Mwalimu Maganga, Katibu Mkuu CWT aliyekataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya arudishwa kwenye Ualimu

Mwalimu Maganga, Katibu Mkuu CWT aliyekataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya arudishwa kwenye Ualimu

Binafsi sidhani kama rais alihusika na uteuzi wa Maganga moja kwa moja na hata hizi figisu figisu rais hahusiki nazo kabisa. Inawezekana upande mwingine unaopigania kuweka vibaraka wao hapo CWT ndio ulichomeka jina la Maganga kwenye ukuu wa wilaya ili apishe watu wapige hela.

Ieleweke, pale CWT kuna mvurugano wa madaraka mpaka sasa ambapo kila upande una back up ya viongozi wanaonufaika na pesa za walimu.
Tukumbuke, Maganga alichukua nafasi ya katibu Seif ambaye alihukumiwa kifungo cha miezi sita. Fuatilia Seif ni rafiki yake nani?

Inaonekana back up ya Maganga haina nguvu. Kama kugomea ishu ya uteuzi, mbona hata rais wa CWT naye aligomea uteuzi!

Kama Maganga akitumia ujasusi wa kiuchumi vizuri anaweza kupata barua ya kuendelea ila inaonekana ni boya tu mana tangu agomee uteuzi angekuwa ameishaseti mipango kwa bi mkubwa, mbona wenzake wanakula kwa urefu wa kama zao, bi mkubwa lazima angemuelewa tu kama angeenda kujieleza kitekniki. Hii ndio Tanzania!
Jamaa hakuwa na back up plan wala support aisee...!
 
Acha kupotosha mdau


Ticha ameomba kibal na muombwaj kakataa kutoa kibal husika unasemaje kuwa anakomolewa???


Arud kwenye ajira yake ili wenzake nao wale
Ndio tatizo la kudandia treni kwa mbele!! Mbona wafrika ndio mabingwa wa fitina, ungekuwa mfuatiliaji wa mambo ungejua nini kimekuwa kina mkuta jamaa toka alipokataa uteuzi, lilikuwa ni suala la muda tu.
 
Hii inanikumbusha kauli moja iliwahi kusemwa na wahenga kuwa ukibebwa bebeka na ukilishwa kamwe using'ate kidole kikulishacho!

Hatimaye rasmi sasa bwana huyo kukiona cha moto kwa kurudishwa kituo chake cha kazi kama Mwalimu Mwandamizi Daraja A katika Manispaa ya Temeke.

Ikumbukwe kwamba Ndg. Japhet Maganga na Viongozi wenzake wa CWT walikataa uteuzi huo January mwaka huu na wakasahau kwamba wanafanya kazi katika serikali hiyo hiyo yenye mamlaka ya kuwasubiri (hii imedhihirisha usemi wa aliye juu mgonje chini)

Leo nilishtuka baada ya kuona barua hii Kutoka Tamisemi ikiwa imeandikwa na manispaa ya Temeke. Maelezo yote yapo kwenye barua hii;

Hivi ni sawa mkurugenzi kusaini tangazo/taarifa hii pasipo hata kuweka jina lake? Au hiyo kuandika cheo chake tu ilitosha?
 
Mantiki ya taarifa za mwajiriwa kuwekwa hadharani ni zipi?

Alipaswa apewe barua yake kisha aripoti kazini. Kubandikwa kwenye mbao za matangazo ni upuuzi usio na maana.

Mbona kabla ya hapo, vibali vyake havikuwa wazi?

Pathetic!.
Kweli ndugu taratibu za kazi ni kati ya mwajiri na mwajiriwa. Ni ujinga wa hali ya juu.
 
Bwana Maganga ana akili sana tena kuzidi wewe mtoa mada alijua fika kuwa cheo cha ukuu wa wilaya ni cheo cha kwenda kudhalilishwa na alikuwa ametegwa ali atenguliwe na kupigwa bench kwa mgongo wa kupangiwa kazi nyingine …kwa hiyo alikuwa mbele ya muda na alifikiri zaidi yako….

Hivi kwa akili yako kabisa alikataa tuu bila kujua kitakachotokea? Alijua fika…
Bora afundishe kwa uhuru kabisa kuliko kwenda kudhalilishwa kwenye ukuu wa wilaya…
Yuko wapi jerry muro? Leo tuu mkuu wa wilaya ya Mtwara katenguliwa…

Alifanya jambo sahihi kabisa
Hakuna kitu angepoteza.. angeenda tu.. angepigwa chini angerudi kufundisha
 
Sasa si unaona Sasa kilichomkuta amepangiwa darasa la tatu c tarehe Moja asubuhi na mapema saa Moja kamili awe darasani kupiga pindi la stadi za kazi. Ningekua Mimi siwezi kupinga teuzi ya mh rais ata kama ingekua mtego Ili niende kuonekana siwezi kazi nitumbuliwe bado nitarudushwa tu kwenye ajira yangu ya awali au nitapangiw nyingine na mamlaka uwenda asingezalilika hivi asaivi angepangiwa sehemu nyingine tofauti na uko msingi mamlaka zingemuonea huruma
Uko sahihi kabisa
 
Hii ingekuwa awamu iliyopita tungeambiwa huyo Mzee ana visasi mara ni sadist etc.

Kwa hali ilivyo,hata huko kwenye ualimu awe macho lazima atakuwa anafuatiliwa kwa karibu!
 
angedhalilishwa kivipi kama performance yake ingekuwa ya kuridhisha?
Sio kila mtu anapenda kua mkuu wa wilaya Kuna wengine wapo tayari hata kuacha kazi kuliko kuteuliwa nafasi za kisiasa na wengine wapo tayari hata kuua au kujidhalilisha Ili wazipate hizo nafasi muhimu ni kuheshimu maamuzi ya watu
 
Bwana Maganga ana akili sana tena kuzidi wewe mtoa mada alijua fika kuwa cheo cha ukuu wa wilaya ni cheo cha kwenda kudhalilishwa na alikuwa ametegwa ali atenguliwe na kupigwa bench kwa mgongo wa kupangiwa kazi nyingine …kwa hiyo alikuwa mbele ya muda na alifikiri zaidi yako….

Hivi kwa akili yako kabisa alikataa tuu bila kujua kitakachotokea? Alijua fika…
Bora afundishe kwa uhuru kabisa kuliko kwenda kudhalilishwa kwenye ukuu wa wilaya…
Yuko wapi jerry muro? Leo tuu mkuu wa wilaya ya Mtwara katenguliwa…

Alifanya jambo sahihi kabisa
Sasa kapata nini kwa kukataa ukuu wa wilaya? Hata kama angeenda kutenguliwa, angerudi kwenye ualimu wake ambao ndio karudi sasa hivi.

Yeye alikataa sio kwa kutaka kurudi darasani, alikataa ili aendelee kuwa katibu wa CWT.

Mtumishi wa umma unabishana na Rais; hii akili sijui ni ya wapi!
 
Kwa mshahara wake ule kama alizichanga vizuri hafi masikini.
 
Back
Top Bottom