Mwalimu gani mkali ushawahi kukutana nae katika maisha yako ya shule...!!!??

Mwalimu gani mkali ushawahi kukutana nae katika maisha yako ya shule...!!!??

Mwaka gani?
Me nlikuwa pale enzi ya Kigava.
1988 to 1991, form 1B, form 2 to form4 group 4 electrical.... Halafu kula na kocha, ticha wa bweni la chabu huyo, halafu kulikuwa na Lihuruku a.k.a Mbungi, si mchezo
 
Niliingia kipindi cha J. B. Vaginga, hao wengine tulikuwa nao.

Mhhh mmenikumbusha mbali hawa watu ni noma aisee.nakumbuka man to man alitukimbiza kutoka kibaoni hadi mnarani alivyotukamata tukaruka kichurachura hadi ofisini kwa kigava.tulipigwa siku hiyo sitasahau
 
Sie ni wa enzi za akina Kaguo, Mbungi (Kiswele), Kocha, Luhwago (Kaka)

Mkuu, ongezea na Olu wa kiingereza fomu one, kulikuwa Mchili bana akianza next next next mtakoma na hesabu zake.... Kitomali duh.

Ila mwalimu poa alikuwa Kinyakanyaka, akianza kukuchara fimbo, ukitoka nduki yameisha...
 
Mhhh mmenikumbusha mbali hawa watu ni noma aisee.nakumuka man to man alitukimbiza kutoka kibaoni hadi mnarani alivyotukamata tukaruka kichurachura hadi ofisini kwa kigava.tulipigwa siku hiyo sitasahau
we utakuwa ulikuwa unakaa Sinza.
 
Duh...
Mwl John Kivera :Manyara Ranch
Mwl Matunda :Meru Primary
Mwl Kaima :Ashira Girls
 
Pale S/M SAMORA MJIMWEMA alikuwa mwalimu JEMBE,huyu jamaa alikuwa anatufundisha hisabati darasa la 6-7,ilikuwa ukimzingua tu anagonga hadi vichwa.

O/level kulikuwa na MOHAMED UTALY,jamaa alikuwa anafundisha COMMERCE.anauliza swali na anakuchagua ujibu hata kama hukunyoosha kidole,ukipata unagongwa bakora kwamba ulikuwa unajua halafu hunyooshi kidole,

MAPUNDA D,(mbuni) huyu alikuwa mnoko balaa.

CHUO,kuna dingi mmoja alikuwa anaitwa MKUMBO alikuwa anafundisha FINANCIAL ACCOUNTING alikuwa anapenda kunyanyasa mabinti wakijichanganya tu amekula kichwa.

wapi MSAKY wa COMMUNICATION SKILLS?
shule ni noma arif.
 
Nyakabungo primary school pale Mwanza alikuwepo mwl Aron, pamoja na jirani yake mwl Banana.

Walikuwa wakisimama maeneo ya parade ground hata kama ni break time watoto wote wanaingia mitini na kurudi madarasani tena bila kusikia kengele ya pili.
 
NAKUMBUKA ENZI NIKIWA SHULE YA MSINGI NYANZA BANA! mkuu wangu wa shule alikuwa mwalimu LEMUNGE! mmh! huyu mama wa kichaga hakuwa na huruma kabisa katika masuala ya academics! hasa katika somo la hesabu! mwalimu alikuwa moto sana bana!

nakumbuka, yeye alikuwa na kawaida ya kuanza na chemsha bongo, ile asubuhi asubuhi tumetoka assemble, anaingia darasani na fimbo kama saba hivi kwa ajili ya kuadabisha wazembe! basi, alikuwa anatoa maswali kumi ya hesabu mchanganyiko, lakini yajibiwe ndani ya dakika moja!!

baada ya hapo mnabadilishana madaftari, mnasahihishiana huku akiwa anasimamia kwa umakini mkubwa! tatizo linakuja kwa wale wote waliopata below 5 bana!! mmh.. fimbo za hapo si mchezo! mwalimu alikuwa anachapa fimbo za mabega mpaka mtu unajuta kwanini umekuja shule, all in all, alitukuza ki-mathematics bana, si haba! tulifaulu wengi!
 
Nyakabungo primary school pale Mwanza alikuwepo mwl Aron, pamoja na jirani yake mwl Banana.

Walikuwa wakisimama maeneo ya parade ground hata kama ni break time watoto wote wanaingia mitini na kurudi madarasani tena bila kusikia kengele ya pili.

hahahahaaaa!!! hao si zaidi ya idd amin! duh!

naikumbuka sana nyakabungo.. iko karibu na nyanza
 
pale S/M KIBASILA kulikuwa na mwalimu anaitwa mwang'onda alikuwa mlemavu wa jicho moja. duuu huyo alikuwa noma angalau mimi sikusoma hapo......shule yetu pale CHANG'OMBE S/M kulikuwa na mwalimu anaitwa mussa huyo loo muda wote yeye anatembea na fimbo ya muuanzi,baaalaaa huyo......
sema sasa alipata ajari ya gari akakatwa mguu mmoja.....mungu amtie gumvu na matumaini ya maisha.
seco kulikuwa na ticha anaitwa NDOA noma.
 
Nilisikia amefariki but niliwahi kumiona,then nikasikia tena amefariki,ilikuaje jamani du rip,

hahahahaaaa!!! jamani imenibidi nicheke tu! sijaelewa kabisa ndio maana sijachukia!

hivi huyu mtu alifariki zaidi ya mara moja?
 
Mwene, wewe acha Mwl Mwang'onda alikuwa noma mm nilisoma kibasila jamaa alikuwa anatandika bakora si mchezo yule bwana, sekondari nilisoma Pugu wee kulikuwa na vichwa viwili hivyo mmoja alikuwa Wajimila aka Cobra na mwingine alikuwa anaitwa Mukulu usiombe uingie anga zao hao ni noma, hasa huyo Mukulu yeye anakwambia adhabu ni kazi isiyo na faida kwa hiyo ukiadhibiwa ukachimbe kisiki sio adhabu basi yeye anakwambia chimba shimo la futi kama nane na upana diameter kama 16 anakwambia ukimaliza ukamwambie, basi ukienda kumwambia anakuja kuangalia halafu anakwambia okota kikaratasi hata ice cream ile zamani anakwambia kitumbukize halafu hapo hapo anakwambia lifukie hilo shimo.
 
Dah! Mwalimu Kimasa wa Nganza sec alikuwa katili sana yule mwalimu! Sijui yuko wapi sikuhizi!
 
Mwalimu Njala Shule ya Turwa hukoo mbali miaka hiyo
 
Back
Top Bottom