NAKUMBUKA ENZI NIKIWA SHULE YA MSINGI NYANZA BANA! mkuu wangu wa shule alikuwa mwalimu LEMUNGE! mmh! huyu mama wa kichaga hakuwa na huruma kabisa katika masuala ya academics! hasa katika somo la hesabu! mwalimu alikuwa moto sana bana!
nakumbuka, yeye alikuwa na kawaida ya kuanza na chemsha bongo, ile asubuhi asubuhi tumetoka assemble, anaingia darasani na fimbo kama saba hivi kwa ajili ya kuadabisha wazembe! basi, alikuwa anatoa maswali kumi ya hesabu mchanganyiko, lakini yajibiwe ndani ya dakika moja!!
baada ya hapo mnabadilishana madaftari, mnasahihishiana huku akiwa anasimamia kwa umakini mkubwa! tatizo linakuja kwa wale wote waliopata below 5 bana!! mmh.. fimbo za hapo si mchezo! mwalimu alikuwa anachapa fimbo za mabega mpaka mtu unajuta kwanini umekuja shule, all in all, alitukuza ki-mathematics bana, si haba! tulifaulu wengi!