Mwalimu atupwa jela miaka 30 kwa kumshawishi mwanafunzi amlawiti

Mwalimu atupwa jela miaka 30 kwa kumshawishi mwanafunzi amlawiti

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa iliyopo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, aliyetambulika kwa jina moja, Said, amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na mwanafunzi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema siku za nyuma mwalimu huyo alijenga urafiki na mwanafunzi wa kidato cha nne (19) anayesoma shuleni hapo kwa kumnunulia vitafunwa shuleni hapo.

Amesema baada ya muda, mwalimu alimtaka mwanafunzi huyo akamtembelee nyumbani kwake na ndipo alipoanza kumuonyesha video chafu kupitia simu janja kisha kumsihi amwingilie kinyume na maumbile.

Ameeleza kuwa baada ya mwanafunzi huyo kuambiwa hivyo alikataa na kusema hawezi kufanya kitendo hicho, ndipo mwalimu alipoanza kumtisha kwa kumwambia asipofanya hivyo atapata adhabu kali mara kwa mara shuleni pamoja na kufukuzwa shule na hapo ndipo alipolazimika kufanya jambo hilo bila ridhaa yake
😳 Umesema alifanya?
 
Dah Dunia imegota mahala pake...Sema nini walimu kama hawa kitaa wana soko kwa masela
Eti alishindwa kutafuta jamaa wa mtaani, amfanye bwana ake, na vipesa anavyo mbona angetaka kubadilisha vijana ni yeye tyuuh.

Au alivutiwa na Dogo wa fomu foo! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom