Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

Sasa kwanini Kipindi Anaindaa Hakuiandaa inavotakiw?
Jamani wewe hujiongezi hata nukta?? Kumbuka tulikotoka na mazingira yalivyokuwepo! Bila kuweka katiba vile hali ingekuwaje? Wasomi wachache wajinga wengi sana......tumetoka kutawaliwa ilikuwa lazima awe vile anyooshe misingi kwanza then baada Kujitambua kama Taifa la watu wanaojielewa na waliosoma then tuweke misingi mizuri ya katiba kwa maslahi ya Taifa sasa!! Soma historia vizuri then linganisha na hali ya wakati ule
 
Hakuna rais nayemlaani kama Nyerere,

①.aliwafukuza wakoloni kabla hawajafanya maendeleo yoyote ukilinganisha na nchi zilizo cherewa kupata Uhuru
②.alishindwa kuona miaka 100 za Uhuru wa Tanganyika itakuweje
③.alijijengea sifa kwamba kwa kila akiongeacho ni chema, hamjui kama yale maneno yaliwafaa watu wa wakati ule?
④.aliahindwa kuimalisha mising ya elimu na afya ambayo ingejengeka hata kesho
⑤. Alipo ilaani Israel, hapa ndo aliwalaani watanzania sasa, maana maneno matakatifu hayatanguki, imeandikwa ,: AILAANIE ISRAEL, AMELAANIWA!
⑥.aliutangazia ulimwengu kwamba Tanzania haina dini, kosa kubwa hili maana yake haina njia ya kumtafuta mungu, kama inaongozwa ibilisi vile, hapa aka kamjaa kalishindwa kuwajengea wananchi hofu kwa Mungu naye kweli akatuacha, ndo maana viongozi wanafanya kazi Kama mawakala wa ibilisi
⑦hana sababu za msing juu ya muungano ambao hauna faida pande zote,

Ukinena mabaya juu ya Israel, utaangamizwa pasipo kujua sababu, mf. Nyrr, Gardaff, sadam,

Ni wakat wa kutubu kwa ajili ya aka kamzee tusijelaaniwa milele↠↛↝↔↪↦✞✟✝
 
Completely
Kama huyu faru john
Duh! Hii nchi hata ukiwa dikteta huwezi kuthubutu kuiongoza zaidi ya miaka kumi. Yaani mlianza na killaza, mkaja juma pombe maharage, mkahamia diabomba sasa hivi mko faru jon!! Ndio maana JK alipoulizwa ikiwa atapenda kuendelea baada ya miaka 10 akasema hataki kuongeza hata sekunde ya urais wake. Mambo gani haya sasa!!!!
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?

Umeona eeh!
Baba wa Taifa, Mwl. JK Nyerere(RIP) alikuwa mwenye hikma na busara sana! Aliliona hili mapema na bila hivo huyo mzee angelifia Ikulu kama angelitaka! Lakini aliamua kung'atuka mapema mwaka 1984!
Leo hii mijitu ya CCM yenye uroho wa madaraka imeamua kuifanya Tanzania ni mali yao na hawataki kusikia habari ya kubadilisha Katiba!
Mwaka juzi kwa maksudi kabisa waliwacheza shere Watanzania kwa kuona kwamba Katiba mpya ingelikuwa kifo cha CCM hivo wakavuruga mchakato wote!!!!!!
Leo Magufuli yuko Ikulu akitimiza utabiri wa Baba wa Taifa kwa kuitawala nchi kidikteta na kibabe akijifanya kama mungu mdogo kwa kuitumia Katiba hii ya kidikteta!!!!
Poleni sana Wabongo!
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?

Nyerere alikuwa mkuu wa wanafiki wote waliopo CCM. Alijua wazi kwamba katiba tuliyonayo haifai, lakini hakutaka kutumia cheo chake (alipokuwa rais kwa miaka takriban 24) au ushawishi wake (akiwa kama muasisi wa CCM na "Baba wa taifa") ili kuibadili na kufanya rais "asigeuke mungu." Nyerere alipotaka Mkapa awe rais mwaka 1995, alisimama kidete na kuhakikisha inakuwa hivyo. Hii ni sawa na Kikwete alipotaka Magu (2015) awe rais alisimama kidete na kufanya iwe hivyo. Sasa utaona kwamba viongozi hawa wakitaka jambo liende ndani ya chama chao na nchi linaenda, ila mabadiliko wasiyoyataka au kuyaamini ndio siku zote huja na visingizio vya kitoto...

Matatizo yeyote yanayoendelea nchini kwetu sasa hivi, baba na mlezi wake ni CCM! Hakuna namna nyingine ya kuchambua suala hili.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
Sasa mbona alishindwa kuwaletea Watanzania katiba mpya na kinyume chake akawaachia hili shimo la jehanamu? siungi mkono kauli yake maana alijua lakini alishindwa kufanya kile kilichokuwa kinatakiwa.
 
Sasa kama alilijua hilo yeye Nyerere alifanya nini kuondoa hilo tatizo?.
By the Way katiba hii hii si iliandikwa kipindi cha utawala wake?
Nyerere ndio alivuruga katiba mara baada ya kupata uhuru,akavunja mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.akaharibu elimu,akafundisha na kupandikiza propaganda,akageuza nchi sera za majaribio bila wananchi kuhoji,tulimwona kama Mungu Mtu,jina maarufu MUSA akisema hageuki nyuma kuwa jiwe.Sio kweli eti alingatuka kwa hiari yake mwenyewe,ni Makali ya IMF ya kufutiwa misaada hadi nchi ikageuka marapurapu na huku wakitaka kumpindua mara nyingi tu.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
Mungu mbariki Nyerere .
 
Braza Embu nifungue kitu kuhusu IMF
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
100000000000000000%
 
kweli kabisa ... nyerere kama vile alikuwa nabii pumzikabkwa aman Mzee wetu
Mkuu punguza mahaba unabii gani wakati yeye na wenzie kumi na nane ndio waliotutungia hiyo katiba mbovu na yeye aliitunga makusudi ili imsaidie ili afanye analotaka

Matatizo yote haya tunayopata yanayousiana na katiba mtu wa kwanza anaetakiwa kunyooshewa kidole ni Nyerere
 
J

Namlaumu sana na hata simwombei, alijua shida itatupata na akakaa kimya.
Pale unapojua tatizo halafu usifanye chochote unakuwa wewe ndio mwenye kubeba lawama wala sio huyo aliokosa Busara
wewe umeifanyia nini nchi hiii? Nyerere alikuwa binadamu km wewe, alikuwa na mapungufu yake km binadamu mwingine yeyote, ni mengi mno mazuri na makubwa aliifanyia nchi hii, ni vema ukayachukua mema yake na mabaya yake ukaweka kando hiyo itakusaidia sana, au km unachuki binafsi tu
 
Mkuu punguza mahaba unabii gani wakati yeye na wenzie kumi na nane ndio waliotutungia hiyo katiba mbovu na yeye aliitunga makusudi ili imsaidie ili afanye analotaka

Matatizo yote haya tunayopata yanayousiana na katiba mtu wa kwanza anaetakiwa kunyooshewa kidole ni Nyerere

ninavyoelewa neno Nabii au Mtume maana yake ni mtu anayetoka kwa Mungu akiwa na ujumbe wa Mungu kwa binadamu, kazi ndizo zinazomthibitisha mtu kama anatoka kwa Mungu au kwa Shetani, huu ni ukweli usio na shaka kuwa Mwalimu ni Nabii mkuu wa Afrika akifuatiwa na manabii wengine mfano, Nkwame Nkruma, Haile Selasie, Keneth Kaunda, Nelson Mandela wakiwemo Jomo Kenyatta, Milton Obote nk

mpeni heshima yake Nyerere acheni chuki zisizo za maana, heshima ya mtu hupimwa kwa kazi alizozifanya, ikiwemo mwenendo na tabia yake kwa kipimo hicho, hakuna mpigania uhuru yoyote Afrika unayeweza kumlinganisha na Nyerere, kazi alizofanya nyerere zilikuwa kubwa kuliko kazi zilizofanywa na wapigania uhuru wengine wa Afrika kwanini asiwe nabii?
 
Katiba inayompa nafasi raisi kuanzisha au kufuta ofisi yoyote iliyochini ya Utumishi wa Umma, Katiba ya ajabu aliyotuachia Nyerere
 
Natafuta mtaalam wa hisabati aniambie kike kichwa anachokichoraga Masoud Kipanya ni umbo gani?
Ile ni polygon mkuu....na tunaweza kukokotoa eneo na mzingo wake vilevile yani (area and circumference)
 
Back
Top Bottom