Kuna mambo katika nchi hii yanatokea huyajui.
Nimepata kisa cha kusikitisha cha mwalimu wa shule ya sekondari Dunda iliyopo Bagamoyo, Pwani kulipwa mshahara wa elfu thelathini na nne (34,000) Tsh baada ya kupewa adhabu na Tume ya Utumishi wa Walimu TSC-Bagamoyo.
Mwalimu huyu amepewa adhabu ya kupunguziwa mshahara wake kutokana na kosa la utoro kazini.
Mwalimu huyu alijitolea sana kulitumikia Taifa hili zaidi ya miaka 20, akiwa kada wa CCM.
Mwalimu huyu aliishi maisha magumu sana kwa mshahara wa 34000 kwa mwezi hali iliyomlazimu atelekeze kazi yake bila kupenda kwani alikosa mpaka pesa ya kujikimu na maisha.
Alishinda na njaa kazini, alikosa mpaka nauli, ilimlazimu kutembea kwa miguu kutoka shule ya sekondari Dunda mpaka Kaole nyumbani kwake takribani ya km.10.
Mume wake kamtelekeza na watoto watatu, maisha ya mwalimu huyu ni magumu mno.
Mh.Rais, msaidie mwalimu huyu kwani ni kada mkubwa wa CCM wilaya ya Bagamoyo.