Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Binti Msichana

Senior Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
109
Reaction score
249
Nimesikitishwa kupata habari kuhusu mwalimu anayefundisha shule ya sekondari Dunda iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani kukimbia kazi ya ualimu baada ya kulipwa 34000 kwa mwezi.

Hii inatokana na adhabu ya kushushwa cheo na kulipwa nusu mshahara na Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kosa la utoro kazini.

Mwalimu huyo wa kike aliishi maisha magumu sana hapo hapo shuleni ,alikosa mpaka hela ya kula ilimlazimu auze miwa na maembe aliyoyaokota hapo shuleni ili apate pesa ya kula.

Uzalendo ukamshinda baada ya mazingira magumu ya kazi aliamua kuondoka kazini bila ya taarifa kwa muajiri.

Habari nilizozipata mwalimu huyo yupo Mlandizi akifanya kazi ya kuhudumia wateja bar.

TSC mnapotoa adhabu ya kupunguza mishahara kwa walimu mzingatie iwapo kama mtuhumiwa ana mikopo benki, isitoshe adhabu ya kupunguza mshahara ni ya kikatili maana mshahara wenyewe hautoshi hapo hapo mnaupunguza.

Habari nilizozipata huyu mwalimu alikuwa na madeni benki na taasisi za fedha hapo Bagamoyo.

Kutokana na mazingira magumu ya kazi mwalimu huyo kaamua kutelekeza kazi yake.
 
34 elfu [emoji849]

Hawa kenge mbona wana masihara mnoo na maisha ya watu hawa, kuna mbuzi ziko juu huko zinafanya makosa yanayoigharimu tanzania yoote lakini hawaguswi.

Lakini kwa kuwa sisi wenyewe ni wazembe haya acha watufanye wanavyojisikia.
 
34 elfu [emoji849]

Hawa kenge mbona wana masihara mnoo na maisha ya watu hawa, kuna mbuzi ziko juu huko zinafanya makosa yanayoigharimu tanzania yoote lakini hawaguswi.

Lakini kwa kuwa sisi wenyewe ni wazembe haya acha watufanye wanavyojisikia.

Kweli mkuu, kuna kenge wanazingua sana katika nchi hii lakini hamna anayewagusa.

Nchi ni yao, serikali ni yao, ila kila jambo lina mwisho wake.
 
Ni elfu thelathini na nne(34000).Mr.Ban huyu mwalimu ni graduate, ana degree kutoka UDSM.
Hiyo mikopo aliipeleka wapi? Na bado akawa mtoro kazini, hadi kufikia kupewa adhabu hiyo. Hapo TSC kosa lao ni nini? Yaani ukope kope kwa interest zako na bado uwe mtoro kazini halafu uendelee kubembelezwa?
 
Back
Top Bottom