Mwalimu asimamishwa kazi kwa kumtukana Rais Samia


Huyu hapa ndio Silinde, ex Chadema. Hapo mtu wa kumuonea huruma ni Lwakatare tu maana hakupendezwa kabisa na upuuzi uliokuwa ukiendelea.

Amandla...
 
Kwani Sasa ni nani na yupo wapi, ? Mbona kawapiga wafia chama, kitu chenye nchi kali kichwani,mkuu
Sasa hivi ni mwanachama kindakindaki wa Chama cha Mapinduzi na ni mbunge pia wa chama hicho. Hicho cha kuwapiga wafia chama hata sikijui.

Amandla...
 
Waandishi siku hizi wapoje? Mkoa haujatajwa, huyo waziri alikuwa wapi wakati wa huo mkutano, hizo taarifa kazitoa wapi? Huo uchunguzi mdogo kaufanya akiwa wapi? Halafu mambo ya chama yanaendaje kwenye serikali, je chadema wanaweza wakatoa malalamiko yao kama chama na serikali ya ccm ikasikiliza! Anyways kuongea maneno kama yale mbele ya kadamnasi sio sawa sana kwa kiongozi wa nchi ila waandishi wajifunze kuandika, wasiandike as if msomaji anajua kila kitu.
 
Ipo siku tu hivi vyeo vitayeyuka kama goliath alivyopingwa na kijana mdogo daudi na akaikomboa Israel, acha wakufute kazi ila mtetezi wetu yu hai
 
Silinde angeachia mamlaka husika zifanye uchunguzi wa kimya kimya (uncompromised investigation ) ndipo hatua stahiki zichukuliwe dhidi mwalimu. Mwalimu Mkuu yupo (msimamizi wa walimu), afisa elimu yupo (Mkuu wa idara), TSC wapo (mamlaka ya nidhamu), mkurugenzi yupo (mwajiri mwakilishi wa Rais), RAS yupo (Mkuu wa utumishi wa Umma ngazi ya mkoa).

Mawaziri kama George Boniphace Simbachawane (mambo ya ndani) ni mara chache kuwasikia wanabwabwaja maneno bila sababu za msingi ila wizara yake inaendelea kufanya vizuri katika utendaji. Rais wa Zanzibar (Haki) Dr. Hussein Mwinyi alihudumu katika wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa zaidi ya miaka 10 na ilikuwa ni nadra sana kumsikia akibwabwaja maneno bila sababu ya msingi.
 
Hivi siku hizi Sheria inasema ukitukana hadharani hukumu yake ni kufukuzwa kazi?
 
kwa hiyo waziri akaacha kazi zake na kuunda tume ya uchunguzi kwa mwalimu mmoja wa shule ya msingi, huku Tanzania nzima watu zaidi ya milioni 60 tukisubiri huduma ya kututatulia kero zetu?
 
Huyu Deputy Mini STAR aache kujikomba. Na ajifunze taratibu za kazi.

Miaka 60 baada ya uhuru halafu bado tuna viongozi ambao ni bootlickers kiasi hiki? Namwomba Rais amtumbue huyu waziri mdogo kwa kosa la kukiuka taratibu za kazi. Kama hatamtumbua basi na yeye atakuwa anakiuka taratibu za kazi.
 
Enzi za Mwendazake sasa hivi angekuwa anakoga lawama kama zote, raha ya Mama Samia ni kwamba hata litokee jambo gani yeye hapati lawama.
 
Utaratibu wa kumfukuza Mtumishi wa umma uko wazi je vikao vya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili vimefanywa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…