Mwalimu atekwa afanyiwa unyama Jijini Arusha

Mwalimu atekwa afanyiwa unyama Jijini Arusha

Screenshot_2016-10-12-16-10-47.png
Hamnaga wapuzi wanaonikeraga kama hao wanaochanganya mafuta na maji ...yan mnaleta siasa kila mahala.kama mwalimu anayo madai ya msingi yashughulikiwe tuachen figisu figisu tuijenge tz rais alisema mambo hayo yataendelea 2020 ...lema hapo anafata nini kwenye hii kesi.Lumumba inabidi mfungue kijidarasa kidogo cha jion cha kuwapiga msasa vijana wenu Wa mitandaoni hatuwez ifikia tz ya viwanda tukiwa na watokwa povu Wa aina hii.achen polisi wafanye kazi yao
 
ninavyo fahamu kama mtu kapata promosion ataangaliwa kama ana mudu kazi hiyo kwa miezi 6 ndo atenguliwe ama aidhinishwe sasa huyu wiki 3 tena bila sababu

hapa kuna shida mkurugenz aangaliwe
 
Sasa kwa taarifa yako humu kwenye mitandao kijamii panasaidia wahanga hao kwa haraka maana wanao chat ni wa2 wa aina tofauti na kwenye nafasi zao,mf:lile tukio la wale mwalimu walio muadhibu yule mwanafunzi kinyama lilianza humu,kuwa mjanja ucwe kama umetoka kjjn sigimbi
 
Sikilza kisa kinachofichua tuhuma za Mkurugenzi wa jiji la Arusha kahamia na mbunge wa viti maalum (CCM), Catherine Magige wakihusishwa na utekaji, kulisha sumu, kujeruhi na kisha kumvua vyeo, mratibu elimu Ngarenaro.

Anaaza kusimulia..

Kwa majina naitwa Batuli Hamad Isaya, ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Unga Ltd, Kata ya Unga Ltd Mkoani Arusha.

Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumatatu tarehe 3 jioni mida ya saa moja, nilikuwa naenda dukani kununua vocha simu yangu ilikata. Kwa hiyo nikachukua hela nikaenda dukani kununua vocha ambapo ni barabarani. Nimefika barabarani nikanunua vocha nikaikwangua nikawa narudi nyumbani.

Kutoka barabarani mpaka nyumbani kwangu kuna uchochoro ambao ni nimrefu kidogo, nikawa nikitembea kuelekea nyumbani huku naingiza vocha kwenye simu, namulika namba naingiza, namulika namba naingiza. Nilivyofika katikati ya uchochoro kuna mkaka alikuwa nyuma yangu, akanisalimia, anambia Batuli mambo? Nikamwambia poa. Sikuhangaika nae kwasababu niliona ni mtu anayenifahamu.

Lakini ghafla, kwa dakika moja akanambia simama hapo ulipo na ufuate maelekezo yangu, tofauti na hapo nitakupiga shaba. Nilipata hofu nikawa nimetetemeka ghafla simu yangu ikawa imedondoka lakini alinambia okota simu yako. Akawa ametoa bastola amenishikia kwa mgongoni.

Baada ya hapo nikawa nimesimama kwa hofu natetemeka, akanambia usiogope, Mimi nahitaji tu kuongea na wewe. Nitakachokuelekeza ukifuate tofauti na hapo nitakupiga shaba ya mgongo. Utarudi ulipotoka utaenda mpaka mwisho wa shule kuna Gari jekundu, utaingia kwenye hilo gari nataka tuzungumze.

Basi, kwa ile hofu niliyokuwa nayo na kutetemeka niligeuka na kuanza kufuata maelekezo aliyonielekeza lakini alikuwa yuko nyuma mimi mbele. Nikaanza kurudi, nikarudi mpaka barabarani nikateremka chini kidogo kwenye hilo gari nikafika, akafungua mlango, akanambia niingie, kulikuwa kuna mkaka alikuwa amekaa ndani ya gari akanipisha nikaingia nikakaa. Akafunga mlango yeye akazunguka upande wa dereva akapanda.

Ndani ya gari taa zilikuwa zimezimwa lakini kulikuwa kuna wakaka wawili, mmoja alikuwa alionipisha na mwingine alikuwa amekaa upande wa kushoto. Nikawa nimekaa katikati yao.

Baada ya muda, yule kaka akawasha gari, akageuza akawa anaelekea upande wa juu.

Nikawa na hofu sana, lakini aliyekuwa amekaa upande wa kulia kwangu akaanza kunisemesha. Akanambia, *we Batuli, ulipoenda kumshitaki Mkurugenzi wako uache mara moja. Na hapo ulipoenda kulalamika usirudi tena, kama unapenda kazi yako kama unapenda maisha yako.* Tulia ufundishe na unyamaze ufunge mdomo kimya.

Wakati huo tulikuwa tumefika eneo moja lina mataa panaitwa Kona ya Esso. Nikawa nimeshtuka sana nikaendelea kupata hofu. Sasa baada ya kuniambia yale maneno, nikawa nimepata wazo. Au kwasababu nilienda kulalamika kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu ishu ya Mkurugenzi? Kwa hiyo nikawa najiuliza maswali kichwani. Lakini baada ya hapo, nikaanza sasa kuhisi kwamba siko salama. Nikaanza kupiga kioo cha gari. Wakati huo tulikuwa tumefika eneo moja naiona sheli kwa mbele, nafikiri ni maeneo ya Kona Mbauda.

Nikawa napiga lile gari kwa nguvu upande wa kulia, kioo kikawa kimevunjika kwa malengo kwamba nipige kelele sasa niombe msaada. Lakini wakati nagonga lile gari, kioo kilivyovunjika, yule kaka aliyekaa kulia kwangu akawa ameniwekea kiwiko cha mkono shingoni. Alivyoniwekea kiwiko cha mkono shingoni akawa amenikandamiza, nikawa najitahidi kutoa ule mkono lakini akawa tayari amenibana eneo la shingo.

Kaka aliyekuwa amekaa upande wa kushoto kwangu, akawa kama vile ananisukuma kichwani, akachukua kitambaa akaniziba puani na mdomoni. Baada ya kuniziba pua na mdomo nikaanza kuhisi kizunguzungu. Lakini baada ya muda nikawa nimeishia kwenye usingizi. Kwa hiyo sikujua tena kilichoendelea.

Lakini baadae, nikawa nahisi tena niko kwenye gari, nasikia sauti za watu wanaongea, nikijarubu kufumbua macho nikawa nashindwa. Nikijaribu kufungua mdomo naona mdomo ni mzito. Baada tena ya muda nikaendelea kupata fahamu taratibu, baadae nikaweza kufungua macho. Ile kufungua nikakutana kuna mkaka alikuwa amekaa pembeni yangu ambaye ni askari lakini ninamfahamu anaitwa Yuda. Alikuwa amekaa pembeni ya kitanda ni mazingira ya hospitali. Wakati huo kulikuwa kuna dokta ananicheki.

Basi wakati nimefungua macho, Yuda alikuwa anaendelea kunihoji, ilikuwaje nikawa numuelezea kwamba kulikuwa kuna watu wamenichukua wamenieleza moja mbili tatu. Wakati Yuda ananihoji dokta akawa anaendelea kunichoma drip, akawa amenitundikia dripu na amenichoma na sindano ndio wakati huo Yuda akawa anamueleza daktari kwamba kuna mabomba haya ya sindano tumeyakuta hapo chini, wakawa wanayacheki baadae dokta akasema kwamba haya mabomba, hii kiboksi mlichokiokota ni kiboksi cha insulin, itakuwa wamemchoma dawa ya sukari ya kuteremsha sukari mpaka chini. Na hapo hapo wakachukua vipimo wakanicheki sukari wakakuta kweli sukari iko chini wakaendelea kunitundikia dripu.

Nikapelekwa WODINI, baadae dokta alinicheki akanambia sijaingiliwa kwenye maumbile yangu ya kike lakini nilikuwa nableed. Nikamuuliza hii bleed inasababishwa na nini akanambia ni hali ya hofu ndio maana bleed inatoka lakini hakuna jeraha lolote.

Ila kwa upande wa tumboni kulikuwa na maumivu makali, kulikuwa na kijereaha ambacho kinaonekana nimechomwa na kitu chenye ncha kali, lakini manesi walivyonicheki wakasema kwamba hata kama ni kisu au ni bisibisi, haijaingia sana ni kisehemu kidogo kama robo sentimeta. Nikaingizwa wodini nikaendelea kupata matibabu. Nikalala pale wodini mpaka asubuhi.

Asubuhi daktari akapita akanicheki nilikuwa na maumivu sehemu za tumbo, akaniandikia kwamba nitafanyiwa ultra sound lakini akanianzishia kwanza antibiotic, na baadae wakanichukua vipimo vya kunicheki maambukizi kwasababu nilichomwa na vitu vyenye ncha kali mkononi pamoja na maeneo ya tumbo. Wkanicheki HIV test baadae nikapelekwa kwenye chumba cha counselling nikafanyiwa counselling, wakanishauri nianze dawa za kuzuia maambukizi kwasababu damu yangu ilikuwa iko negative. Nikakubali nikaanza hizo dawa, wakashauri nilale tena kwa siku ya pili ili waangalie kama mwili wangu utakuwa na mabadiliko yeyote.

Kwahiyo nikabaki pale hospitali ya Mt Meru mpaka siku iliyofuatia asubuhi, nikawa niko vizuri lakini asubuhi daktari akanishauri niendelee kutumia hizi dawa nisifanyiwe tena ultrasound. Kama nitaonekana nina tatizo lolote basi nitarudi kwa ajili ya vipimo zaidi. Kwa hiyo akaniandikia dawa za kumeza antibiotic, wakanipa na hizo dawa ambazo nilikuwa nimeshazianza jana yake nikaruhusiwa kwenda nyumbani.

Sasa nikawa najaribu kuwaza kwamba hili tukio kwanini litokee na kwanini wale watu waniambie hivi. Nikajaribu kuwaza sasa kuna kipindi kama wiki nne zilizopita katika idara yangu ya kazi nilipata promotion. Nilipata barua ya kuniteua kuwa Mratibu wa Elimu katika Kata ya Ngarenaro, nikaipokea, hiyo barua ilikuwa inaonesha ni tarehe 17/9/2016 nikaenda kuripoti kwenye kituo nilichoelekezwa nikaanza kazi mara moja. Kata hiyo ina shule kama 9. Nikaanza majukumu ambayo barua ilikuwa imenielekeza. Lakini nikafanyakazi wiki la kwanza, wiki la pili, wiki la tatu.

Wiki la nne tukiwa ndani ya kikao ambacho kiliitishwa na Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo ukumbu wa AICC ambaye aliwaita walimu wa Sekondari nikapigiwa simu na mlinzi wangu wa Kata ambaye ni Afisa Taaluma, Sara, akanambia unaitwa, njoo huku mbele nifuate. Nikamfuata ndani ya ukumbi, kufika pale akanambia nenda kwa Mr Mallya kuna maagizo, nikamfuata akanambia unatakiwa urudi kwenye kituo chako. Nikamwambia sawa. Nikajua ni maelekezo ya kazi, nikarudi kwenye kituo changu pale nikatulia nikawa nasubiri labda kuna kitu chochote.

Mpaka saa tisa na nusu, sikuona chochote, baadae tena nikapigiwa simu, unaitwa Ofisi za Elimu. Nikarudi tena Ofisi za Jiji. Nilivyofika nikakutana na barua Afisa Elimu amenipa barua ya kutengua uteuzi wangu. Nikaipokea ile barua pale pale nikaifungua nikaisoma imeandikwa Kutengua Uteuzi wa Kuwa Mratibu wa Elimu Kata ya Ngarenaro. Nilipoisoma tena, kwanza nikashtuka, nikatetemeka, nikasema nimefanya nini? Ni nini nimeshindwa? Sikupata majibu sahihi, nikamuuliza Afisa Elimu hii barua ni vipi? Akasema mimi sijui kinachotakiwa fuata maelekezo ya barua iliyokuelekeza, aliyekuteua ndio aliyekutengua.

Basi nikaipokea barua mara moja nikarudi kituo cha kazi nikaripoti nikamuomba Mwalimu Mkuu wangu akanipangia vipindi nikaendelea na kazi. Lakini baada ya siku mbili, nilianza kujiuliza kichwani, hii nafasi ndogo nimepewa nimeshindwa kwasababu gani? Nikataka sababu zilizonisababisha kushindwa hii kazi.

Nilichokifanya nilienda kwa Mkuu wa Wilaya ambaye ni DC wangu, nikamuelezea kwamba, nikamshirikisha kulikoni kwamba nimepata promotion ndani ya wiki nne halafu wamenitengua lakini hawajanipa sababu za msingi na sielewi ni kitu gani ambacho nimekosea, napaswa kujua kwasababu Mimi nimejiendeleza, nina skills, nina uwezo wa kufanya kazi, sasa kama kazi kama hii ndogo nimeshindwa kufanya kazi kubwa nitawezaje na nimeshatuma application mbalimbali?

Kwakweli, Mkuu wa Wilaya akaniambia , akasoma zile barua, nikampa background kidogo ya kazi ambazo nimeshawahi kufanya, nimeshiriki kazi nyingi katika jamii, akanambia hii itakuwa ni sintofahamu, ananiambia hebu ziache hizo barua zako zote mbili nitafuatilia nijue kwa Mkurugenzi kuna sintofahamu gani. Baadae ikabidi nimuelezee Mimi naona kama vile *Mkurugenzi wa Jiji la Arusha*

Hajanitendea haki, kwasababu, kwanza alipaswa kuniambia ni kitu gani ambacho nimekosea, kitu gani ambacho nimeshindwa, yaani kipi ambacho sijakifanya mpaka aniandikie barua ya kunitengua? Lakini sikupata ushirikiano. Ushirikiano ni kwamba rudi kafanye kazi ukae kimya.

Sasa nikawa nahusianisha hii *kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ndio imepelekea mimi kuja kufanyiwa kitendo kama hiki nilichofanyiwa au ni kipi kilichosababisha?* Sikupata majibu sahihi.

Lakini baadae nikaendelea kuvuta kumbukumbu zangu ziku za nyuma, nilivyopata hii barua ya promotion, katika haya maGrupu ya WhatsApp, ambayo niliona Mheshimiwa *Mbunge Catherine Magige alishawahi kuandika kwamba watashughulika na vyeo vyangu, watanishughulikia na wakasema kwamba hawaongei na mbwa wataongea na mwenye mbwa* na hawakunisight kabisa jina langu. Lakini nikafuatilia nikaona ni meseji ambazo hazina mantiki nikawa nimetulia.

Sasa baada ya kupata hili tukio la kutekwa ndio nimeanza kuhusianisha, *je, ni Mkurugenzi ndio kwasababu nimelalamika kwa Mkuu wa Wilaya ndio amesababisha hili au ni Mbunge Catherine Magige kwasababu ya kumuadvise katika kazi zake ameona namkosoa sana katika kazi zake ndogondogo?* Nimeshindwa kupata majibu.

Na mpaka kufikia sasa hivi naendelea na dawa ambazo zinanisababishia kuharisha, kutapika na *Kesi hii iko Polisi kwasababu Polisi ndio walioniokota.*

Polisi wameahidi watalishughulikia lakini leo nina siku ya tisa sijaona reaction yeyote na wameniahidi kwamba wanaendelea kufuatilia. Sasa sijajua wanafuatilia nini au sijajua ninasaidikaje kwasababu mpaka dakika hii sielewi lakini iko mikononi mwa Polisi walishachukua maelezo, wamekuja kunitembelea, wanafuatilia. Na *hata RCO alikuja hospitali kunisalimia* kwa hiyo bado wanafuatilia.

Kwa hiyo nilikuwa naiomba Serikali kama itaweza kunisaidia afya yangu niendelee kuchunguzwa kwasababu mpaka dakika hii *sina uhakika kama sindano nilizochomwa ni kweli ni hizo za insulin kwamba sukari ishuke au ni virusi vya Ukimwi wameniingizia ili nife taratibu, au ni nini kimewekwa katika mwili wangu*, bado sijajiridhisha kwasababu sijachekiwa sumu kwenye mkojo, sijachekiwa...yaani sielewi kwakweli.

Kwa hiyo ni ninaomba kwa yule ambaye anaweza kunisaidia basi anisaidie.

Naomba pia swala hili hata Mh Rais aweze kulifahamu kama kuna mtendaji ambaye anaweza kuenguliwa nafasi yake pasipo kujua kosa lolote, ni vyema akalifahamu. Ikawa ni vizuri na Mimi nikaelewa kwamba nilichofanyiwa ni haki? Uko kwenye nafasi, hujawahi kufanya kosa lolote, hujakutwa na kashfa yeyote, hujahusika na watoto hewa au hujahusika na ubadhirifu wa fedha, umetenguliwa pasipo sababu ya msingi na kila ukihoji wanakwambia kwamba nyamaza kimya endelea kufanya kazi.

Nashindwa kuelewa kwakweli, bado naona Mkurugenzi wangu wa Jiji la Arusha hajanitendea haki, labda kuna sintofahamu lakini ni vyema akaiweka wazi kwasababu naona kwanza amenichafulia faili kutokana na nina uwezo wa kufanya kazi. Na kazi nafanya.

Kwahiyo, kama kuna chombo cha sheria kinafuatilia kitende haki"

Hizi ndo document za mwalimu huyo.

View attachment 416340 View attachment 416341 View attachment 416343 View attachment 416346
Bado siamini Maelezo yako hasa baada ya kutoa barua ya promotion maana haijakamilika.
 
Hii Habari inamchezo
Na kwa vile ni Arusha,sishangai kabisaaa
Haya ndio yale mambo ya yule Mwaandishi wa Habari wa DW wa Zanzibar aliesema katekwa,leo kimyaa baada ya kuumbuka.

Sasa ni ngum saana kwa mtekaji kujieleza namna ile,na ni ngum saana mtekaji kuwa mnajuana halafu yeye ndio afanye tukio.Na pia uwezo wa kupambana na watu mpaka ukavunja kioo cha gari,labda iwe ni ushahidi tu,lakini ngum saana mtekaji kukuachia wazi kirahisi namna hiyo.

Ukweli utajulikana,ila Pole saana,na hope utasaidiwa
Ila Mshahara wa dhambi siku zote ni mauti
 
UKATILI WA KUTISHA ARUSHA: MKURUGENZI WA JIJI NA MBUNGE VITI MAALUM WATAJWA KWENYE JARIBIO LA KUUA.

Mwalimu Batuli Hamad (pichani kushoto) ametekwa, kupigwa, kutobolewa tumboni kwa kitu chenye ncha kali, na kuchomwa sindano inayodhaniwa ni ya sumu kisha kutelekezwa porini bila fahamu huko mkoani Arusha usiku wa jumatatu tarehe 03/10/2016, katika tukio linalodhaniwa kuratibiwa na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Ndg.Athumani Kihamia na Mbunge wa viti maalumu mkoani humo (CCM) Catherine Magige.

Mwalimu huyo wa shule ya msingi Unga Ltd Arusha anahusisha tukio la kutekwa kwake na kufanyiwa vitendo vya kikatili na mgogoro uliopo baina yake na Mkurugenzi wa jiji hilo na mbunge huyo wa viti maalumu.

Tukio hilo limeripotiwa kituo cha polisi kati Arusha na kupewa RB namba AR/RB/12730/2016.

#Matukio_Kabla_ya_Kutekwa

Tarehe 17/08/2016 Mkurugenzi wa jiji hilo Ndg.Athumani Kihamia alimpandisha cheo Mwalimu Batuli kuwa Mratibu wa Elimu kata ya Ngarenaro. Uteuzi huu ulitokana na Mwalimu huyo kukidhi vigezo vyote muhimu vya kitaaluma na uzoefu kazini. Batuli ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika tasnia ya ualimu, na shahada ya elimu baada ya kujiendeleza kimasomo. Kwahiyo uteuzi wake kuwa mratibu elimu ni jambo ambalo alistahili.

Mwalimu huyu anadai kuwa alifanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika nafasi yake mpya. Lakini ghafla tar.19/09/2016 mwezi mmoja tu baada ya kuteuliwa, aliandikiwa barua na Mkurugenzi Kihamia ya kutengua uteuzi wake kama Mratibu wa Elimu na kumrudisha shule ya Msingi Unga Ltd akaendelee kufundisha.

Lakini barua ya Mkurugenzi Kihamia haikueleza kwanini amemshusha cheo Mwalimu Batuli. Barua hiyo ilisema tu kwamba Batuli ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya Mratibu elimu lakini haikusema ni majukumu gani ambayo Batuli alishindwa kutimiza.

Mwalimu Batuli hakuridhika na maamuzi hayo, kwa sababu hakuelezwa kosa lake, wala hakupewa nafasi ya kujitetea. Hata hivyo mwezi mmoja tu aliofanya kazi ni kipindi kifupi sana kuweza kupima utendaji wake. Kipindi hiki alitakiwa kufanyiwa "mentorship" na "orientation" ya nafasi yake mpya kabla ya kuanza kupima utendaji wake.

Vilevile Kanuni za utumishi wa umma na sheria ya ajira na mahusiano kazini no.6 ya mwaka 2004, kwa pamoja vinaeleza hatua za kuchukua kwa mtumishi aliyeshindwa kutimiza wajibu wake. Mojawapo ni barua mbili za onyo na nafasi ya kujitetea kabla hajavuliwa madaraka. Lakini haikua hivyo kwa Batuli. Yeye hakuandikiwa hata barua moja ya onyo wala hakupewa nafasi ya kujitetea. Ni dhahiri kuwa hakutendewa haki.

Kwahiyo akatafuta nafasi ya kukutana na Mkurugenzi Kihamia ili ajue sababu ya kushushwa cheo na ajue ni wapi alipokosea ili aweze kufanyia kazi mapungufu yake. Lakini Kihamia alimpuuza na hakumpa nafasi ya kumsikiliza.

Hivyo basi Mwalimu Batuli akaamua kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ili kueleza suala lake. Mkuu huyo wa wilaya Ndg.Gabriel Fabian Dagarro alimpokea Mwalimu Batuli na kumsikiliza, ambapo alionesha kushangazwa na uonevu aliofanyiwa. Mkuu huyo wa wilaya aliahidi kufanyia kazi suala hilo kwa kuwasiliana na Mkurugenzi Kihamia.

Mkurugenzi Kihamia hakufurahishwa na kitendo cha Mwalimu Batuli kufikisha suala lake kwa Mkuu wa wilaya kwani alitafsiri kuwa ameenda kushtakiwa. Baada ya hapo ndipo akatekwa na kufanyiwa ukatili wa kutisha. Mwalimu huyu kwa sasa anaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mt.Meru.

Akiongea na waandishi wa habari amehusisha tukio la kutekwa kwake na mgogoro baina yake na Mkurugenzi Kihamia kwa sababu watekaji wakati wanampiga walikua wakimwambia "Utajutia uamuzi wako wa kwenda kumshtaki Mkurugenzi huko ulikoenda"

Baada ya kuokotwa akiwa amepoteza fahamu Mwalimu Batuli alikimbizwa hospitali ya mkoa ya Mt.Meru ambapo alipewa matibabu na kutibiwa jeraha la tumboni alilotobolewa na kitu kinachodaiwa chenye ncha kali. Hata hivyo haijajulikana sindano aliyochomwa ilikua na kitu gani kingine japo uchunguzi wa awali umeonesha kuwa ilikua na "Insulin"

#Catherine_Magige_anahusikaje?

Kwa mujibu wa Mwalimu Batuli, anasema siku chache baada ya kuteuliwa kuwa Mratibu wa elimu kata ya Ngarenaro aliingia kwenye mgogoro na mbunge Magige kupitia group moja la whatsapp ambalo wote wawili wapo. Katika group hilo Batuli anadai alimkosoa Mbunge Magige ktk mambo mbalimbali yanayohusu ubunge wake. Ukosoaji wake ulikua wa nia njema ili Magige aweze kufanyia kazi mapungufu yake na kuboresha utumishi wake.

Lakini Magige alichukulia ukosoaji huo "in negative perception" na akadhamiria kumchukulia hatua Mwalimu Batuli. Kupitia group hilo la Whatsapp Magige anadaiwa kumwambia Batuli kuwa ATAMSHUGHULIKIA. Na baada ya muda mfupi Mwalimu Batuli akaandikiwa barua ya kutenguliwa katika nafasi yake ya Mratibu wa elimu kata ya Ngarenaro.

Kwahiyo Batuli anaamini alifukuzwa kazi kwa majungu na sio kweli kwamba alishindwa kutimiza wajibu wake wa kazi. Inaaminika kuwa Magige alipeleka majungu kwa Mkurugenzi Kihamia baada ya kukasirishwa na kukosolewa kwenye group la Whatsapp. Kihamia nae akafanyia kazi majungu ya Mbunge huyo na kuamua kutengua uteuzi wa Batuli.

Ndio maana kwenye barua ya kumvua madaraka alishindwa kueleza ni majukumu gani ambayo Batuli alishindwa kutimiza. Na hata Batuli alipoomba kukutana na Mkurugenzi huyo alikataa kwa sababu alijua kwamba amemvua madaraka kwa majungu tu na hakuwa na sababu yoyote ya msingi.

Hii ina maana kuwa mgogoro kati ya Batuli na Magige ulioanzia kwenye group la Whatsapp, ulitengeneza mgogoro mpya kati ya Mkurugenzi Kihamia na Batuli, ambao umepelekea yeye kutekwa na kufanyiwa vitendo vya kikatili.

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:

1. Rais Magufuli atengue uteuzi wa Kihamia mara moja. Katika kipindi cha miezi miwili tu tangu ateuliwe kuwa mkurugenzi Arusha amegubikwa na kashfa nyingi kuliko wakurugenzi wote nchini.

Wiki jana alipata kashfa ya ufisadi wa mafuta ya gari yake ambapo alitumia lita 1900 badala ya lita 300 alizopewa kwenye bajeti. Sasa ameingia katika kashfa nyingine ya kuhusika kutekwa kwa Mwalimu Batuli. Hivi mtu wa aina hii anaendelea kuachwa madarakani ili iweje? Mnataka afanye makubwa zaidi ya haya ndo mchukue hatua?

Kutekwa kwa Mwalimu Batuli, kupigwa, kuchomwa bisibisi tumboni, na kuchomwa sindano ya "sumu" ni ushahidi kwamba alikusudiwa kuuawa. Yani watekaji waliamini wamemuua Batuli lakini akapona kwa miujiza ya Mungu. Sasa jiulize mtumishi wa umma anayetajwa kwamba alihusika kwenye njama hizi je anastahili kuendelea kubaki kwenye nafasi yake?

2. Vyombo vya dola vifanyie uchunguzi suala hili na kama kweli itadhibitika kuwa Magige na Kihamia wanahusika, basi wachukuliwe hatua za kisheria. Pia chama cha mapinduzi kichukue hatua kali za kinidhamu kwa Mbunge wake Catherine Magige ikiwa Polisi watadhibitisha kuwa alihusuka.

3. Waalimu wamekuwa kama yatima nchi hii. Wananyanyaswa, wanaonewa, wanadhalilishwa lakini hawawezi kusema na hata wakisema wanapuuzwa. Sasa ni wakati wa kujitokeza na kupinga uonevu huu.

Kwahiyo nategemea kuona waalimu nchi nzima bila kujali itikadi zao, wakijitokeza na kulaani tukio hili. Nategemea pia wanaharakati wa haki za binadanu na wanaharakati wa masuala ya kijinsia wakijitokeza kwa wingi kulaani ukatili huu dhili ya Mwalimu Batuli. Kwa nguvu ileile mliyojitokeza kulalamikia tukio la Mbeya, mjitokeze kulalamikia tukio hili pia.

Kataa uonevu. Pinga ukatili wa kijinsia. Kataa unyanyasaji katika vituo vya kazi. Pinga viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya kunyanyasa wanyonge

14657376_1157122947712729_5121507863715443659_n.jpg

14657372_1157123131046044_2921391089228839025_n.jpg
 
Mods mmepost kabla sijamalizia kuandika heading....isomeke ...Malisa aanika ukatili wa Mkurugenzi Jiji la Arusha
 
Rais anavotafuta sifa huyu ataondoka naye tu we subiri muda si mrefu......
 
Bavicha mnahangaika sana na mambo ya kudhania,suala la ajira ya mtu mnashupalia na kuweka siasa.Huyu mwalimu inawezekana pia kala hela ya watu mnamsingizia mkurugenzi ili kuchafua tu kisa kashiriki kuzuia posho
 
JPM hata akijifungia magogoni mwaka mzima hawezi pata wasafi kutoka hicho chama.
 
Back
Top Bottom