Mwalimu Mwakasege kufundisha katika semina ya Karismatiki ya Kanisa Katoliki jijini Dodoma 31/05/2022

Maaskofu gani we mjinga?
Ukiona mtu anakimbilia kutukana basi ameshindwa hoja...
Jadili hoja kwa utulivu acha matusi na Hasira

Tatizo lenu mnadhani ukatoliki ni mali yenu...katoliki siyo mali yenu wala Biblia siyo mali yenu

Katoliki ni mali ya Mungu na Ujue mbinguni hawaendi wakatoliki peke yao....

Yesu siyo mali ya wakatoliki peke yao
Yesu alikuja kwa ajili ya Wote wenye dhambi...

Msalaba siyo kwa ajili ya wakatoliki peke yao msalaba ni kwa ajili ya kila aaminiye....
 
Mh sidhani. Mbona Iringa siyo wamewafungia waumini wote walioenda kwa Mwamposa hadi wakiri imani upya.
Pale Iringa Mtume.Mwamposya alikuwa analala kwenye Nyumba ya Uaskofu Kanisa Katoliki Kihesa
S
 
Akili ya mwakasege ni sawa na mapadri 32.
Acha UPUUZI wewe Unaijua akili za mapadre? Au unadhani ni sawa na hao wachungaji walokole? Mjesuit mmoja ni sawa na hao wachungaji 1000 na Mwakasege ndani.Sema tu wengi hawajachagua maisha ya kuhubiri kwa kelele na kupayuka Bali mafundisho ya ukimya (Monks/Frior)
 
Ukiona mtu anakimbilia kutukana basi ameshindwa hoja...
Jadili hoja kwa utulivu acha matusi na Hasira

Tatizo lenu mnadhani ukatoliki ni mali yenu...katoliki siyo mali yenu wala Biblia siyo mali yenu

Katoliki ni mali ya Mungu na Ujue mbinguni hawaendi wakatoliki peke yao....

Yesu siyo mali ya wakatoliki peke yao
Yesu alikuja kwa ajili ya Wote wenye dhambi...

Msalaba siyo kwa ajili ya wakatoliki peke yao msalaba ni kwa ajili ya kila aaminiye....
Ni mali yetu. Kama hujui habari ndio hiyo. Wakatoliki ndio wakristo. Nyie wengine ni waasi tu. Ukidhani bibilia imekusanywa na nani Yani labda? Adui yeyote wa ukristo anadeal na kanisa la ulimwengu sio vijikanisa. Vimadhehebu.
 
Milembe ina kitanda chako special. Wahi ukatibiwe
Ni mali yetu. Kama hujui habari ndio hiyo. Wakatoliki ndio wakristo. Nyie wengine ni waasi tu. Ukidhani bibilia imekusanywa na nani Yani labda? Adui yeyote wa ukristo anadeal na kanisa la ulimwengu sio vijikanisa. Vimadhehebu.
 
MAPATO YA MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE

Je, mmeona kilichotokea Dodoma? Mmeona? Binafsi yangu nimeona aibu, aibu kubwa. Nimeona haya ya uso, haya tele. Nimeona haya kwa niaba ya Wakatoliki, kwenye kongomano la Dodoma. Nimesikiliza mahubiri ya Mwakesege nikapata ushahidi mkamilifu wa mwendelezo ule ule wa ujinga wetu. Nimesikitika sana. Hata nyie sikilizeni mada hiyo hasa dakika thelathini za mwisho. Ameshinda! Amewateka Wakatoliki kuokoka, sijui wale mapadre wawili waliokuwa wawezeshaji wenza wameokoka nao! Wakatoliki wameokoka baada ya mada! Lakini twendeni pole pole katika mambo mawili leo: ujinga wa lugha za kale za Biblia na uovu wa kiroho.

Ujinga wa Lugha za Kale
Mada ilihusu Sauli kuwa Paulo. Kwa wanaojua lugha za kale zaa Biblia, huu ni ujinga wa wazi kwamba mtu hajui Kiebrania wala Kiyunani (Kigiriki). Niwahabarisheni. “Sauli” na “Paulo” ni matamshi ya jina moja lile lile lakini kadiri ya makabila tofauti tu, wala hakuna maana yoyote ya mabadiliko ya kitu ama mtu. Mapadre waliokuwapo pale walipaswa walau kukanusha mada hii, maana bila shaka walihudhuria vipindi vya lugha za Kiebrania na Kiyunani (Kigiriki) Seminarini. Lakini huenda walikuwa wanapenda sana kipindi cha mapumziko!
Nisikilizeni vyema. Jina “Sauli” ndiyo matamshi ya Kiebrania, yaani kwa lugha ya Wayahudi, wakati “Paulo” ni matamshi ya Kiyunani au Kigiriki kwa watu wa mataifa. Yaani kwa “SAULI” ndivyo alivyokuwa anaitwa alipokuwa anafanya uinjilishaji kati ya Wayahudi wenzake, lakini baadaye alipohamia kwa watu wa mataifa katika Asia Ndogo, Ugiriki na Roma, watu wa huko ndiyo wakawa wanamwita “PAULO.” Aidha, matamshi ya “PAULO” ni ya Kilatini vile vile. Ndiyo maana yanatumika matamshi ya “PAULO” katika nusu ya Kitabu cha Matendo ya Mitume, si vinginevyo. Hakuna suala la kiteolojia hapo.
Kwa hili, hebu niwadarasisheni kwa mifano midogo miwili. Mtu anayeitwa “CLARE” nchini Uingereza na Marekani, wanakozungumza Kiingereza, ataitwa “CIARA” nchini Italia wanakozungumza Kiitaliano, ataitwa “KLARA” hapa Tanzania maana tunatamka kwa Kiswahili, lakini huyo huyo ataitwa “KALALA” huko Songea kwani wanatamka Kingoni.
Mfano mwingine. Mtu anayeitwa “YAKOBO” huku kwetu Tanzania, ataitwa “JAMES” huko Uingereza, ataitwa “JIMMY” huko Marekani, ataitwa “DIEGO” huko Argentina wanakozungumza Kihispania na ataitwa “TIAGO” huko Ureno, Brazili, Angola na Msumbiji wanakozungumza Kireno. Hivi ni ujinga wa lugha tu kuhubiri kwamba kulikuwa na kitu katika kutoka matamshi “SAULI” kwenda “PAULO.” Kwa vyovyote hili ni jambo dogo na lenye kutibika.

Uovu wa Kiroho – “Wakatoliki Kuokoka”
Uovu wa kusikitikiwa zaidi ni uharibifu uliofanywa na mkutano huo. Hakika haya ni madhara yatakayohitaji JIK kuoshwa. Wakatoliki wamehubiriwa waokoke licha ya kwamba kwa sakramenti ya Ubatizo walishafanyika Wakristo Wakatoliki. Wamekubalishwa kwamba walikuwa na upungufu kiroho. Wamekubali kuokoka, jambo ambalo maana yake ni kupingana na Yesu pamwe na Maandiko Matakatifu. Haya ni mapato ya ujinga ule ule niliokuwa nimeudokeza hapo mwanzo. Watu wetu hawajui “lipi ni la Kikatoliki” na “lipi si la Kikatoliki.” Wanapokea na kula vyote. Asalale! Hawana uwezo wa kupambanua “SUPU” na “SUMU.” Hawana uwezo wa kupambanua “KARIBU” na “KALIBU.” Alahaula!
Kwa hili, msishawishike kuniita nabii maana ilikuwa hatari ya wazi. Hata mlemavu wa macho aliweza kuiona. Hata mlemavu wa masikio aliweza kuisikia. Hata mlemavu wa miguu angeliweza kuikimbia.
Sikilizeni. Sisi Wakatoliki hatuthubutu kupingana na Yesu kwa kujinasibu TUMEOKOKA kwa sababu Yesu mwenyewe aliliweka jambo hilo katika wakati ujao (future tense) – ATA… na siyo wakati uliotimilika (perfect tense) – AME…. Soma alivyosema Yesu mwenyewe, “Mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye ATAKAYEOKOKA” (Mk 13:13). Hata Mtume Paulo tumsome vizuri. Mtume Paulo ameandika, “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa kukiri hata kupata wokovu – yaani mwishoni mwa maisha haya siyo sasa” (Rum 10:9-10). Hivi ndivyo tunavyopaswa kumwelewa Mtume Paulo na si vinginevyo. Usinikaidi. Ndiyo maana ya kusema pia, “Anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Kor 10:12).
Hivi mtu kudai “NIMEOKOKA” ni kusiganisha wakati wa kitenzi alichotumia Yesu na hiyo ndiyo maana ya “UPINGA KRISTO” na “UPINGA MAANDIKO MATAKATIFU.” Kumbe, kabla mwamini hajamaliza mapambano na ulimwengu huu si maungwana kujinasibu ameokoka. Ni majigambo hatari kabisa kiroho. Kuupata uzima wa milele, ndiyo kukaa kulia na kushoto kwa Mungu, ni tangazo la mwishoni kabisa na litafanywa na Mungu mwenyewe (Mt 25:34, Mk 10:40). Tungalipo hapa duniani chochote kinaweza kutokea wakati wowote. Ndiyo maana Yesu alisema pia, “Wa kwanza watakuwa kuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza” (Mk 10:31). Hii maana yake tuishi tukichelea “kipindupindu cha kiroho.”
Aghalabu, busara hii tunaweza kuikokotoa hata kutoka Agano la Kale, maana humo imeandikwa, “Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe, mtu mgeni wala si midomo yako mwenyewe” (Mit 27:1-2). Na YbS 11:27-28 yanasema, “Tena taabu ya saa moja huleta usahaulifu wa furaha; na mwisho wa mtu ndio ulio ufunuo wa habari zake. Usimwite mtu heri kabla ya kufa kwake; aidha mtu hujulikana kwa kuwatazama watoto wake”. Ndiposa katika busara hii, Waswahili husema, “Kabla hujafa, hujaumbika.”

Yalikuwa Matokeo Tarajiwa
Lakini mwenzenu sikushangaa matokeo hasi baada ya mada ya Mwakesege. Sikushangaa kuwaona Wakatoliki wakisimamishwa kuokoka. Wamesonga mbele “KUOKOKA.” Nilishaandika kwenye mada yangu, “NI MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE”, “Mwamba ngoma ngozi kwake.” Si mmeona wenyewe? Mtu alipewa hadhira ya Wakatoliki, watu anaowatafuta kwa hamu kubwa, basi amewavunia kapuni mwake kilaini kabisa. Nikufikirishe. Kigogota anayefanya kazi kubwa ya kubangua miti akitafuta funza wa kula, panzi akimtua mdomoni pake atamtema? Hii ni aibu kubwa kweli kweli! Wachungaji wa kondoo tunachunga nini? Hapa tumewauza kondoo mchana kweupe. Ni aibu kubwa! Wakatoliki wamesemeshwa “SALA YA TOBA” hadharani na hakuna mkubwa yeyote Mkatoliki aliyepinga hilo kwa mwono wa Kikatoliki.
Tazameni hiyo video. Hakuna mchungaji aliyewalinda kondoo kabisa. Kinyume chake aliyewazoa amepigiwa makofi ya kupongezwa na kushukuriwa. Jamani, Mwakesege ameshinda mbele ya watu tuliompelekea huku tukiona. Mwakasege oyeee! Amewapata watu wetu tele. Je, sasa mtaka ushahidi mwingine wa ujinga wetu? Kumbe, heri na heko maparoko vijana na Askofu wa Iringa kwa hatua mliyochukua! Huku kwingine usingizi wa pono unaendelea kwenye vitanda vya samadari na magodogo ya QFL! Haya twende tu! Lakini ufa huu tusiotaka kuuziba sasa, tujiandae kujenga ukuta! Mwiba huu tusiotaka kuutoa leo, tujiandae miguu kutuzukia matende!
Mzee wenu Pd. Titus Amigu
 
Natamani Wakarismatik wayasome haya na Mapadre pia wayasome.

KASORO 3 ZINAZOLITAFUNA KANISA KATOLIKI.
1.Waamini wapenda miujiza na mbingu ya mtelemkoni.
2.Mapdre wavivu wa kujiandaa na kufundisha imani kwa waamini. Wapo mapadre wanaojitoa kwa bidii ili kukizi kiu ya wahitaji lakini kumekuwa wimbi kubwa la mapdre wasio jishughulisha kabisa katika kifundisha imani katoliki.
3.Kukosa umoja wa kiimani na ufahamu. Yaani viongozi wa kanisa wako pande mbili. Wapo wanaohafiki ukarismatiki na wanaopinga. Yaani kifupi ni kwamba kikosi kimoja kina wanajeshi wanaopingana kimikakati. Kuna hatari hapo,kuna mwanya katikati na kupitia huo mwanya adui lazima atakuja kwa staili ya Bruce Lee.
 
Nakubaliana na Padre Amigu. Hivi Mkatoliki wa kawaida baada ya pale umemuachia maswali gani juu ya sala ile ya toba na kitubio? Umemuachia maswali gani juu ya ubatizo wake uliomfanya awe Mkristo? Kwamba kwa ile sala fupi ndio ameokoka? Nilitegemea ufafanuzi mfupi kwa Wakatoliki ili wajue wanachofanya kama hatua za kuamua kubadilika.

Hivi hatuoni Wakristo akina Paulo wakiwakemea kwa dhambi na mwenendo mbovu? Waliambiwa hawajaokoka au watubu? Hivi pale ndio unakuwa umempokea Yesu? Unamjua Yesu unayempokea kwa Ekaristi?

Ukweli ni huu, kwavile sisi Wakatoliki, mapadre kwa asilimia nyingi tumekuwa wavivu wa kuhubiri kweli, acha kweli nyingine ituhubiri. Hata mitume Kanisa lilipozidi walichagua baada ya kufunga na kuomba baadhi ya waamini kuhudumu meza ya Bwana ili wao wapate muda wa kwenda kulisha watu neno.

Maaskofu wanapaswa kuona dharura ya kuanza kufundisha imani ya kweli! Wakristo wote ( si Wakatoliki tu) wana kiu ya kweli ambayo inapatikana kama bidhaa hadhimu!
 
ni kwa vile tu kuna uhuru wa kuongea. Elimu ya Padre sio ya kitoto mzee
Nyie hamna akil nyote!! Suala la MUNGU halihitaji elimu mnayoijua nyie makanjanja...elimu ya MUNGU anakupa yeye mwenyewe kwa kazi maalumu kupitia ROHO MTAKATIFU. YESU alihubir injili miaka 3 hakwenda kusoma chuochote..wala hakwenda kufundshwa na walimu wa torati..lakin alikuwa anawapiga maswali hao walimu wa torati had wanapoteana! Someni biblia nyie watoto wa mama maria
 
MAPATO YA MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE

Je, mmeona kilichotokea Dodoma? Mmeona? Binafsi yangu nimeona aibu, aibu kubwa. Nimeona haya ya uso, haya tele. Nimeona haya kwa niaba ya Wakatoliki, kwenye kongomano la Dodoma. Nimesikiliza mahubiri ya Mwakesege nikapata ushahidi mkamilifu wa mwendelezo ule ule wa ujinga wetu. Nimesikitika sana. Hata nyie sikilizeni mada hiyo hasa dakika thelathini za mwisho. Ameshinda! Amewateka Wakatoliki kuokoka, sijui wale mapadre wawili waliokuwa wawezeshaji wenza wameokoka nao! Wakatoliki wameokoka baada ya mada! Lakini twendeni pole pole katika mambo mawili leo: ujinga wa lugha za kale za Biblia na uovu wa kiroho.

Ujinga wa Lugha za Kale
Mada ilihusu Sauli kuwa Paulo. Kwa wanaojua lugha za kale zaa Biblia, huu ni ujinga wa wazi kwamba mtu hajui Kiebrania wala Kiyunani (Kigiriki). Niwahabarisheni. “Sauli” na “Paulo” ni matamshi ya jina moja lile lile lakini kadiri ya makabila tofauti tu, wala hakuna maana yoyote ya mabadiliko ya kitu ama mtu. Mapadre waliokuwapo pale walipaswa walau kukanusha mada hii, maana bila shaka walihudhuria vipindi vya lugha za Kiebrania na Kiyunani (Kigiriki) Seminarini. Lakini huenda walikuwa wanapenda sana kipindi cha mapumziko!
Nisikilizeni vyema. Jina “Sauli” ndiyo matamshi ya Kiebrania, yaani kwa lugha ya Wayahudi, wakati “Paulo” ni matamshi ya Kiyunani au Kigiriki kwa watu wa mataifa. Yaani kwa “SAULI” ndivyo alivyokuwa anaitwa alipokuwa anafanya uinjilishaji kati ya Wayahudi wenzake, lakini baadaye alipohamia kwa watu wa mataifa katika Asia Ndogo, Ugiriki na Roma, watu wa huko ndiyo wakawa wanamwita “PAULO.” Aidha, matamshi ya “PAULO” ni ya Kilatini vile vile. Ndiyo maana yanatumika matamshi ya “PAULO” katika nusu ya Kitabu cha Matendo ya Mitume, si vinginevyo. Hakuna suala la kiteolojia hapo.
Kwa hili, hebu niwadarasisheni kwa mifano midogo miwili. Mtu anayeitwa “CLARE” nchini Uingereza na Marekani, wanakozungumza Kiingereza, ataitwa “CIARA” nchini Italia wanakozungumza Kiitaliano, ataitwa “KLARA” hapa Tanzania maana tunatamka kwa Kiswahili, lakini huyo huyo ataitwa “KALALA” huko Songea kwani wanatamka Kingoni.
Mfano mwingine. Mtu anayeitwa “YAKOBO” huku kwetu Tanzania, ataitwa “JAMES” huko Uingereza, ataitwa “JIMMY” huko Marekani, ataitwa “DIEGO” huko Argentina wanakozungumza Kihispania na ataitwa “TIAGO” huko Ureno, Brazili, Angola na Msumbiji wanakozungumza Kireno. Hivi ni ujinga wa lugha tu kuhubiri kwamba kulikuwa na kitu katika kutoka matamshi “SAULI” kwenda “PAULO.” Kwa vyovyote hili ni jambo dogo na lenye kutibika.

Uovu wa Kiroho – “Wakatoliki Kuokoka”
Uovu wa kusikitikiwa zaidi ni uharibifu uliofanywa na mkutano huo. Hakika haya ni madhara yatakayohitaji JIK kuoshwa. Wakatoliki wamehubiriwa waokoke licha ya kwamba kwa sakramenti ya Ubatizo walishafanyika Wakristo Wakatoliki. Wamekubalishwa kwamba walikuwa na upungufu kiroho. Wamekubali kuokoka, jambo ambalo maana yake ni kupingana na Yesu pamwe na Maandiko Matakatifu. Haya ni mapato ya ujinga ule ule niliokuwa nimeudokeza hapo mwanzo. Watu wetu hawajui “lipi ni la Kikatoliki” na “lipi si la Kikatoliki.” Wanapokea na kula vyote. Asalale! Hawana uwezo wa kupambanua “SUPU” na “SUMU.” Hawana uwezo wa kupambanua “KARIBU” na “KALIBU.” Alahaula!
Kwa hili, msishawishike kuniita nabii maana ilikuwa hatari ya wazi. Hata mlemavu wa macho aliweza kuiona. Hata mlemavu wa masikio aliweza kuisikia. Hata mlemavu wa miguu angeliweza kuikimbia.
Sikilizeni. Sisi Wakatoliki hatuthubutu kupingana na Yesu kwa kujinasibu TUMEOKOKA kwa sababu Yesu mwenyewe aliliweka jambo hilo katika wakati ujao (future tense) – ATA… na siyo wakati uliotimilika (perfect tense) – AME…. Soma alivyosema Yesu mwenyewe, “Mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye ATAKAYEOKOKA” (Mk 13:13). Hata Mtume Paulo tumsome vizuri. Mtume Paulo ameandika, “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa kukiri hata kupata wokovu – yaani mwishoni mwa maisha haya siyo sasa” (Rum 10:9-10). Hivi ndivyo tunavyopaswa kumwelewa Mtume Paulo na si vinginevyo. Usinikaidi. Ndiyo maana ya kusema pia, “Anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Kor 10:12).
Hivi mtu kudai “NIMEOKOKA” ni kusiganisha wakati wa kitenzi alichotumia Yesu na hiyo ndiyo maana ya “UPINGA KRISTO” na “UPINGA MAANDIKO MATAKATIFU.” Kumbe, kabla mwamini hajamaliza mapambano na ulimwengu huu si maungwana kujinasibu ameokoka. Ni majigambo hatari kabisa kiroho. Kuupata uzima wa milele, ndiyo kukaa kulia na kushoto kwa Mungu, ni tangazo la mwishoni kabisa na litafanywa na Mungu mwenyewe (Mt 25:34, Mk 10:40). Tungalipo hapa duniani chochote kinaweza kutokea wakati wowote. Ndiyo maana Yesu alisema pia, “Wa kwanza watakuwa kuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza” (Mk 10:31). Hii maana yake tuishi tukichelea “kipindupindu cha kiroho.”
Aghalabu, busara hii tunaweza kuikokotoa hata kutoka Agano la Kale, maana humo imeandikwa, “Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe, mtu mgeni wala si midomo yako mwenyewe” (Mit 27:1-2). Na YbS 11:27-28 yanasema, “Tena taabu ya saa moja huleta usahaulifu wa furaha; na mwisho wa mtu ndio ulio ufunuo wa habari zake. Usimwite mtu heri kabla ya kufa kwake; aidha mtu hujulikana kwa kuwatazama watoto wake”. Ndiposa katika busara hii, Waswahili husema, “Kabla hujafa, hujaumbika.”

Yalikuwa Matokeo Tarajiwa
Lakini mwenzenu sikushangaa matokeo hasi baada ya mada ya Mwakesege. Sikushangaa kuwaona Wakatoliki wakisimamishwa kuokoka. Wamesonga mbele “KUOKOKA.” Nilishaandika kwenye mada yangu, “NI MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE”, “Mwamba ngoma ngozi kwake.” Si mmeona wenyewe? Mtu alipewa hadhira ya Wakatoliki, watu anaowatafuta kwa hamu kubwa, basi amewavunia kapuni mwake kilaini kabisa. Nikufikirishe. Kigogota anayefanya kazi kubwa ya kubangua miti akitafuta funza wa kula, panzi akimtua mdomoni pake atamtema? Hii ni aibu kubwa kweli kweli! Wachungaji wa kondoo tunachunga nini? Hapa tumewauza kondoo mchana kweupe. Ni aibu kubwa! Wakatoliki wamesemeshwa “SALA YA TOBA” hadharani na hakuna mkubwa yeyote Mkatoliki aliyepinga hilo kwa mwono wa Kikatoliki.
Tazameni hiyo video. Hakuna mchungaji aliyewalinda kondoo kabisa. Kinyume chake aliyewazoa amepigiwa makofi ya kupongezwa na kushukuriwa. Jamani, Mwakesege ameshinda mbele ya watu tuliompelekea huku tukiona. Mwakasege oyeee! Amewapata watu wetu tele. Je, sasa mtaka ushahidi mwingine wa ujinga wetu? Kumbe, heri na heko maparoko vijana na Askofu wa Iringa kwa hatua mliyochukua! Huku kwingine usingizi wa pono unaendelea kwenye vitanda vya samadari na magodogo ya QFL! Haya twende tu! Lakini ufa huu tusiotaka kuuziba sasa, tujiandae kujenga ukuta! Mwiba huu tusiotaka kuutoa leo, tujiandae miguu kutuzukia matende!
Mzee wenu Pd. Titus Amigu
Hii ungepandisha kama thread kabisa wa kujitegemea kule juu afu ukamtag johnthebaptist
 
paqwa
Duh Mungu atusaidie sana... !!

Au mkuu mimi ndio ninakuelewa vibaya, unamaanisha siku hiyo ya hukumu Yesu atasimama mlangoni kuhoji kama mtu ni Mkatoliki ndio anaingia mbinguni na wengine ambao sio wakatoliki kwao ni jehanamu?? Au sijakuelewa vizuri!?
 
Nyie hamna akil nyote!! Suala la MUNGU halihitaji elimu mnayoijua nyie makanjanja...elimu ya MUNGU anakupa yeye mwenyewe kwa kazi maalumu kupitia ROHO MTAKATIFU. YESU alihubir injili miaka 3 hakwenda kusoma chuochote..wala hakwenda kufundshwa na walimu wa torati..lakin alikuwa anawapiga maswali hao walimu wa torati had wanapoteana! Someni biblia nyie watoto wa mama maria
Kama elimu si muhimu Yesu asingechagua watu 12 maalum na kuwafundisha kwa miaka 3 ikiwemo practically. Sauli alipewa kazi na Yesu lakini hakumwambia nenda kafungue Kanisa! Alimuagiza kwa mitume na alikaa nao kipindi kirefu kabla Roho Mtakatifu hajaagiza mitume wawatume kuhubiri! Wewe ukitokewa na Yesu live si utafungua Kanisa haraka haraka?

Hapo mwisho nimependa zaidi...kweli sisi ni watoto wa Mama yetu tunayempenda sana Bikira Maria! Huyu ndio Eva mpya! Eva ndio mama wa wote wenye mwili, Bikira Maria ndio mama wa Wakristo! Yesu akiwa mzaliwa wa kwanza na sisi nduguze!

Mimi ni nani nisimpe heshima ya kipekee kama Mungu muumba wangu alimchagua kuwa mama yake na kumpa mwili ambao ndio uliotukomboa kwa mauti yake? Mimi ni nani nisimpe heshima ya pekee kama Elizabeth akijawa Roho Mtakatifu alisema "imekuwaje mama wa Bwana wangu kunitembelea?"

Kama jinsi Yesu alivyoishika torati alizishika amri kumi za Mungu ikiwemo ya nne waheshimu baba na mama...? Kama Yesu aliye mtu kweli na Mungu kweli alimheshimu mama yake, mimi nani nisitoe upekee kwenye hilo?

Hivi unavyosema nyie watoto wa Maria kwa kejeli huoni unamkejeli mama wa Bwana wako? Unafikiri Yesu anafurahi mnavyo mdegrade mama yake ili kuwa prove wrong Wakatoliki?
 
MAPATO YA MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE

Je, mmeona kilichotokea Dodoma? Mmeona? Binafsi yangu nimeona aibu, aibu kubwa. Nimeona haya ya uso, haya tele. Nimeona haya kwa niaba ya Wakatoliki, kwenye kongomano la Dodoma. Nimesikiliza mahubiri ya Mwakesege nikapata ushahidi mkamilifu wa mwendelezo ule ule wa ujinga wetu. Nimesikitika sana. Hata nyie sikilizeni mada hiyo hasa dakika thelathini za mwisho. Ameshinda! Amewateka Wakatoliki kuokoka, sijui wale mapadre wawili waliokuwa wawezeshaji wenza wameokoka nao! Wakatoliki wameokoka baada ya mada! Lakini twendeni pole pole katika mambo mawili leo: ujinga wa lugha za kale za Biblia na uovu wa kiroho.

Ujinga wa Lugha za Kale
Mada ilihusu Sauli kuwa Paulo. Kwa wanaojua lugha za kale zaa Biblia, huu ni ujinga wa wazi kwamba mtu hajui Kiebrania wala Kiyunani (Kigiriki). Niwahabarisheni. “Sauli” na “Paulo” ni matamshi ya jina moja lile lile lakini kadiri ya makabila tofauti tu, wala hakuna maana yoyote ya mabadiliko ya kitu ama mtu. Mapadre waliokuwapo pale walipaswa walau kukanusha mada hii, maana bila shaka walihudhuria vipindi vya lugha za Kiebrania na Kiyunani (Kigiriki) Seminarini. Lakini huenda walikuwa wanapenda sana kipindi cha mapumziko!
Nisikilizeni vyema. Jina “Sauli” ndiyo matamshi ya Kiebrania, yaani kwa lugha ya Wayahudi, wakati “Paulo” ni matamshi ya Kiyunani au Kigiriki kwa watu wa mataifa. Yaani kwa “SAULI” ndivyo alivyokuwa anaitwa alipokuwa anafanya uinjilishaji kati ya Wayahudi wenzake, lakini baadaye alipohamia kwa watu wa mataifa katika Asia Ndogo, Ugiriki na Roma, watu wa huko ndiyo wakawa wanamwita “PAULO.” Aidha, matamshi ya “PAULO” ni ya Kilatini vile vile. Ndiyo maana yanatumika matamshi ya “PAULO” katika nusu ya Kitabu cha Matendo ya Mitume, si vinginevyo. Hakuna suala la kiteolojia hapo.
Kwa hili, hebu niwadarasisheni kwa mifano midogo miwili. Mtu anayeitwa “CLARE” nchini Uingereza na Marekani, wanakozungumza Kiingereza, ataitwa “CIARA” nchini Italia wanakozungumza Kiitaliano, ataitwa “KLARA” hapa Tanzania maana tunatamka kwa Kiswahili, lakini huyo huyo ataitwa “KALALA” huko Songea kwani wanatamka Kingoni.
Mfano mwingine. Mtu anayeitwa “YAKOBO” huku kwetu Tanzania, ataitwa “JAMES” huko Uingereza, ataitwa “JIMMY” huko Marekani, ataitwa “DIEGO” huko Argentina wanakozungumza Kihispania na ataitwa “TIAGO” huko Ureno, Brazili, Angola na Msumbiji wanakozungumza Kireno. Hivi ni ujinga wa lugha tu kuhubiri kwamba kulikuwa na kitu katika kutoka matamshi “SAULI” kwenda “PAULO.” Kwa vyovyote hili ni jambo dogo na lenye kutibika.

Uovu wa Kiroho – “Wakatoliki Kuokoka”
Uovu wa kusikitikiwa zaidi ni uharibifu uliofanywa na mkutano huo. Hakika haya ni madhara yatakayohitaji JIK kuoshwa. Wakatoliki wamehubiriwa waokoke licha ya kwamba kwa sakramenti ya Ubatizo walishafanyika Wakristo Wakatoliki. Wamekubalishwa kwamba walikuwa na upungufu kiroho. Wamekubali kuokoka, jambo ambalo maana yake ni kupingana na Yesu pamwe na Maandiko Matakatifu. Haya ni mapato ya ujinga ule ule niliokuwa nimeudokeza hapo mwanzo. Watu wetu hawajui “lipi ni la Kikatoliki” na “lipi si la Kikatoliki.” Wanapokea na kula vyote. Asalale! Hawana uwezo wa kupambanua “SUPU” na “SUMU.” Hawana uwezo wa kupambanua “KARIBU” na “KALIBU.” Alahaula!
Kwa hili, msishawishike kuniita nabii maana ilikuwa hatari ya wazi. Hata mlemavu wa macho aliweza kuiona. Hata mlemavu wa masikio aliweza kuisikia. Hata mlemavu wa miguu angeliweza kuikimbia.
Sikilizeni. Sisi Wakatoliki hatuthubutu kupingana na Yesu kwa kujinasibu TUMEOKOKA kwa sababu Yesu mwenyewe aliliweka jambo hilo katika wakati ujao (future tense) – ATA… na siyo wakati uliotimilika (perfect tense) – AME…. Soma alivyosema Yesu mwenyewe, “Mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye ATAKAYEOKOKA” (Mk 13:13). Hata Mtume Paulo tumsome vizuri. Mtume Paulo ameandika, “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa kukiri hata kupata wokovu – yaani mwishoni mwa maisha haya siyo sasa” (Rum 10:9-10). Hivi ndivyo tunavyopaswa kumwelewa Mtume Paulo na si vinginevyo. Usinikaidi. Ndiyo maana ya kusema pia, “Anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Kor 10:12).
Hivi mtu kudai “NIMEOKOKA” ni kusiganisha wakati wa kitenzi alichotumia Yesu na hiyo ndiyo maana ya “UPINGA KRISTO” na “UPINGA MAANDIKO MATAKATIFU.” Kumbe, kabla mwamini hajamaliza mapambano na ulimwengu huu si maungwana kujinasibu ameokoka. Ni majigambo hatari kabisa kiroho. Kuupata uzima wa milele, ndiyo kukaa kulia na kushoto kwa Mungu, ni tangazo la mwishoni kabisa na litafanywa na Mungu mwenyewe (Mt 25:34, Mk 10:40). Tungalipo hapa duniani chochote kinaweza kutokea wakati wowote. Ndiyo maana Yesu alisema pia, “Wa kwanza watakuwa kuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza” (Mk 10:31). Hii maana yake tuishi tukichelea “kipindupindu cha kiroho.”
Aghalabu, busara hii tunaweza kuikokotoa hata kutoka Agano la Kale, maana humo imeandikwa, “Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe, mtu mgeni wala si midomo yako mwenyewe” (Mit 27:1-2). Na YbS 11:27-28 yanasema, “Tena taabu ya saa moja huleta usahaulifu wa furaha; na mwisho wa mtu ndio ulio ufunuo wa habari zake. Usimwite mtu heri kabla ya kufa kwake; aidha mtu hujulikana kwa kuwatazama watoto wake”. Ndiposa katika busara hii, Waswahili husema, “Kabla hujafa, hujaumbika.”

Yalikuwa Matokeo Tarajiwa
Lakini mwenzenu sikushangaa matokeo hasi baada ya mada ya Mwakesege. Sikushangaa kuwaona Wakatoliki wakisimamishwa kuokoka. Wamesonga mbele “KUOKOKA.” Nilishaandika kwenye mada yangu, “NI MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE”, “Mwamba ngoma ngozi kwake.” Si mmeona wenyewe? Mtu alipewa hadhira ya Wakatoliki, watu anaowatafuta kwa hamu kubwa, basi amewavunia kapuni mwake kilaini kabisa. Nikufikirishe. Kigogota anayefanya kazi kubwa ya kubangua miti akitafuta funza wa kula, panzi akimtua mdomoni pake atamtema? Hii ni aibu kubwa kweli kweli! Wachungaji wa kondoo tunachunga nini? Hapa tumewauza kondoo mchana kweupe. Ni aibu kubwa! Wakatoliki wamesemeshwa “SALA YA TOBA” hadharani na hakuna mkubwa yeyote Mkatoliki aliyepinga hilo kwa mwono wa Kikatoliki.
Tazameni hiyo video. Hakuna mchungaji aliyewalinda kondoo kabisa. Kinyume chake aliyewazoa amepigiwa makofi ya kupongezwa na kushukuriwa. Jamani, Mwakesege ameshinda mbele ya watu tuliompelekea huku tukiona. Mwakasege oyeee! Amewapata watu wetu tele. Je, sasa mtaka ushahidi mwingine wa ujinga wetu? Kumbe, heri na heko maparoko vijana na Askofu wa Iringa kwa hatua mliyochukua! Huku kwingine usingizi wa pono unaendelea kwenye vitanda vya samadari na magodogo ya QFL! Haya twende tu! Lakini ufa huu tusiotaka kuuziba sasa, tujiandae kujenga ukuta! Mwiba huu tusiotaka kuutoa leo, tujiandae miguu kutuzukia matende!
Mzee wenu Pd. Titus Amigu
Hahahaha mkuu we tulia yani nimebarikiwa na kongamano lile na vile Mungu amemtumia mtumishi wake Mwl. Mwakasege kwa viwango vya juu...yani mahubiri yale adi mapadre walibaki wanatafakari..

Huu ni wakati wa uamsho na watu wanapata nafasi ya kuijua ile kweli na hakika itawaweka huru!!
Mkuu nikushauri usiwe close minded, jaribu kumsikiliza Mwl. Mwakasege hata kwa mahubiri yake mengine pasipo kutanguliza ubaguzi kua huyu ni Mlutheri na mimi ni Mkatoliki, acha Roho Mtakatifu ajifunue mwenyewe!!

Nb: Mimi ni Mkatoliki ila sijifungi eti sitaki kusikiliza mahubiri ya fulani kwa kua si dhehebu langu..namshukuru sana Mungu kwa hilo kwani nimefahamu na ninaendelea kufahamu ukweli ni upi!!!
 
Duh Mungu atusaidie sana... !!

Au mkuu mimi ndio ninakuelewa vibaya, unamaanisha siku hiyo ya hukumu Yesu atasimama mlangoni kuhoji kama mtu ni Mkatoliki ndio anaingia mbinguni na wengine ambao sio wakatoliki kwao ni jehanamu?? Au sijakuelewa vizuri!?
Ukisema Mkatoliki inakaa kidhehebu kwa mtazamo wa zama zetu lakini maana yake ni imani ya kweli. Imani ya kweli ni ipi ni mjadala mrefu! Mfano kama wewe si Mkatoliki fahamu huamini uwepo wa Yesu hai katika Ekaristi ( mwili na damu yake). Nje ya Kanisa Katoliki wanachukulia kama alama na kumbukumbu tu! Ndio maana wanafanya meza ya Bwana wanavyotaka! Wengine hata wewe unaweza kuji fanyia meza ya Bwana! Purely unbiblical!

Sasa bila Ekaristi tayari Ukristo una shida ambayo wengi hawaioni tukiwemo sisi Wakatoliki! Hakuna fundisho Yesu alifundisha watu hawakumuelewa na mbaya zaidi waliamua kumuacha kama juu ya mwili na damu yake katika maumbo ya mkate na divai! Ukizama kwa kina juu ya fundisho hili utaanza kuelewa nini nimemaanisha!
 
Hahahaha mkuu we tulia yani nimebarikiwa na kongamano lile na vile Mungu amemtumia mtumishi wake Mwl. Mwakasege kwa viwango vya juu...yani mahubiri yale adi mapadre walibaki wanatafakari..

Huu ni wakati wa uamsho na watu wanapata nafasi ya kuijua ile kweli na hakika itawaweka huru!!
Mkuu nikushauri usiwe close minded, jaribu kumsikiliza Mwl. Mwakasege hata kwa mahubiri yake mengine pasipo kutanguliza ubaguzi kua huyu ni Mlutheri na mimi ni Mkatoliki, acha Roho Mtakatifu ajifunue mwenyewe!!

Nb: Mimi ni Mkatoliki ila sijifungi eti sitaki kusikiliza mahubiri ya fulani kwa kua si dhehebu langu..namshukuru sana Mungu kwa hilo kwani nimefahamu na ninaendelea kufahamu ukweli ni upi!!!
Usijifunge kusikiliza mahubiri lakini lazima uwe unajua imani yako vizuri kinyume chake utapepea na kila upepo wa mafundisho.

Ni kosa kusema hadi Mapadre wamejitafakari, hakika itakuwa ndani yao wanapata shida kuvumilia baadhi ya upotofu lakini kuhubiri habari za wokovu ni jukumu lao la msingi na hawawezi kupata shida na mtu anayehubiri hiyo kweli. Habari njema au injili ndio wokovu wenyewe sio ile sala ya dakika 2 kwamba sasa ndio umeokoka!

Wokovu sio tukio la mara moja ...ni safari ndio maana maandiko yanasema atakayevumilia hata mwisho ataokoka! Tatizo ni mapungufu yetu kwenye mafundisho lakini ni hatari madhaifu hayo yakitumika kutafuta ovyo kushiba nje ya utaratibu! Njaa haipaswi kukufanya ule chochote bali utatafuta kinachofaa!
 
Back
Top Bottom