wa CCM kanali Lubinga kuwa wavumilivu na kufanya kazi kwa uzalendo, uaminifu ,uadilifu na kuzingatia maadili ya taaluma zao
 
Kama aĺikuwa analipwa mshahara wake na anatekeleza majukumu yake vizuri, alikwenda kuomchongea mkuu wa shule ili iweje? Hizo zilizofujwa zilikuwa zake? Tulishuhudia 1.5 tilioni zinafujwa hadharani mbona hakujitokeza kumchongea mfujaji kama yeye alikuwa na machungu sana juu ya ufujaji? Kiufupi uhamisho bila malipo ilikuwa ni halali yake. NI MIMI CR WA SUA AGRIBUSINESS 2008-2011, MKARA MTIIFU NILIYEWAHI KUISHI ETHIOPIA
Aisee kweli shule zimefungwa ngoja zifunguliwe baadhi ya maoni duni yatoweke jukwaani
 
Mwalimu ambaye aliwahi kudhulumiwa fedha zake za uhamisho na akajibiwa vibaya na mkurugenzi wa Tanga Jiji amefariki dunia juzi na amezikwa leo mkoani Arusha.
Mwalimu huyo alinyimwa fedha za uhamisho na alipofika kwa mkurugenzi alijibiwa vibaya na kupoteza fahamu kisha kupelekwa hospitali kwa ambulance.
Hatahivyo hakuna uhusiano wa mojakwamoja katiya ya kifo hicho na ukandamizaji wa mkurugenzi,bali siku chache kabla ya mdai huyo kukata roho alikua anasema ataenda kumuomba mkurugenzi amlipe hela zake za uhamisho.
Mwalimu huyo alilazimika kuhamishwa shule kwani alipinga wizi uliofanywa na aliyekua Mkuu wa shule(jina kapuni) na akidai anabaraka zote za mkurugenzi. Waliamua wasimlipe mwalimu huyo hela zake za uhamisho kwa kumkomoa kisa ameeleza ukweli wote TAKUKURU wa namna ambavyo hela zilikua zinaibiwa na aliyekua mkuu wa shule.

Mkuu huyo wa shule alifanya ubadhirifu wa fedha za umma bila hofu yoyote akidai hana anayemuogopa kwani anabaraka za mkurugenzi na afisa elimu wake. Hata alipoiba baadhi ya hela alisema ametumwa na mkurugenzi na afisa elimu hivyo anawapelekea mgao wao wakubwa hao. Hata baada ya kesi kupelekwa TAKUKURU mkuu huyo wa shule aliendelea kuishi kama malaika kwani alipewa cheo na kwenda kufanya kazi katika ofisi ya afisa elimu sekondari kama sehemu ya kupongezwa kwa kuwa mwizi.

Pia afisa elimu taaluma aliyeibua wizi huo alinyanyasika na kuamua kuacha kazi kwa manyanyaso aliyopitia.Baadae aliyekua mkuu wa shule mwizi akapewa nafasi ofisini hapo na kukalia kiti cha afisa elimu taaluma aliyenyanyasika na kuamua kuacha kazi kwa mazingira magumu aliyopitia. Je kama afisa ananyanyasika mpaka aamue kuacha kazi unajua ni aina gani ya majaribu aliyopitia mama yule? Mtu mishi wa kawaida ananyanyasika kiasi gani kama afisa elimu taaluma wamemnyanyasa akaikimbia ofisi na kuamua kukaa tu nyumbani?
Haya yote Ummy anayajua na hachukui hatua kama mbunge tena na waziri mwenye dhamana.
Tanga haipo salama kabisa chini ya Mayeji na afisa elimu sekondari ndugu Gwakisa.
Mh. Rais elekeza vyombo vyako vifanye uchunguzi hali ni mbaya sana,rushwa ndio imetawala haki hakuna watu wako wameumizwa. Kama kwa Sabaya umeweza kwanini isiwe kwa Mayeji na Gwakisa?

Mkurugenzi Daud Mayeji nakukumbusha kwamba dhuluma haitakujenga bali itakubomoa na kukuletea balaa maishani. Kuanzia sasa huna baraka za Mungu.

Umeshirikiana na Afisa utumishi afisa elimu na washauri wako wengine kukandamiza walimu wanne katiya 17 uliowahamisha kisa hawaungi mkono wizi uliofanywa na aliyekua Mkuu wa shule ambaye ni mtu wako wa karibu sana. Ummy anajua na ameshindwa kulikabili tatizo hilo lililosababishwa na marafiki zake wa karibu sana. Mwalimu aliyeiba nirafiki sana wa Ummy Mwalimu

TAKUKURU wanazotaarifa za wizi huo na nizaidi ya mwaka na miezi takriban kumi lakini hakuna kinachoeleweka. Kila aliyetoa ushirikiano kwa TAKUKURU amenyanyaswa na mkurugenzi na afisa elimu. Maana yake nikwamba TAKUKURU wamekua sio waadilifu kwa kutoa siri za mahojiano kati yao na mashahidi.
Mamlaka husika ingilieni kati ukandamizaji wa mkurugenzi, afisa elimu na TAKUKURU Tanga Jiji.

Kwakua taifa na familia wamempoteza mtumishi na mpendwa wao,itoshe tu kusema,bwana ametoa naye ametwaa jina lake lihimidiwe, Aaaamin
Halafu Kuna watu wanapendekeza Ummy awe waziri mkuu.
Hivi mnaona hii nchi haina wenyewe?
 
R.IP MWALIMU...TUNZENI HUU UZI TUACHOSUBIRI NI KARMA TU KUFANYA KAZI YAKE..
 
1077B2ED-40B6-48A9-87AF-8327A471EE82.jpeg
 
Back
Top Bottom