Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ni akili za kimasikini na kifukara sana.Hizi ndizo akili za watanzania maana 99.9% ni machawa hawana msimamo na wala hawafuati wanachotaka.
Yeye hakutaka uteuzi akakataa, ila watu wanamnanga kama vile kuna kosa alilofanaya
Kuna watu hawataki kazi fulani tu, bila kujali zina heshima gani, zina fursa gani, hawazitaki tu.
Tuheshimu maamuzi yao.
Zaidi, serikali inapokuteua na kutangaza uteuzi bila hata kukuambia wewe kabla ya kutangaza uteuzi, ni kama imekudharau fulani hivi kwamba ni lazima ukubali uteuzi.
Kuna watu wana commitments za kifamilia, kijamii etc, hawawezi kuacha maisha yao sehemu fulani mara moja waende sehemu nyingine kisa uteuzi wa rais.
Mimi nilifurahi kusikia kuna watu wamekataa teuzi, serikali iwape hawa watu hata professional courtesy ya kuwaarifu kabla ya kutangaza, na kuwapa nafasi ya kukubali au kukataa uteuzi, rais asije kuaibika kukataliwa uteuzi na mteule wake.