Mwalimu Japhet Maganga wa CWT hafukuziki? Jibu hili hapa

Mkuu kama wamemfanyia huo uhuni bila kufuata Sheria, ndio unategemea akienda mahakamani serekali watatii amri ya mahakama?
 
Hivi vitu mama vimekuzidi kimo, wewe unachoweza kujadili ni habari za Hamas na Israel tu japo ni kwa kiwango kidogo saaaaana.
 
Sheria inasema mtumishi asiporipoti kazi kwa siku 3 mfululizo bila sababu wala ruhusa kutoka kwa mwajiri anakuwa amejifuta kazi mwenyewe.
Sheria gani hiyo mkuu? Misingi ya haki asili ni kuwa lazima mtu asikilizwe kabla ya kufanya jambo dhidi yake. Usipoenda kazini kwa zaidi ya siku 5 basi hapo kunakua na msingi wa kufunguliwa mashtaka ya nidhamu ya utoro, ambapo utajitetea kwa nini hukufika kazini siku 5. Hakuna kujifukuza kazi automatic kwa sababu tu hujaenda kazini zaidi ya siku 5. Ni lazima upewe mashtaka na kusikilizwa.

Sasa Hao CWT si wanachama wake wanalalamika kila siku kuwa chama hakiwasaidii na kinawakata makato makubwa (2%) na wengi wanataka kujitoa ila CWT haitaki kuwaachia. Kwa hiyo kina Maganga walikataa kuondoka ili wazilinde fedha walizozipora kwa wanachama wao..yaani kuna wema wowote kwenye kulinda fedha iliyopatikana kwa uharamu?
 
Cwt kuna mchwa hata kama serikali imeshindwa kuchota simply eti akina Maganga wamezuia mbona bado hela za walimu zinaliwa ni kama hazina mwenyewe na ushahidi uliwahi tolewa wazi enzi za Magu kwa report ya ukaguzi iliyofanywa na CAG
 
Cwt kuna mchwa hata kama serikali imeshindwa kuchota simply eti akina Maganga wamezuia mbona bado hela za walimu zinaliwa ni kama hazina mwenyewe na ushahidi uliwahi tolewa wazi enzi za Magu kwa report ya ukaguzi iliyofanywa na CAG
Sasa kwanini hawachukuliwi hatua za kinidhamu?
 
Hiyo faragha iliyoingiliwa hapo ni ipi? Tangazo kuwekwa hadharani sio kosa. Maana Bado anaweza kuhadaa watu wasiojua kuwa Bado yuko CWT.
Hata mkataba wa ajira ya Mtu unapokoma say, kwenye Benki kwa mfano, inashauriwa kiifahamisha na kuutahadharisha umma kuhusu ukomo wa mkataba na Mtu husika. Sioni tatizo hapo.
 
Mimi nadhani serikali iko sahihi,hata sisi walimu huwa tunatumia mbinu hii,mwanafunzi anaweza kunigomea tukiwa wawili yakaisha kimya ila akinigomea darasani kukiwa na wanafunzi wanashuhudia au parade wanafunzi wote wanaona huyo lazima afukuzwe shule mbele ya parade huku wanafunzi wote wakiona ili iwe fundisho kwa wengine.

Huyo jamaa kagomea U-DC kwakuwa anapata hela nyingi za sisi walimu malofa ambazo twakatwa kila mwezi,hivyo naunga mkono huyo jamaa kushughulikiwa,ila nadhani sahihi kabisa ilikuwa ni kuishughulikia cwt ili ituachie huru walimu,can you imagine cwt wanachukua mfuko mmoja wa cement toka kwa salary yangu kila mwezi,cha kushangaza sina hata kiwanja,huku wao wakituna mashavu kama paka shume.


I hate #CWT
 
Sasa kwanini hawachukuliwi hatua za kinidhamu?
Serikali haifanyi mambo kwa pupa ila kwa strategies ndio maana iliamua kuchukua soft measures ili kutozua taharuki lakini haka kajamaa kakawa myopic kwa kukatalia mamlaka ya uteuzi.Huyu jamaa ameidhalilisha sana serikali kwa kujifanya nunda
 
Isitoshe hao Cwt wakishirikiana na maafisa utumishi wanawakata walimu mishahara yao pasipo ridhaa yao kinyume na sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 ambayo inataka mwalimu ajiunge na chama cha wafanyakazi kwa hiari yake kwa kujaza TUF 15 na kuomba kujiunga na chama husika .Kwanza hicho kiburi cha kumgomea Rais kimesukumwa na nini zaidi ya hela za Cwt ambazo hazina auditing na wanajichotea bure ni kama hazina mwenyewe.Wenye mamlaka huyo jamaa achunguzwe financial status yake in detail
 
Basi tujiulize kwanini hataki kurudi Temeke ambako ndio ajira yake iliko kwani CWT Kuna nini mpaka anang'ang'ania? Akaimbe cheichei na watoto ndio wito na ajira yake iliko
 
Aondolewe huyo mwana kulitafuta mwana kulipata, kwanini akatae kurudi Temeke sasa Kama kweli hakuhitaji uteuzi wa Raisi mbona anang'ang'ania CWT???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…