Mwalimu Maganga, Katibu Mkuu CWT aliyekataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya arudishwa kwenye Ualimu

Hizi ndizo akili za watanzania maana 99.9% ni machawa hawana msimamo na wala hawafuati wanachotaka.
Yeye hakutaka uteuzi akakataa, ila watu wanamnanga kama vile kuna kosa alilofanaya
Ni akili za kimasikini na kifukara sana.

Kuna watu hawataki kazi fulani tu, bila kujali zina heshima gani, zina fursa gani, hawazitaki tu.

Tuheshimu maamuzi yao.

Zaidi, serikali inapokuteua na kutangaza uteuzi bila hata kukuambia wewe kabla ya kutangaza uteuzi, ni kama imekudharau fulani hivi kwamba ni lazima ukubali uteuzi.

Kuna watu wana commitments za kifamilia, kijamii etc, hawawezi kuacha maisha yao sehemu fulani mara moja waende sehemu nyingine kisa uteuzi wa rais.

Mimi nilifurahi kusikia kuna watu wamekataa teuzi, serikali iwape hawa watu hata professional courtesy ya kuwaarifu kabla ya kutangaza, na kuwapa nafasi ya kukubali au kukataa uteuzi, rais asije kuaibika kukataliwa uteuzi na mteule wake.
 
Unahisi angeeenda afu akatenguliwa asingeweza kurudi kwenye kazi yake ya awali ya ualimu...?
Hapana angerudi tu na kuendelea kuwa mwalimu wa daraja A, Kwa ufupi alipisha na gari la mshahara....
 
Mnavyo toa maoni utadhani jamaa amefungwa jela maisha🤔🤔, amesha pata pesa ya kutosha kwenye ukatibu sasa anarudi kwenye kazi yake aliyo izoea huku akiendelea kula pesheni yake taratiiiibu,
 
Kwani lazima arudi huko?? Akiamua kujiajiri inakuwaje?? Hizi tabia za kibongo za kuviziana na kukomoana ndizo zinatuharibia maendeleo kama nchi! Hovyo kabisa!!
 
Mantiki ya taarifa za mwajiriwa kuwekwa hadharani ni zipi?

Alipaswa apewe barua yake kisha aripoti kazini. Kubandikwa kwenye mbao za matangazo ni upuuzi usio na maana.

Mbona kabla ya hapo, vibali vyake havikuwa wazi?

Pathetic!.
Kwenye hii dunia ukijifanya mjinga basi watu wanakujibu kulingana na ujinga wako ili uelewe kirahisi. Hiyo ndo lugha anayoweza kuelewa kirahisi huyo Mwalimu
 
Kwa taarifa yako hata angekubali uteuzi ule hadi sasa asingelikuwa mkuu wa wilaya…lengo lilikuwa ni kuwakomesha ukuu wa wilaya ilikuwa njia ya kuwachomoa na kuwahadhiri walijua fika
 
Mantiki ya taarifa za mwajiriwa kuwekwa hadharani ni zipi?

Alipaswa apewe barua yake kisha aripoti kazini. Kubandikwa kwenye mbao za matangazo ni upuuzi usio na maana.

Mbona kabla ya hapo, vibali vyake havikuwa wazi?

Pathetic!.
Hata mimi nashangaa sana.

Lakini ndo hivyo tena imeshafanyika. Na bila shaka haya ndiyo "maagizo toka juu" maana nakumbuka boss wao mkuu Rais Samia just recently alipokuwa anafungua kile kikao cha TCD alisema hili kuwa na watu wanaopewa kazi na serikali halafu wanakataa, hao hawastahili

Kwa hiyo obviously, hilo ni agizo la kumdhalilisha mwalimu huyu.

Hivi ndivyo serikali ya CCM inavyoji behave, kishetani shetani tu.
 
Cha ajabu mkurugenzi sio aliyepost ila afisa habari wa Tamisemi ndo kapost najiuliza imekuwaje wizara itume report ya Mamlaka ya manispaa
Ili kumdhalilisha tuu…najiuliza utaratibu huu umeanza lini?
 
USAHIHI ni kuwa "AMEKATALIWA KUPEWA KIBALI NA KURUDISHWA KUFUNDISHA DARASANI" na sio "KURUDISHWA KWENYE UALIMU" kwa sababu siku zote yeye amekuwa ni mwalimu na hata kama akistaafu au akifa bado atakufa au kustaafu na UALIMU wake
 
Mantiki ya taarifa za mwajiriwa kuwekwa hadharani ni zipi?

Alipaswa apewe barua yake kisha aripoti kazini. Kubandikwa kwenye mbao za matangazo ni upuuzi usio na maana.

Mbona kabla ya hapo, vibali vyake havikuwa wazi?

Pathetic!.
Kiukweli nimeshangaaa sana Kumbe ni Mwalimu. Maana ya Ualimu naona haijui. Ni muhimu apangiwe majukumu Mengine kwenye ualimu hatoshi
 
Kulazimisha uchawa au ukada kwenye vyama vya wafanyakazi si sawa kabisa. Teuzi hizo hazikuwa za nia njema, waliozikataa wanastahili hongera na naamini watanzania watawapa nafasi kwa mlango mwingine Kiongozi.
 
Umenena vyema ndugu yangu, huyu mwalimu alikua mbele ya muda kifikra kuliko wengi wetu na Phd zao.
 
Daaah pole yake sana... tusifurahie anguko la wenzetu... hii tabia ya kukomeshana imejaa sana zerikalini.

Wangempa tu hitaji la moyo wake
 
Waalimu wanachama wa CWT - Chama cha Waalimu Tanzania waonyeshe solidarity na waandamane kupinga viongozi wao kuburuzwa na watawala.
Kuburuzwa vipi wakati ajira yake rasmi ni tamisemi.. huko kwengine alikuwa anafanya kwa ruhusa ya mwajiri wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…