Mwalimu Nyerere kwanini alichagua Twiga? Ni Mnyama dhaifu sana!

Uko sahihi mkuu, lakini huu upole unaona jinsi unavyotugharimu kipindi hiki?
 
kama kwa alama ya Twiga mziki wake ndio huu; Full blast

alama ya Simba si ndio tutapoteana mazima kama nyumbu wa Serengeti.?
 
Hahah mkuu Nyegere naona mziki wako si mchezo,hapo uko tayari kupambana na Simba watatu,acha tu uwe nembo ya taifa.

Mkuu mng'ato ... naona unanipendekeza niwe nembo ya Taifa! .... unajua balaa letu lakini sisi kina Honey Badger aka nyegere?

 
Leo nakuunga mkono wewe mwana Lumumba, kweli tulitakiwa kuwa na nembo ya mnyama mwenye nguvu ma akili. Nahisi twiga katufanya tumekuwa wapole kama tulivyo
Ukishaona watu wanageukia vitu vya kijinga tena vya kiimani kama nembo na kuihusisha na mafanikio yao basi ujue hao watu ni wavivu wakubwa na wanatafuta kisingizio. Dawa ya mafanikio ni kazi tu na hakuna mbadala wake. Wakongo hapa jirani wamemweka chui lakini bado matatizo kibao. Kuna mataifa kibao alama zao ni za wanyama wakali wakali lakini bado ni maskini wa kutupwa.
 
Daaa umenikumbusha movie ya The Lion King. Hapo namuona akiwa na Simba.
 
Barbarosa tushukuru hata huyo twiga, ungesemaje kama angewekwa nyumbu?
 
Kamabarage hahusiki na mnyama huyo hilo ni chaguo la mkoloni so tumerithi tuu
 
Simba ana nguvu; mbabe anawaonea wanyama wengine. Huyo anafaa kuwa alama ya nchi kama Marekani yenye mabavumabavu zinazoonea nchi nyingine. Tanzania hatuko hivyo. Twiga ni mrefu mwenye shingo ndefu inayomuwezesha kuona mbali. Vivyo hivyo Mwalimu alikuwa anaona mbali. Kwa mfano aliona kwamba tukianza kuchimba madini yetu tutakuja kuliwa tu na wataalamu wa nje wanaokuja kuyachimba. Hivyo ni bora kuyaacha yakae ardhini tu mpaka tutakaposomesha wataalamu wetu wenyewe. Hiyo ilikuja kuwa wazi alipong'atuka waliomfuata wakaanza kuchimba madini ya kila aina. Ndiyo unakuta tunapewa mrahaba wa 3% pamoja na kuwa mali hiyo ni yetu. Ndiyo maana awamu ya sasa inapigana kuongeza hiyo asilimia mpaka 16% ingawa hata hiyo bado ni ndogo. Kwa ufupi, Mwalimu alikuwa anaona mbali na Twiga ndiye mnyama mwenye uwezo huo. Na Twiga hamuonei mnyama mwingine mdogo mdogo. Utakuta anachunga pamoja na swala au digidigi bila kugombana. Na Tanzania ndivyo tulivyo. Hatuingilii nchi nyingine isipokuwa tukilazimishwa kama alivyofanya Amin. Kinyume chake, Marekani kila kukicha yuko huko na kule kuchokoza tu kama alivyo Simba.
 
 


Chui siyo Mfalme wa Nyika, kwanza ni mmoja kati ya Wanyama waoga sana na huishi kwa kujificha mtini.
 
Tungekuwa tunachagua sasa tungechafua faru au mbwa mwitu maana kwa sasa ndo tunu tuliyonayo, zama zile hawa wanyama walikuwepo wengi tu na hatukujua kama wangekuja kuwa tunu, ata ivyo tumemachi twiga na mlima kilimanjaro, sifa ya nchi hii ni urefu katika kila kitu, mlima mrefu, ziwa refu, chanzo cha mto mrefu, ziwa lenye kina kirefu n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…