Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

Misemo mingine ya nyerere kuisema ni kuonyesha udhaifu wa marehemu, huo sio unabii ni sawa na baba mwenye nyumba anaiambia familia yake kuwa mlango fulani umelegea akija mwizi atauvunja kirahisi. Siku mwizi akiiba kupitia huo mlango watoto wanasema baba shujaa alitabiri kuingia kwa mwizi kirahisi. Nyerere kama alijua udhaifu wa katiba yetu alikuwa na ushawishi mkubwa wa kuiweka sawa badala ya kusubiri mtu mwenye busara kuitumia, je asipokuwa na busara....
 
Huwa nawalaani sana wabunge wengi wa ccm maana bila ujinga wao tungekuwa na katiba inayo enda na wakati tulionao na amabayo ingelijengea heshima taifa na maendeleo kwa ujumla ,lakin kwa kwa ujinga wao wa mshikamano wakaendelea kulipoteza taifa gizani kabisa
Hivi wewe hujui waliopinga katiba ya Warioba? Uko nao hukohuko kwa chadema ambao ni Sumaye, Kingunge na Lowassa!
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
Duuuhh umenikumbusha mbali sana .hakika Nyerere ni baba Wa taifa .basi sisemi tena [emoji87] [emoji87]
 
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa
Pamoja nakutambua kuwa katiba ni mbovu
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
majuzi tulimsikia Ridhiwani mtoto WA rais aliyepita Mh. Jakaya Kikwete akisema kwamba kuna kipindi alimuuliza baba yake kuhusu ukimya wake anapotukanwa kwenye mitandao. Rais alimjibu na kusema yeye ni rais ana mamlaka makubwa sana hivyo hawezi kutamka ovyo kwa wanaomsema ovyo. Mamlaka ya rais wa Tanzania yanahitaji rais mwenye Busara sana hata kama hana akili Sana. Busara kwanza.
 
ndiyo nakubaliana na kauli hiyo, refference rais Magufuli.
 
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa
Marekani ilipata Uhuru mwaka gani?wakati inapata Uhuru illiteracy
Ilikua kwa kiwango gani? Wakoloni waliacha misingi gani marekani na huku kwetu waliacha misingi ipi/
 
Sasa kama alilijua hilo yeye Nyerere alifanya nini kuondoa hilo tatizo?.
By the Way katiba hii hii si iliandikwa kipindi cha utawala wake?

Aliendelea kuwaonyesha CCM namna ya kuiba kura wakati za chaguzi.
 
majuzi tulimsikia Ridhiwani mtoto WA rais aliyepita Mh. Jakaya Kikwete akisema kwamba kuna kipindi alimuuliza baba yake kuhusu ukimya wake anapotukanwa kwenye mitandao. Rais alimjibu na kusema yeye ni rais ana mamlaka makubwa sana hivyo hawezi kutamka ovyo kwa wanaomsema ovyo. Mamlaka ya rais wa Tanzania yanahitaji rais mwenye Busara sana hata kama hana akili Sana. Busara kwanza.
kama jk alilijua hilo kwanini hakurekebisha sheria hizo???????...........badala yake akasaini sharia tena kwa dharura!!!!...........sheria hizo zinazo mwongezea rais madaraka ya ki-mungu.
 
J

Namlaumu sana na hata simwombei, alijua shida itatupata na akakaa kimya.
Pale unapojua tatizo halafu usifanye chochote unakuwa wewe ndio mwenye kubeba lawama wala sio huyo aliokosa Busara

Alifikiria chama chake nitakuwa cha mfano. Lakini kimejionyesha ndiyo chama jambazi kuliko vyama vyote duniani.
 
Mzee nyerere mnafki...yeye alikuwa na ushawishi na uwezo wa kubadili katiba why ajafanya hivyo?....
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
Tatizo sio mtu, tatizo ni mfumo.
Watanzania sijui tumelogwa na nani, kukataa hatujui, kuburuzwa tunalalamika
 
Mwl.nyerere naye katika hili aliteleza sana lijua kabisa katiba yetu ni mbovu na kwa kipindi kile alikuwa na power ya kusikilizwa chochote angetaka kiwe kwenye katiba kingekuwa hivyo hadi leo.alafu anakuja kutoa kauli kama hiyo huu ni ujinga.
mateso yote tunayoyapata yanayotokana na katiba nyerere ndio alisababisha
 
Uko sawa, tufanyeje sasa? Alosababisha alishatangulia mbele ya haki.

TUSEME SISIEMU HAPANA KWA KAULI MOJA
 
N kwa katiba hii tukimpata mgonjwa wa akili ndio tumekwisha! "Msipofanya kazi mtakufa na njaa, serikali haina shamba"! Daudi Albert Bashite hakiki vyeti vyako basi!
 
Back
Top Bottom