Mwalimu Nyerere anaishi katika sura ya Magufuli

Mwalimu Nyerere anaishi katika sura ya Magufuli

masahihisho. Nyerere aliwapenda watu wake .
nyerere alijenga nyumba za watumishi wa umma . huyu alisimamia zikauzwa nyingine kwa kina nanio
Nyerere alipenda watu kwa sababu aliamini kweli katika msingi wa UTU. BINADAMU WOTE NI SAWA. Magufuli anaamini katika UVITU, siyo UTU. Kwa Magufuli, vitu ni muhimu zaidi ya UTU. Ndio maana hakuelewa watu walipokuwa wanalia njaa. watu hawahitaji chakula, bali wanahitaji barabara. watu hawahitaji kupandishiwa mshahara, bali wanahitaji kununuliwa ndege na kupiga picha ndani ya ndege. kuipanda siyo muhimu.

Kuhusu usawa wa Binadamu, Magufuli anaamini katika BINADAMU HAWAKO SAWA. Ana chati yake ya mgawanyo wa binadamu, kama ifuatavyo:
1) WALIOMPIGIA KURA. Hawa ni binadamu wa daraja la kwanza. Hawatakiwi kubomolewa nyumba zao, hata kama wamejenga eneo ambalo halitakiwi kisheria. inabidi serikali itafute namna ya kurekebisha mambo ili wasibugudhiwe.
2) NDUGU na JAMAA.. Hawa kwa Magufuli ni watu muhimu sana. watapata vyeo mbalimbali.
3) WAPINZANI. Kwa Magufuli, hawa SIYO BINADAMU KAMILI. ila kama mtu anahama upinzani na kuhamia CCM, anaweza KUMSAMEHE MADHAMBI YAKE YA KUWA MPINZANI. Wapinzani ni watu wa kupigwa mabomu, kusumbuliwa, kupimwa mkojo, Kubomolewa nyumba, kupotezwa, na hata kupigwa risasi na kuuwawa.
 
Leo ninawaletea ufafanunuzi wa mambo yanayoashiria ufanano wa kiutendaji kati ya Mwl Nyerere na Ndg Magufuli Mwkt wa CCM na Rais wa Tanzania, kwa kuwa viongozi hufananishwa na hutofautishwa kwa utendaji wao katika kutoa uongozi.

-Ukweli

Mwalimu mwanzoni mwa miaka ya 1960 alipojiuzulu Uwaziri Mkuu kwenda kujenga Chama nakumuachia Serikali Mzee Kawawa, aliandika vitabu vitatu kimojawapo ni TUJIJISAHIHISHE ni kitabu kidogo chenye kurasa zisizozidi ishirini ambapo amesisitiza katika kusema kweli na neno Kweli limetajwa zaidi ya mara ishirini.
"Ukweli unatabia moja nzuri sana, haujali mkubwa wala mdogo, haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa.."

Hayo ni baadhi ya maneno katika kitabu hicho, yanayosisitiza kusema ukweli na kuheshimu ukweli. Hii ni sawa kabisa kwa Magufuli ambaye toka awali amekuwa ni kiongozi anayesisitiza kusema ukweli na kwa sasa ni mwasisi wa msemo "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu".

-Kusimamia Misingi

CCM ina msingi wa vitu viwili, Haki na Watu. Mwalimu mwaka 1968, akitoa hotuba aliyoiita, "Lazima Chama Kiwasemee watu" na moja ya kauli zake ni, "kazi ya Chama cha Siasa kilicho imara ni lazima kiwe kama daraja la kuwaunganiaha watu na serikali walioichagua." Mwalimu alisema akiwaasa viongozi wa Chama kuwa karibu na wananchi na kuwa watetezi wa haki za wanyonge.

Hiyo tunaishuhudia tena kwa Magufuli ambapo kwa kiasi kikubwa amekuwa akiwasisitiza viongozi wa Chama kuwa sikio la wananchi na hata mageuzi ya Chama yamelenga kukifanya kuwa "Chama Cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu"

-Falsafa ya kazi

Mwaka 1976 Mwalimu aliandika kitabu "kila mtu afanye kazi" kinachoeleza kwa undani umuhimu wa kazi katika maisha binafsi na kwa taifa. Sasa ni miaka 40 Magufuli amekuja na falsafa inayofanana ya "Hapa Kazi Tu".

- Sera ya Viwanda na Kilimo

Mwalimu aliweza kuanzisha programu za kilimo ikiwemo "utekelezaji wa siasa ni kilimo" - 1974, sera ya viwanda vidogo vidogo (SIDO), vya kati ikiwemo viwanda vya nguo urafiki, Mwatex, Mutex, Mbeyatex, n.k Sawa kabisa na Magufuli ambaye ndoto yake ni Viwanda. Miezi miwili iliyopita amezindua mradi mkubwa wa kilimo awamu II utakaogusa maisha ya wakulima wadogo kwa kuwapatia mikopo nafuu ya kilimo.

-Udhibiti wa madini

Katika suala la madini Mwalimu alifanya utambuzi wa maeneo yenye madini, hakuruhusu uchimbaji uanze mbali na changamoto tulizokuwa tukizipitia kama Taifa, kwa kuwa Watanzania hatukuwa na elimu ya kutosha ya Madini. Magufuli amekuja amekuta mikataba kandamizi iliyoingiwa na watangulizi wake baada ya mwalimu hivyo ameifumua mikataba yote ya Madini na kufanya haki ya mtanzania kuheshimiwa na kuweza kuingia makubaliano kutoka 3% ya awali mpaka 50/50%.

- Reli, Umeme na Anga.

Mwalimu aliweza kujenga Reli ya TAZARA miaka ya 1970, kwa upande mwingine alikuwa na ndoto kubwa ya ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme maarufu kama Stiegler's Gorge ambao ulikwamishwa, shirika la ndege lilikuwa na ndege za AirTanzania kabla halijafa katika awamu zilizofuata. Miaka 30 sasa Magufuli amefufua shirika la ndege na mpaka sasa serikali imefanikiwa kununua ndege Saba ndogo za kati na kubwa. Ujenzi wa Reli ya kisasa unaendelea naujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler's Gorge umeanza.

Vijana wa miaka ya 1990, Nyerere tunayesimuliwa nakumsoma amerejea katika sura ya Magufuli na ni jukumu letu kumpa ushirikiano na kufanya naye kazi kuhakikisha tunatekeleza na kufikia ndoto ya TViwanda.

Na mwandishi wetu,
Said Said Nguya
[email protected]
Vipi giza lifananishwe na nuru? Vipi mashariki ifananishwe na magharibi? Vipi ahera ifananishwe na kuzimu? Vipi harusi ifananishwe na msiba? Kwa vipi upumbavu ufananishwe na ujinga? Kwa vipi ukweli ifananishwe na uongo?
 
Nyerere alipenda watu kwa sababu aliamini kweli katika msingi wa UTU. BINADAMU WOTE NI SAWA. Magufuli anaamini katika UVITU, siyo UTU. Kwa Magufuli, vitu ni muhimu zaidi ya UTU. Ndio maana hakuelewa watu walipokuwa wanalia njaa. watu hawahitaji chakula, bali wanahitaji barabara. watu hawahitaji kupandishiwa mshahara, bali wanahitaji kununuliwa ndege na kupiga picha ndani ya ndege. kuipanda siyo muhimu.

Kuhusu usawa wa Binadamu, Magufuli anaamini katika BINADAMU HAWAKO SAWA. Ana chati yake ya mgawanyo wa binadamu, kama ifuatavyo:
1) WALIOMPIGIA KURA. Hawa ni binadamu wa daraja la kwanza. Hawatakiwi kubomolewa nyumba zao, hata kama wamejenga eneo ambalo halitakiwi kisheria. inabidi serikali itafute namna ya kurekebisha mambo ili wasibugudhiwe.
2) NDUGU na JAMAA.. Hawa kwa Magufuli ni watu muhimu sana. watapata vyeo mbalimbali.
3) WAPINZANI. Kwa Magufuli, hawa SIYO BINADAMU KAMILI. ila kama mtu anahama upinzani na kuhamia CCM, anaweza KUMSAMEHE MADHAMBI YAKE YA KUWA MPINZANI. Wapinzani ni watu wa kupigwa mabomu, kusumbuliwa, kupimwa mkojo, Kubomolewa nyumba, kupotezwa, na hata kupigwa risasi na kuuwawa.
Thumb up! Well said!!! A very strong and vividly comment.
 
Wakati mwingine Dunia huwa inajirudia. Zama za nyerere naziona kwa magufuli. Ununuzi wa ndege, umeme wa stiglers Gorge, stard gage yote ni mwendelezo wa baba wa taifa. Binafsi naona miaka 10 haitoshi. Kumbuka maendeleo hayana chama.
 
Naunga mkono hoja Mimi Binafsi natamani hata MAGUFULI aongoze miaka 20.asante Sana MWENYEZI MUNGU KUTUPA hii ZAWADI watanzania hatimaye umetukumbuka..hapa kazi tu
 
Naunga mkono hoja Mimi Binafsi natamani hata MAGUFULI aongoze miaka 20.asante Sana MWENYEZI MUNGU KUTUPA hii ZAWADI watanzania hatimaye umetukumbuka..hapa kazi tu
True walahi
 
Acha upumbavu wewe wa kufananisha madubwasha na mwalimu Nyerere.
Acha kabisa kabisa koma.
 
Wakati mwingine Dunia huwa inajirudia. Zama za nyerere naziona kwa magufuli. Ununuzi wa ndege, umeme wa stiglers Gorge, stard gage yote ni mwendelezo wa baba wa taifa. Binafsi naona miaka 10 haitoshi. Kumbuka maendeleo hayana chama.
na MATAKO ya nyani yanajionesha katika uso wa nani...? nauliza tu
 
Wakati mwingine Dunia huwa inajirudia. Zama za nyerere naziona kwa magufuli. Ununuzi wa ndege, umeme wa stiglers Gorge, stard gage yote ni mwendelezo wa baba wa taifa. Binafsi naona miaka 10 haitoshi. Kumbuka maendeleo hayana chama.
Una mjua nyerere kweli wewe nyau..! Kuanzia sura nyerere hakuwa na mbichwa, kichwa yake ilijaa madini, maneno yake yalijaa hekima, matendo yake yalijieleza vyema, dhamira yake haikuwa na hila, sura yake iliwakilisha watanzania, elimu yake haikuwa BRN, na mwisho hakuwa wala kutamani kuitwa dr/professor/ aliishia kuitwa mwalimu ila aliwafundisha maprofesa huyu ndiye nyerere.

Kiufupi hafananishwi kwa sura au kwa wasifu wa nje na ndani.
 
Kuchefuana sahizi ndo kilichobaki....umeshashiba supaget ndomana...
 
Hivi kwani yeye amefanya kitu gani kipya mpaka mnataka kubadilisha katiba kwani yeye ni nani anakitu gani bwana katiba iheshimiwe mbona USA [emoji631] marais wanafanya mambo makubwa na wanabadilika
 
Back
Top Bottom