Mwalimu Mwakasege yupo Mbeya kwa Huduma ya kiroho (MANA)

Sidhani Kama haya mafundisho huwa yanawasaidia watu. Wanavyozidi kusikiliza ndivyo wanavyozidi kupigika, kuwa wambeya zaidi, wezi, wahuni, wakonjwa etc.

Kuna haja ya kuwa na mjadara wa kitaifa kuona Kama dini zetu zinatusaidia au lah
Ukiona mahubiri fulani hayajakubadilisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine basi tambua unatakiwa ujitafakari wewe binafsi mahusiano uliyonayo na Mungu wako. Sio kila neno litakuponya!
 
We nadhani hata huelewi kinachoongelewa.
 
Kuna tatizo kubwa sana kati yako na Mwakasege mbali na huduma anayoifanya. Ninefuatilia mafundisho yake yote sijawahi ona anahubiri bila kurejea biblia. Sema tumezoeshwa kuwa chini ya wachungaji, Padre, mitume, manabii hivyo tukimuona Mwakasege tunahisi anakosea. Ukweli ni kwamba ndani ya jengo la kanisa sio ndyo wokovu wa kweli unapatikana humo. Wokovu upo kwa mtu mmoja mmoja.
 
Wewe hujui kitu juu ya Neno la Mungu. Ni mtu wa kupelekwa pelekwa tu kama mkokoteni wa punda. Nakuona ulivyo mtupu.
 
Ndugu yangu. Nira yako usijifunge na mchungaji bali jifunge na Yesu, kwasababu hata huyo mchungaji unaetaka kujifunga nira nae anamtegemea YESU.
 
Ndugu yangu. Nira yako usijifunge na mchungaji bali jifunge na Yesu, kwasababu hata huyo mchungaji unaetaka kujifunga nira nae anamtegemea YESU.
Nadhani hapo ndipo nahisi wakristo tunapotea.

Ukristo ni umoja. Tunaaswa kuwa wamoja na kamwe tusitengane..

Ukristo unatuhitaji kutembea na wale waliamini kama sisi.. ndio lengo la kuwa na kanisa. Sasa ukisema nira niifunge na Yesu pekee maana yake naleta utengano au nachagiza hali ya hukumu..kwa kuwatenga wasioamini

Wakati huo huo tunaombwa twende na wasioamini tukawe chachu au chumvi kwao.. tushike lipi!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Okay naanza kukuelewa, maana yako ni kwamba Mwakasege awe na darasa kwa watu maalum kwa vile alipewa kipawa kwa hilo kundi.

Sawa, je hao wenye dhambi kama Bujibuji watafundishwa na nani ?

Pia lengo la wahubiri wengi siyo kuokoa roho za watu ili waende Mbinguni, lengo lao ni ukwasi.
 
Jane kachanganyikiwa
 
Naomba kukuomba urudi mpaka verse ya 11 zilipotajwa hizo huduma tano kisha utuambie kuwa umeangalia nini kujua kua mstari wa 12 ulilenga huduma ya ualimu pekee?

Pia nimeona sehemu umemgusia roho mtakatifu,me nadhani kosa kubwa sana ulilo nalo katika uelewa wako ni kudhani kua roho mtakatifu atajifunua sawa kwako na kwa mtu mwingine,Roho mtakatifu hajawahi kutabirika kua atatenda namna hii wala namna ile,ni mpya kila wakati.

Pia wacha kukariri,hata wakati wa Yesu alipokua akiponya watu siku ya sabato,kuna watu kama wewe walioikariri torati walikua wakipinga wakidai haitakiwi kuponya siku ya sabato...and yet kumbuka Yesu alisema hajaja kuipindua torati and still aliponya watu siku ya sabato...hivyo usitake kuniambia eti mwakasege asihubirie wazinzi au walevi ambao Yesu alikufa kwaajili yao kwamba akawahubirie watakatifu wa kanisani na kuwaacha walevi mpaka muinjilisti aje.

Na huo mstari uliouweka hapo unasema KWA KUSUDI LA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU sasa hapa uelewe mtu ambae hayuko kamili katika utakatifu maana yake ana dhambi ndani yake so inaweza kua ulevi pia na uzinzi.

Kitu kisicho kamili maana yake kimepungukiwa jambo,na usipokua kamili katika utakatifu maana yake unahali fulani ya dhambi japo umeokoka.
 
Mwakasege mmoja wao
 
Sidhani Kama haya mafundisho huwa yanawasaidia watu. Wanavyozidi kusikiliza ndivyo wanavyozidi kupigika, kuwa wambeya zaidi, wezi, wahuni, wakonjwa etc.

Kuna haja ya kuwa na mjadara wa kitaifa kuona Kama dini zetu zinatusaidia au lah
We upo nyuma nyuma kama koti, hahahaha
 
Yesu alikua mwalimu au rabi alikua chini ya uangalizi wa mchungaji yupi
 
Personally I thank for your msg, hao mengine achana nao kuna Siku wanaelewa tu,
 
Ikitokea nimeokoka katika mkutano wake akiondoka ntakuwa nasali wapi?
Mkuu, ulishaokoka?

Huduma ya Mwakasege ina wanakamati toka madhehebu mbalimbali, wakiwemo Wachungaji. Huwezi kukosa pa kulelewa, utachukukiwa na Wachungaji eanaoshirikisne naye kwenye huduma.

Madhalani, kwa watu wanookoka kwenye semina zake, huandaliwa semina ya siku "kadhaa" na baada ya hapo, hukanidhiwa kwa Wachungaji wa Makanisa.

Mara nyingine, hizo semina hufanyikia kwenye Makanisa mbalimbali mara tu baada ya semina.

Nakumbuka kuna mwaka nilihudhuria semina yake jijini Mwanza, baada ya semina, wale waliookoka walitangaziwa Makanisa ambayo hizo semina za kuukulia wokovu zitaendelea kufanyika. Nakumbuka baadhi ya Makanisa yaliyotajwa siku hiyo ni AIC, PAG, RC, ANGLICAN, n.k.

Hutakosa pa kulelewa kiroho. Wanakamati wa huduma yake watakuelekeza pa kwenda baada ya kushauriana nawe. Hawatakulazimisha, watakushauri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…