Mzee Mwakasege husisitiza sana Kuokoka ktk mafundisho yake.Wakati anafunga semina ya Neno la Mungu wilayani Kahama Mwalimu Mwakasege amesema amealikwa na.Kanisa Katoliki jijini Dodoma kuwa mnenaji Katika semina ya Karismatiki
Mwalimu Mwakasege atahudumu kwa siku.mbili 31/05/2022 na 01/06/2022
Chanzo: Upendo tv
Sina shaka ktk semina hii atawahubiria na kuwafundisha wakarismatiki juu ya Wokovu wa kweli na Kuokoka. Wakarismatiki wanadai na wanaamini wameokoka, jambo la kusiktisha bado wanamwomba Maria (aliyekuwa mama wa kimwili wa Bwana Yesu Kristo), wanaomba dua na sala zao kwa the so called watakatifu akina Petro, Yakobo, Yohana, na wengine, wanawaomba malaika, wanafanya ibada za wafu, wanaabudu kwa kutumia sanamu, na kadhalika.
Ngoja tusubiri maana ngoma nayo ikilia sana, hupasuka ati!