Roho Mtakatifu alizigawa hizi huduma specifically kwa ajili ya makundi tofauti ya watu. Point yangu ni kuwa kila moja ya huduma zile 5 inalenga kundi Fulani la watu. Huduma ya uinjilisti ndiyo inalenga aina hizo za wenye dhambi, huduma ya uchungaji kanisa kwa ujumla nk.
Huduma ya ualimu/ kufundisha inalenga watu ambao hapo awali walikuwa wenye dhambi na sasa wapo kanisani ili kukuzwa wapate kuufikia ukamilifu wa Kristo.
Sasa jaribu kufuatilia kituko cha mikutano ya Mwakasege uone. Yeye amekusanya mchanganyiko wa waliookoka, wapagani, makahaba, walevi, wanaotafuta wachumba. Yaani full mchanganyiko. Then anaanza kuwafundisha( kumbuka huduma yake siyo uinjilisti). Hivi hapo kuna lengo lolote linafikiwa wakati targeted audience yenyewe imeshakosewa?
No wonder mafundisho yanayofundishwa ni potofu lakini watu wameganda tu wanaendelea kusikiliza. Unatarajia mtu asiye na uelewa hata chembe wa Neno la Mungu anaweza kuhoji mafundisho ya uongo? Obvious, atakaa na kukubali tu akiambiwa sijui "mafundisho ya ndoto" sijui "kumkomboa mzaliwa wa kwanza"