Mwalimu Mwakasege kufundisha katika semina ya Karismatiki ya Kanisa Katoliki jijini Dodoma 31/05/2022

Mwalimu Mwakasege kufundisha katika semina ya Karismatiki ya Kanisa Katoliki jijini Dodoma 31/05/2022

Yaani hao waliompa mwaliko watashushiwa ban na kanisa katoliki. Hawataamini macho na masikio yao. Yetu macho
Soma heading vizuri.
Hawa ni wa RC waliojitenga sio wale og
 
Katoliki karismatiki na walokole hamna tofauti na style Yao ya kuabudu ni moja...Hilo kanisa lao hapo ubungo nilikuwa naona wanaalika wachungaji kibao wao kilokole kutoka nchi nyingi ..sijajua mgogoro wa katoliki main na katoliki karismatiki ulishavipi ndio maana zamani walikuwa wanakatazwa kuingia kwenye makanisa Yao...
 
Huyu mzee nikiwaga kwenye wifi iliyotulia huwa nachukuaga madini kwake.

Yuko smart sana huyu mzee.
Hebu tushikishe hayo "Madini" aliyonayo! Hivi amesoma Chuo au Vyuo gani vinavyotambulika vya Teolojia hapa Duniani? Na je Ni Mmoja wa Majalimu wa Teolojia hapa Tanzania?
 
Nami nililiona hilo. Labda angealika ambao tayari wameokoka na wako kwenye utumishi. Kuna watu walikuja kuombewa tu au kuokoka. Kama walikuwepo walio kwenye utumishi, basi walikuwa kiduchu mno!
Mtu unapaswa kwanza kujiuliza upako ni nini?

Je kuna mifano ya upako wa aina hizo mbili katika Biblia?
Kama hakuna achana na hayo mafundisho.

Kwa ufupi ni kuwa upako ni tendo lilotumika katka Agano la kale kwa wafalme, nabii na kuhani. Ilikuwa ni ishara ya nguvu katika huduma zao.

Katika Agano jipya upako ni Roho Mtakatifu, mfano Yesu anasema Roho wa Bwana yu juu yangu amenipaka mafuta kuwahubiri maskini ....Lk 4:18.

Unaposema upako wa wito na wa kazi unamaana ya Roho Mtakatifu mara mbili?

Fanya utafiti
 
Hebu tushikishe hayo "Madini" aliyonayo! Hivi amesoma Chuo au Vyuo gani vinavyotambulika vya Teolojia hapa Duniani? Na je Ni Mmoja wa Majalimu wa Teolojia hapa Tanzania?
Uko sawa swali lako angalia uzi wangu no 47
 
Unauhakika uzi huu ulikuwa kwenye jukwaa hili jana, au unaropoka tu?
Tumia akili yako hiyo kidogo uliyobakiza vizuri mwamba! Hili jukwaa ndilo lina washiriki wengi hivyo ni rahisi kupeleka ujumbe kuliko majukwaa mengine!
 
Uzuri wa Mwalimu Mwakasege ni kuwekeza kwake katika mafundisho ya imani kupitia Biblia Takatifu!

Hauzi maji ya upako, hauzi sabuni, hana muda mchafu wa kukashifu imani ya watu wengine, hana ujanja ujanja! Jambo hili linamfanya aheshimiwe na makundi yote ya dini ukilinganisha na watu kama Kakobe, Mwamposa, nk.
Siku ukitafakari maandiko utagundua kuwa naye ana makandokando mengi mno
 
Huwa nabarikiwa sana na huduma ya huyu mtumishi wa Bwana, sio kwamba hawapo wengine ila nikimsikiliza huyu naelewa sana. Ingawa huwezi kubalika na kila mtu kama baadhi wanaoanza kuponda, ila Mwl. Mwakasege anatumiwa na Mungu kwa viwango vya juu mno!!
 
Hebu tushikishe hayo "Madini" aliyonayo! Hivi amesoma Chuo au Vyuo gani vinavyotambulika vya Teolojia hapa Duniani? Na je Ni Mmoja wa Majalimu wa Teolojia hapa Tanzania?
Hayo ya teolojia ni yako mkuu,mimi husikiliza hekima zake.

Nilikuwa napenda kukaa hata na babu yangu kusikiliza stori na hekima zake na wala babu yangu huyo hana chuo alichosoma akatambulika.

Kwa kumalizia ni kuwa mimi kumsikiliza mtu siwezi sharti kwamba awe amesoma chuo au hajasoma ninachoangalia nini anasema..
 
Akili ya mwakasege ni sawa na mapadri 3

Hayo ya teolojia ni yako mkuu,mimi husikiliza hekima zake.

Nilikuwa napenda kukaa hata na babu yangu kusikiliza stori na hekima zake na wala babu yangu huyo hana chuo alichosoma akatambulika.

Kwa kumalizia ni kuwa mimi kumsikiliza mtu siwezi sharti kwamba awe amesoma chuo au hajasoma ninachoangalia nini anasema..
Mafundisho ya Laana na Mambo ya Miti ya Ukoo ndio Hekima yenyewe?
 
Uzuri wa Mwalimu Mwakasege ni kuwekeza kwake katika mafundisho ya imani kupitia Biblia Takatifu!

Hauzi maji ya upako, hauzi sabuni, hana muda mchafu wa kukashifu imani ya watu wengine, hana ujanja ujanja! Jambo hili linamfanya aheshimiwe na makundi yote ya dini ukilinganisha na watu kama Kakobe, Mwamposa, nk.
Noted mkuu

Mafuta aliyonayo mwl Mwakasege Ni tofauti kabisa na wengine
 
Hana tamaa, angekua na tamaa angeanzisha kanisa na ana watu wengi.
Nimehudhuria semina zake, kwanza kamati yake ya maandalizi wapo smart kufunga mahema na huduma nyinginezo.
Huwa nabeba daftari kabisa , maana nchi hii mwalimu ni Nyerere na Mwakasege tu, wengine ni "maticha" tu.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Ni kweli mkuu


Iyo paragraph ya mwisho una maana sisi wengine maticha tu
 
Nami nililiona hilo. Labda angealika ambao tayari wameokoka na wako kwenye utumishi. Kuna watu walikuja kuombewa tu au kuokoka. Kama walikuwepo walio kwenye utumishi, basi walikuwa kiduchu mno!
Still, somo lilikuwa linawagusa waumini wote; sema tu kulikuwa na vipande vipande vingine ambavyo vilikuwa vinawahusu ambao tayari wako ngazi ya juu zaidi ya ile ya muumini wa kawaida
 
Sadaka haiombwi; ni wajibu wako kama Mkristo kutoa sadaka pasi kulazimishwa. Hakuna ibada inayokamilika bila sadaka.

Na ukiwa mtu "sane" utajiongeza mbele zaidi na kuwaza kwamba hadi inafikia unakaa chini na kulisikiliza na kupokea Neno la Mungu; basi ujue kuna investment kubwa imefanyika. Gharama kubwa sana zinatumika kuandaa semina hizi; so hutojiuliza mara mbili kuhusu kutoa sadaka au kutoa chochote au kujitoa muda wako kwa ajili ya kusupport huduma hizi. It is a privilege kufanya kitu kwa ajili ya ufalme wa Mungu
Umetoa maelezo sahihi kabisa japo haujajibu swali nililouliza ndugu.
 
Karismastiki katoliki ni kawaida kuwaalika wahubiri wengine kutoka uprotestanti,hata kwenye makongamano ya wazi pia.
 
Umetoa maelezo sahihi kabisa japo haujajibu swali nililouliza ndugu.
Nafikiri lugha uliyotumia kwamba "anaomba" sadaka; haijakaa sawa. Mtumishi wa Mungu haombi sadaka ni sawa na kusema Mungu anakuomba sadaka . Ni hivi muda wa sadaka ukifika atasema sasa hivi ni muda wa sadaka; either yeye au kiongozi wa ibada ndiyo atatoa hiyo ratiba. Na pia huwa kuna sadaka ambayo ni optional kwa watu wanaowiwa kutoa chochote kusupport huduma (partnership), utapewa maelekezo yake.
 
Back
Top Bottom