Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Nikiwa mtoto mdogo pale Ikulu niliwahi kumona Mwalimu akitoa hotuba ndefu pembeni ya hayati Rashid Kawawa miaka ile ya 80 mwanzoni.
Mwalimu alijaliwa karama binafsi za ushawishi {charismatic leader}, alikuwa akiufahamu uwezo huo aliojaaliwa na Mungu lakini haikumfanya akavimba kichwa na kujiona kama vile siku zote hakanyagi ardhi. Alijishusha na akapenda zaidi ushawishi wa hoja zenye kuweza kumshawishi msikilizaji.
Aliweza kujenga hoja za kuutetea Muungano wa Tanzania na mpaka leo hazijapoteza mantiki kila zinapochezwa radioni katika vipindi maalum vya kisiasa.
Umoja huwadanganya wale wanaokuwa ndani yake kiasi cha kutotazamana wao kwa wao kwa maana ya udhafu wao wa asili, unawafanya wanaongea na kufikiria kwa aina moja hivyo umoja ni utajiri wenye kuficha dhambi zao mmoja mmoja.
Wamarekani wanajiita USA wanajitambulisha hivyo mahali popote pale. Hakuna anayejitambulisha kuwa ni mtexas au mu-atlanta, kwao kinachotangulia mbele ni wimbo wa Taifa wa kwao, akiwepo mwanamuziki kabla ya ufunguzi wa michuano ya mpira wa kikapu atapewa fursa ya kuimba wimbo wao kabla ya mechi kuanza.
Nguvu yao ya kiuchumi inaanza kwanza na kila mmojawao kutanguliza dhana ya umoja kabla hata chochote chenye manufaa hakijaanza kufanyika, yoyote anayekuja akitanguliza fikra za majimbo yanayosimama yenyewe huyo atapingwa kwa hoja na akazidisha ubishi atapotezwa na taasisi za kifedhuli kina FBI na CIA.
Nguvu ya umoja umekwenda Ulaya nzima na kila mwaka anajumuisha mwanachama mpya ndani ya NATO, Kiasi cha kumpa hasira Vladmir Putin aliyeshindwa kuona jirani yake Ukraine akiingizwa Ulaya akiwa mwanachama mpya aliye karibu kabisa na Russia. Umoja ni nguvu siku zote kwani unatufanya tufikirie tukiwa kitu kimoja na huo ni utajiri wa mwanzo kabisa wa kijamii.
Nawasikiliza wazenji wanasiasa namna wanavyojidanganya kwamba wanao uwezo wa kujitegemea pia na namna majibu mujarab wanayopewa kutoka kwa wale wanaharakati wa huku bara, wanasahau dhana mahiri ya umoja ndio inayowapa kiburi cha kunyoosheana vidole.
Nje ya umoja kuna kundi kubwa la makabila 120 yenye kila aina ya ubaya yanapotazamwa yakiwa peke yao. Nje ya umoja kuna wepesi mkubwa sana wa kujificha kwenye ubaguzi wa kikabila na kikanda ukionekana eti ndio sababu ya umaskini wetu kwa ujumla.
USA wana miaka 246 ya uhuru wao na hakuna namna ya siku moja mwanaharakati akajenga hoja nyepesi ya kutaka kuuvunja umoja wao wa kitaifa.
Kule Ulaya wameweza kuunganisha nguvu mpaka wakamkera Putin akaishambulia Ukraine, busara za kawaida tu zinayo haki ya kukubaliana kwenye namna mbalimbali za kuja na muafaka wenye lengo la kuunganisha zaidi nguvu zetu kuliko kuamini katika zile sababu za kila mtu aondoke na fito!.
Naamini katika kuja na suluhisho la kuunganisha nguvu kwa kufanya vikao vyenye kuziondoa kero za kiuongozi kuliko kudhani kuwa kuongeza serikal nyingine ndio njia yenye muafaka.
Tunaringia nchi yetu wakati wa kutambulishwa ndani ya muungano wetu, tukishapata huo utambulisho tunaoulilia ndio tutakapokutana na mengi ya bandia ndani ya uhusiano mpya bila ya kuwa na huyo anayeonekana ni adui.