Mwalimu Mwakasege kufundisha katika semina ya Karismatiki ya Kanisa Katoliki jijini Dodoma 31/05/2022

Mwalimu Mwakasege kufundisha katika semina ya Karismatiki ya Kanisa Katoliki jijini Dodoma 31/05/2022

So
Usijifunge kusikiliza mahubiri lakini lazima uwe unajua imani yako vizuri kinyume chake utapepea na kila upepo wa mafundisho.

Ni kosa kusema hadi Mapadre wamejitafakari, hakika itakuwa ndani yao wanapata shida kuvumilia baadhi ya upotofu lakini kuhubiri habari za wokovu ni jukumu lao la msingi na hawawezi kupata shida na mtu anayehubiri hiyo kweli. Habari njema au injili ndio wokovu wenyewe sio ile sala ya dakika 2 kwamba sasa ndio umeokoka!

Wokovu sio tukio la mara moja ...ni safari ndio maana maandiko yanasema atakayevumilia hata mwisho ataokoka! Tatizo ni mapungufu yetu kwenye mafundisho lakini ni hatari madhaifu hayo yakitumika kutafuta ovyo kushiba nje ya utaratibu! Njaa haipaswi kukufanya ule chochote bali utatafuta kinachofaa!
Kwahiyo mkuu unataka kusema lilikua ni kosa kwa wanakarismatiki Jimbo la Dodoma kumpa mualiko Mwl. Mwakasege kufundisha hiyo juzi?

Nikukumbushe tu kua Yesu alivyokuja duniani hakuja kwa ajili ya watu fulani tu bali alikuja kwa ulimwengu mzima bila kujali dini sijui dhehebu...
Yohane 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Mkuu unaweza kusema sala ya dakika mbili tu ila nina uhakika itafanya mabadiliko makubwa sana kwenye maisha ya watu waliotoka kuokoka, na Mungu haesabu sijui huyu ameokokea kwa nani ila cha muhimu ni kuokoka!!
 
You see, hata wewe tayari kuna mafundisho yanaelekea kukutoa kwenye kweli. Mfano Mwakasege amesema pale ukiokoka unapigwa chapa right? Kwa andiko gani? Ubatizo ndio chapa na mlango wa Ukristo. Kumjua zaidi Mungu na njia zake ni swala la mafundisho sio kuokoka.

Vipi huoni Waislamu wanaoamua kuacha ya dunia ikiwemo ulevi na kuifuata kikamilifu dini yao waliitwa mbele kuokoka?

Kidogo kidogo utaanza kuacha kitubio, Ekaristi itakuwa ktk picha ya kilokole! Rozali utaiona ni ritual tu! Hii itakuingia kidogo kidogo

Sijasema asialikwe bali tuwe na muongozo ili kulinda tunachoamini. Mwakasege alipania ku promote ulokole! Angalia hekima ya mchungaji Kimaro jana! Hakuingilia msingi unaotutofautisha and he preached very well.
 
Kwahiyo wewe shida ni kuokoka tu?
 
Suala la MUNGU halihitaji elimu mnayoijua nyie makanjanja...elimu ya MUNGU anakupa yeye mwenyewe kwa kazi maalumu kupitia ROHO MTAKATIFU.
Yaani ukae tu ndani bila kusoma eti unasubiri Roho Mtakatifu akupe elimu! Ndio mnadanganywa hivyo hivyo kwamba kuna hela za miujiza
 
You see, hata wewe tayari kuna mafundisho yanaelekea kukutoa kwenye kweli. Mfano Mwakasege amesema pale ukiokoka unapigwa chapa right? Kwa andiko gani? Ubatizo ndio chapa na mlango wa Ukristo. Kumjua zaidi Mungu na njia zake ni swala la mafundisho sio kuokoka.

Vipi huoni Waislamu wanaoamua kuacha ya dunia ikiwemo ulevi na kuifuata kikamilifu dini yao waliitwa mbele kuokoka?

Kidogo kidogo utaanza kuacha kitubio, Ekaristi itakuwa ktk picha ya kilokole! Rozali utaiona ni ritual tu! Hii itakuingia kidogo kidogo

Sijasema asialikwe bali tuwe na muongozo ili kulinda tunachoamini. Mwakasege alipania ku promote ulokole! Angalia hekima ya mchungaji Kimaro jana! Hakuingilia msingi unaotutofautisha and he preached very well.
Mkuu kwani kuokoka ni nini? (Nini maana ya kuokoka?)
 
Hili kanisa katoliki inabidi libadilike bila hivyo litakuja kukosa waumini kabisa maana ndo kanisa ambalo waumini wake wengi wanakimbia baada ya kuisoma biblia vizuri.
Yaani wafuate biblia kama ilivyoandikwa na sio kama wanavoijua wao.
Nashauri mambo haya yafuatayo.
1. Waondoe masanamu na mapicha yote kanisani.
2. Mapadri na maaskofu waruhusiwe kuoa.
3. Watu waache kuungama kwa padri
4. Kuwe na huduma ya kichungaji na maombezi.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka
Asante. Lile andiko la atayeamini na kubatizwa ataokoka wanafikiri tunalipinga! Kila mbatizwa ameokoka maana tayari anachapa ya wokovu ambao anapaswa kuulinda hata mwisho kama ulivyonukuu. Tatizo tunataka kusimika namna mpya ya mtu kuwa Mkristo nje ya kuamini na kubatizwa!

Waulize waliookoka siku ile watabatizwa tena? Sasa kama hapana ni wokovu upi? Kuzaliwa mara ya pili ni kupitia ubatizo tu sio ile sala fupi na kuaminisha watu kuwa wameshaokoka! Baada ya pale akitenda dhambi lazima akafanye kitubio kama Mkristo mwingine yeyote! No exception!

Nimesema huko juu, hata nyakati za mitume wabatizwa wengine waliishi kinyume na wokovu waliopokea, wale hawakuambiwa waokoke kwa sala fupi bali waliungama dhambi zao na kufanya malipizi! Mkristo mbatizwa anapaswa kuhubiriwa jinsi ya kutunza wokovu wake na kama amekengeuka anarudia ahadi zake za ubatizo! Sio kuokoka! Hii ni myth iliyoibuka majuzi tu hata waanzilishi wa uprotestant kama Lutheran wanaushangaa!
 
Hili kanisa katoliki inabidi libadilike bila hivyo litakuja kukosa waumini kabisa maana ndo kanisa ambalo waumini wake wengi wanakimbia baada ya kuisoma biblia vizuri.
Yaani wafuate biblia kama ilivyoandikwa na sio kama wanavoijua wao.
Nashauri mambo haya yafuatayo.
1. Waondoe masanamu na mapicha yote kanisani.
2. Mapadri na maaskofu waruhusiwe kuoa.
3. Watu waache kuungama kwa padri
4. Kuwe na huduma ya kichungaji na maombezi.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Biblia ni sehemu ya mafundisho ya Kanisa! Biblia imekuja karne ya 4 tu na ni zao la Kanisa! Yesu alituachia Mitume ( Kanisa) na Roho Mtakatifu tu! Hakutupa kitabu kinachoitwa Biblia. BTW Biblia ni Catholic book inspired by holy spirit.

Biblia yenyewe hasemi popote kuwa Wakristo waamini yaliyoandikwa humu tu kama Quran! Biblia inakiri kupitia kitabu cha Timothy kuwa The church is the pillar and foundation of truth!

Mwenye authority of scriptures interpretation ni Kanisa na si mtu fulani!
 
Ni mali yetu. Kama hujui habari ndio hiyo. Wakatoliki ndio wakristo. Nyie wengine ni waasi tu. Ukidhani bibilia imekusanywa na nani Yani labda? Adui yeyote wa ukristo anadeal na kanisa la ulimwengu sio vijikanisa. Vimadhehebu.
Kwa hiyo Mbingu ni maalum kwa wakatoliki pekee?
 
MAPATO YA MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE

Je, mmeona kilichotokea Dodoma? Mmeona? Binafsi yangu nimeona aibu, aibu kubwa. Nimeona haya ya uso, haya tele. Nimeona haya kwa niaba ya Wakatoliki, kwenye kongomano la Dodoma. Nimesikiliza mahubiri ya Mwakesege nikapata ushahidi mkamilifu wa mwendelezo ule ule wa ujinga wetu. Nimesikitika sana. Hata nyie sikilizeni mada hiyo hasa dakika thelathini za mwisho. Ameshinda! Amewateka Wakatoliki kuokoka, sijui wale mapadre wawili waliokuwa wawezeshaji wenza wameokoka nao! Wakatoliki wameokoka baada ya mada! Lakini twendeni pole pole katika mambo mawili leo: ujinga wa lugha za kale za Biblia na uovu wa kiroho.

Ujinga wa Lugha za Kale
Mada ilihusu Sauli kuwa Paulo. Kwa wanaojua lugha za kale zaa Biblia, huu ni ujinga wa wazi kwamba mtu hajui Kiebrania wala Kiyunani (Kigiriki). Niwahabarisheni. “Sauli” na “Paulo” ni matamshi ya jina moja lile lile lakini kadiri ya makabila tofauti tu, wala hakuna maana yoyote ya mabadiliko ya kitu ama mtu. Mapadre waliokuwapo pale walipaswa walau kukanusha mada hii, maana bila shaka walihudhuria vipindi vya lugha za Kiebrania na Kiyunani (Kigiriki) Seminarini. Lakini huenda walikuwa wanapenda sana kipindi cha mapumziko!
Nisikilizeni vyema. Jina “Sauli” ndiyo matamshi ya Kiebrania, yaani kwa lugha ya Wayahudi, wakati “Paulo” ni matamshi ya Kiyunani au Kigiriki kwa watu wa mataifa. Yaani kwa “SAULI” ndivyo alivyokuwa anaitwa alipokuwa anafanya uinjilishaji kati ya Wayahudi wenzake, lakini baadaye alipohamia kwa watu wa mataifa katika Asia Ndogo, Ugiriki na Roma, watu wa huko ndiyo wakawa wanamwita “PAULO.” Aidha, matamshi ya “PAULO” ni ya Kilatini vile vile. Ndiyo maana yanatumika matamshi ya “PAULO” katika nusu ya Kitabu cha Matendo ya Mitume, si vinginevyo. Hakuna suala la kiteolojia hapo.
Kwa hili, hebu niwadarasisheni kwa mifano midogo miwili. Mtu anayeitwa “CLARE” nchini Uingereza na Marekani, wanakozungumza Kiingereza, ataitwa “CIARA” nchini Italia wanakozungumza Kiitaliano, ataitwa “KLARA” hapa Tanzania maana tunatamka kwa Kiswahili, lakini huyo huyo ataitwa “KALALA” huko Songea kwani wanatamka Kingoni.
Mfano mwingine. Mtu anayeitwa “YAKOBO” huku kwetu Tanzania, ataitwa “JAMES” huko Uingereza, ataitwa “JIMMY” huko Marekani, ataitwa “DIEGO” huko Argentina wanakozungumza Kihispania na ataitwa “TIAGO” huko Ureno, Brazili, Angola na Msumbiji wanakozungumza Kireno. Hivi ni ujinga wa lugha tu kuhubiri kwamba kulikuwa na kitu katika kutoka matamshi “SAULI” kwenda “PAULO.” Kwa vyovyote hili ni jambo dogo na lenye kutibika.

Uovu wa Kiroho – “Wakatoliki Kuokoka”
Uovu wa kusikitikiwa zaidi ni uharibifu uliofanywa na mkutano huo. Hakika haya ni madhara yatakayohitaji JIK kuoshwa. Wakatoliki wamehubiriwa waokoke licha ya kwamba kwa sakramenti ya Ubatizo walishafanyika Wakristo Wakatoliki. Wamekubalishwa kwamba walikuwa na upungufu kiroho. Wamekubali kuokoka, jambo ambalo maana yake ni kupingana na Yesu pamwe na Maandiko Matakatifu. Haya ni mapato ya ujinga ule ule niliokuwa nimeudokeza hapo mwanzo. Watu wetu hawajui “lipi ni la Kikatoliki” na “lipi si la Kikatoliki.” Wanapokea na kula vyote. Asalale! Hawana uwezo wa kupambanua “SUPU” na “SUMU.” Hawana uwezo wa kupambanua “KARIBU” na “KALIBU.” Alahaula!
Kwa hili, msishawishike kuniita nabii maana ilikuwa hatari ya wazi. Hata mlemavu wa macho aliweza kuiona. Hata mlemavu wa masikio aliweza kuisikia. Hata mlemavu wa miguu angeliweza kuikimbia.
Sikilizeni. Sisi Wakatoliki hatuthubutu kupingana na Yesu kwa kujinasibu TUMEOKOKA kwa sababu Yesu mwenyewe aliliweka jambo hilo katika wakati ujao (future tense) – ATA… na siyo wakati uliotimilika (perfect tense) – AME…. Soma alivyosema Yesu mwenyewe, “Mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye ATAKAYEOKOKA” (Mk 13:13). Hata Mtume Paulo tumsome vizuri. Mtume Paulo ameandika, “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa kukiri hata kupata wokovu – yaani mwishoni mwa maisha haya siyo sasa” (Rum 10:9-10). Hivi ndivyo tunavyopaswa kumwelewa Mtume Paulo na si vinginevyo. Usinikaidi. Ndiyo maana ya kusema pia, “Anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Kor 10:12).
Hivi mtu kudai “NIMEOKOKA” ni kusiganisha wakati wa kitenzi alichotumia Yesu na hiyo ndiyo maana ya “UPINGA KRISTO” na “UPINGA MAANDIKO MATAKATIFU.” Kumbe, kabla mwamini hajamaliza mapambano na ulimwengu huu si maungwana kujinasibu ameokoka. Ni majigambo hatari kabisa kiroho. Kuupata uzima wa milele, ndiyo kukaa kulia na kushoto kwa Mungu, ni tangazo la mwishoni kabisa na litafanywa na Mungu mwenyewe (Mt 25:34, Mk 10:40). Tungalipo hapa duniani chochote kinaweza kutokea wakati wowote. Ndiyo maana Yesu alisema pia, “Wa kwanza watakuwa kuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza” (Mk 10:31). Hii maana yake tuishi tukichelea “kipindupindu cha kiroho.”
Aghalabu, busara hii tunaweza kuikokotoa hata kutoka Agano la Kale, maana humo imeandikwa, “Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe, mtu mgeni wala si midomo yako mwenyewe” (Mit 27:1-2). Na YbS 11:27-28 yanasema, “Tena taabu ya saa moja huleta usahaulifu wa furaha; na mwisho wa mtu ndio ulio ufunuo wa habari zake. Usimwite mtu heri kabla ya kufa kwake; aidha mtu hujulikana kwa kuwatazama watoto wake”. Ndiposa katika busara hii, Waswahili husema, “Kabla hujafa, hujaumbika.”

Yalikuwa Matokeo Tarajiwa
Lakini mwenzenu sikushangaa matokeo hasi baada ya mada ya Mwakesege. Sikushangaa kuwaona Wakatoliki wakisimamishwa kuokoka. Wamesonga mbele “KUOKOKA.” Nilishaandika kwenye mada yangu, “NI MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE”, “Mwamba ngoma ngozi kwake.” Si mmeona wenyewe? Mtu alipewa hadhira ya Wakatoliki, watu anaowatafuta kwa hamu kubwa, basi amewavunia kapuni mwake kilaini kabisa. Nikufikirishe. Kigogota anayefanya kazi kubwa ya kubangua miti akitafuta funza wa kula, panzi akimtua mdomoni pake atamtema? Hii ni aibu kubwa kweli kweli! Wachungaji wa kondoo tunachunga nini? Hapa tumewauza kondoo mchana kweupe. Ni aibu kubwa! Wakatoliki wamesemeshwa “SALA YA TOBA” hadharani na hakuna mkubwa yeyote Mkatoliki aliyepinga hilo kwa mwono wa Kikatoliki.
Tazameni hiyo video. Hakuna mchungaji aliyewalinda kondoo kabisa. Kinyume chake aliyewazoa amepigiwa makofi ya kupongezwa na kushukuriwa. Jamani, Mwakesege ameshinda mbele ya watu tuliompelekea huku tukiona. Mwakasege oyeee! Amewapata watu wetu tele. Je, sasa mtaka ushahidi mwingine wa ujinga wetu? Kumbe, heri na heko maparoko vijana na Askofu wa Iringa kwa hatua mliyochukua! Huku kwingine usingizi wa pono unaendelea kwenye vitanda vya samadari na magodogo ya QFL! Haya twende tu! Lakini ufa huu tusiotaka kuuziba sasa, tujiandae kujenga ukuta! Mwiba huu tusiotaka kuutoa leo, tujiandae miguu kutuzukia matende!
Mzee wenu Pd. Titus Amigu
Umeandika shairi refu sana ila All in all Wakatoliki wameokoka Tena maelfu kwa maelfu....

Wewe ni nani hata upinge....

Na Bado Moto unaendelea...na Sasa litakuwa linafanyika kila mwaka...
 
You see, hata wewe tayari kuna mafundisho yanaelekea kukutoa kwenye kweli. Mfano Mwakasege amesema pale ukiokoka unapigwa chapa right? Kwa andiko gani? Ubatizo ndio chapa na mlango wa Ukristo. Kumjua zaidi Mungu na njia zake ni swala la mafundisho sio kuokoka.

Vipi huoni Waislamu wanaoamua kuacha ya dunia ikiwemo ulevi na kuifuata kikamilifu dini yao waliitwa mbele kuokoka?

Kidogo kidogo utaanza kuacha kitubio, Ekaristi itakuwa ktk picha ya kilokole! Rozali utaiona ni ritual tu! Hii itakuingia kidogo kidogo

Sijasema asialikwe bali tuwe na muongozo ili kulinda tunachoamini. Mwakasege alipania ku promote ulokole! Angalia hekima ya mchungaji Kimaro jana! Hakuingilia msingi unaotutofautisha and he preached very well.
Unakuwa mbishi lakini hujasoma maandiko ni kweli ukiokoka unapigwa Chapa yaani Muhuri...baada ya wokovu unapigwa muhuri wa Roho Mtakatifu
Soma:-

(Waefeso 1:13-14)

Au unafikiri Mwakasege alibuni hayo maneno??
Unapompinga mtu hakikisha na wewe umesoma biblia na kuimaliza ili uwe na uhakika ya kwamba neno hilo ni la kutunga au ni Maandiko.
 
Yaani ukae tu ndani bila kusoma eti unasubiri Roho Mtakatifu akupe elimu! Ndio mnadanganywa hivyo hivyo kwamba kuna hela za miujiza
Mwakasege hajawahi kuwafundisha watu wasisome au wasipate elimu..Yeye mwenyewe ni Msomi na Amewahi kuwa Afisa mipango na Udhibiti...

Pia amewahi kuwa Mshauri wa Raisi kwenye sekta ya Uchumi...kipindi cha rais Mkapa...kamwe hajawahi kupingana na suala la kusoma..

hii ni yako tu umetunga..
 
Naona na Baba askofu Ruwaichi kaandaa kongamano lingine....
Kweli Mafuriko hayazuiwi kwa Mikono
FB_IMG_1654270839631.jpg
 
Mpaka leo pamoja na technolojia ya kupata maarifa kukuwa bado kuna watu mnamuamn huyo mwalimu wenu wa uongo mwakasege?.[emoji16][emoji28]

Inauma ila ndio ukweli huo hakuna mwalimu, nabii, mchungaji wala mwinjilist wa kweli nyakat hizi maana wote wanatumia mafundisho ya uongo yaliyochakachuliwa na mkoloni.

Haijarish wanatumia maneno gan yanayogusa hisia zenu, lkn haiondoi ukweli kwamba hawana Roho wa kweli, bali roho ya mpinga kristo(ant-african spiritual reality),
mafundisho ya hawa walimu wenu yanatoka katika roho inayomiliki dini zote na kila aina ya imani na vitabu vyake

Huyo mtu wenu anawajaza sumu akilin ambayo ni ngumu kuiondoa ukishanasa, ni wengi tulikuwa wafuasi wa huyo mwalimu wenu wa uongo, lkn sasa tumeshazinduka ktk uo usingizi/kifo cha kiroho.

Mkoloni si mjinga kukupeni dini, eti ikukomboe for what? Kwa upendo gani?[emoji16], ukweli mchungu sana na unauma sana, zile siku ambazo ukweli utawekwa wazi tutakimbiana na wengi mtapata ukichaa maana yale mliyoaminishwa mtakuta ni uongo by100%..keep this komenti....
1654276692035.jpg
 
Ni mali yetu. Kama hujui habari ndio hiyo. Wakatoliki ndio wakristo. Nyie wengine ni waasi tu. Ukidhani bibilia imekusanywa na nani Yani labda? Adui yeyote wa ukristo anadeal na kanisa la ulimwengu sio vijikanisa. Vimadhehebu.
La kwako na nani wewe mmatumbi muabudu mizimu. Dini umeletewa lakini jinsi unavyoonyesha chuki dhidi ya wakristo wengine inaonyesha unaweza kuua. Umenifanya mpaka ni nimekufuru shenziii.
 
Back
Top Bottom