Kwanza nieleweke, sipingi wafanyakazi kuwa wananchama wa vyama vya wafanyakazi, na pia kulipa ada ya kuendeshea hivyo vyama (Trade Unions).
Hoja yangu iko sehemu moja tu. Vyama vya wafanyakazi vikusanye michango ya ada kwa wanachama wake kwa usawa! Yaani wanachama wote watozwe viwango sawa vya ada kila mwezi.
Kinachofanywa na CWT ndiyo kinacholalamikiwa na wadau wengi wa Elimu nchini. Yaani wanawakata wananchama wao 2% ya ada kila mwezi kwenye mishahara yao, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo. Maana hizo 2% hutofautiana kutoka mwanachama mmoja kwenda mwingine.
Badala yake wangetumia mfumo wa kuwakata kwa usawa kama walivyo anzisha hao wa elfu 5 kwa mwezi. Au unataka kuniambia na nyinyi TUGHE pia mnakatwa kwa mfumo huu wa 2% kwenye basic salaries zenu kila mwezi? Na kama na nyinyi pia mnafanyiwa hivyo, basi na mtakuwa mnaibiwa pia.