Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Nao wamezidi kujifanya vichwa ngumu huwezi kupewa hiyo adhabu kwa kuonewa na lazima alishapata kuonywa juu ya mwenendo wake na hakusikia barmaid huyu
Wanawake wanapitia mengi, huendi alimnyima mtu uchi, kwa hiyo kosa dogo anaadhibiwa pakubwa angalau alegeze sketi
 
Hiyo mikopo aliipeleka wapi? Na bado akawa mtoro kazini hadi kufikia kupewa adhabu hiyo. Hapo TSC kosa lao ni nini? Yaani ukope kope kwa interest zako na bado uwe mtoro kazini halafu uendelee kubembelezwa?
Relax kidogo
 
Mbona mwenda zake aliongeza makato ya loan board 2 times mlikaa kimya? Hii nayo itakuwa imechangia
 
Kuna mambo katika nchi hii yanatokea huyajui.

Nimepata kisa cha kusikitisha cha mwalimu wa shule ya sekondari Dunda iliyopo Bagamoyo, Pwani kulipwa mshahara wa elfu thelathini na nne (34,000) Tsh baada ya kupewa adhabu na Tume ya Utumishi wa Walimu TSC-Bagamoyo.

Mwalimu huyu amepewa adhabu ya kupunguziwa mshahara wake kutokana na kosa la utoro kazini.

Mwalimu huyu alijitolea sana kulitumikia Taifa hili zaidi ya miaka 20, akiwa kada wa CCM.

Mwalimu huyu aliishi maisha magumu sana kwa mshahara wa 34000 kwa mwezi hali iliyomlazimu atelekeze kazi yake bila kupenda kwani alikosa mpaka pesa ya kujikimu na maisha.

Alishinda na njaa kazini, alikosa mpaka nauli, ilimlazimu kutembea kwa miguu kutoka shule ya sekondari Dunda mpaka Kaole nyumbani kwake takribani ya km.10.

Mume wake kamtelekeza na watoto watatu, maisha ya mwalimu huyu ni magumu mno.

Mh.Rais, msaidie mwalimu huyu kwani ni kada mkubwa wa CCM wilaya ya Bagamoyo.
 
Mmmh!!!!
Huo ni ukatili ata kama mtu kakosa sio kumpa adhabu ya namna hiyo.

Kwanza sheria inasemaje juu ya adhabu kwa watumishi?
 
Tatatizo hizi taarifa huwa mnazileta za upande mmoja tu! Yawezekana huyo mwalimu ana matatizo makubwa ndo maana akapewa adhabu hiyo na isitoshe hiyo mishahara si inatoka hazina moja kwa moja.. na wao pia watakuwa wanalijua tatizo ndo maana wanamwingizia huo mshahara
 
Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Na laana hii ni kupiga piga watoto na kuwatukana matusi yenye kejeri.
 
Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Umetumia lugha ngumu kidogo kwa walimu. Kati ya walimu na mapolisi wapi wanafanya kazi ya laana?
 
Kuna mambo katika nchi hii yanatokea huyajui.

Nimepata kisa cha kusikitisha cha mwalimu wa shule ya sekondari Dunda iliyopo Bagamoyo, Pwani kulipwa mshahara wa elfu thelathini na nne (34,000) Tsh baada ya kupewa adhabu na Tume ya Utumishi wa Walimu TSC-Bagamoyo...
kwani ukisema vwewe ndo huyo mwalimu utauawa endelea kuwa kada
 
Nimesikitishwa kupata habari kuhusu mwalimu anayefundisha shule ya sekondari Dunda iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani kukimbia kazi ya ualimu baada ya kulipwa 34000 kwa mwezi...
Hiyo inaitwa mwana kulifaindi mwana kuligeti. Kwa nini aamue kujipa likizo?
 
Back
Top Bottom