Mwalimu Nyerere kwanini alichagua Twiga? Ni Mnyama dhaifu sana!

Ni kweli mkuu Tai ametajwa kwenye Biblia,lakini si unajua Shetani ana tabia ya kuteka mambo ya kimungu na kuyageuza yawe for his advantage.And please also note that Bundi ni ndege,lakini ni kweli pia kwamba anaweza kutumiwa kwa mambo ya kichawi kama vile Njiwa,Paka mweusi,Mbayuwayu nk.
 
Alishapewa heshima yake wakati wa uongozi wa Mw. Nyerere. Kiwanda cha ku-assemble magari cha NYUMBU!
 
Nyerere hakumchagua twiga. Twiga alishachaguliwa tangu enzi za ukoloni alichofanya yeye ni kurithi tuuù
 



Kuna umuhimu somo la uraia ambalo zamani liliitwa siasa kufundishwa upya. Leo watu awaelewi hata maana ya alama ya twiga. Lakini pia watanzania hawajui tabia za wanyama ambao wengi tunao nchini. Tulifundishwa shuleni kwanini Tanzania tuliamua kuwa na Twiga kama alama ya Taifa letu. Sifa za Twiga ni kama zifuatazo;
1. Ni mnyama mrefu kuliko wote anaona mbali.
2. Twiga upenda kula majani yaliyo mazuri machanga si makavu hivyo utafuta matawi ya juu.
3. Twiga ni mpole na mtaratibu.
4. Twiga akichokozwa ni mnyama wa hatari sana, anapokasirika anauwezo wa kumuuwa simba kwa teke moja tu.
Hivyo Twiga uwa anaonesha nguvu zake pale anapochokozwa. Ndo hivyo tulivyo watanzania. Tu wakarimu na wapole, ila mtu akitaka kukuingilia ndipo uonesha nguvu zetu. Wakati wa vita ya Idd Amini, Tanzania tulichokozwa tulikaa kimia Idd Amini alipozidi tulimuonesha sisi ni nani. Tanzania iliogopewa sana. Ulimwengu ulijua Tanzania tungeshindwa hiyo vita. Lakini Tukashinda. Huu ndo uhalisia wa Twiga. Mpole ila simba akitaka kuona makali ya Twiga amchokoze au kutaka kula mtoto wake ndo atatambua twiga ni nani. Ndo maana ili kumuuwa Twiga wanahitajika simba wengi hata kumi. Kwa sababu ana nguvu za ajabu. Usilalamike sisi kuwa na alama ya Twiga ni alama ya pekee duniani nchi nyingi hazina hii alama. Hizo za Tai, simba zinajirudia rudia. Kwanza simba anawaogopa mbwa mwitu, Tai kiboko yake black mamba. Tazama hapa uone nguvu ya Twiga anavyowasambaratisha simba.

 
Shida siku hizi mpk kuna mpk masimba mashoga,bora tubaki na twiga wetu tu wao bado hawajapata kashfa.

Au kama vp tumtumie NYEGERE kama nembo ya Taifa.
Kwamba tuna genye ?
Maana mdau mmoja kasema anatumika twiga sababu watanzania ni wakarimu
 
Leo nakuunga mkono wewe mwana Lumumba, kweli tulitakiwa kuwa na nembo ya mnyama mwenye nguvu ma akili. Nahisi twiga katufanya tumekuwa wapole kama tulivyo
Twiga hakamatwi na Simba mmoja. Lazima wawe zaidi ya watatu. Hivyo Simba kwa Twiga sio lolote sio chochote. Aende mmoja aone kazi atakayopata.
2: Twiga Hali majani ya chini Kama wafanyavyo wala manyasi wengine watembeao. Twiga hula MATAWI YA JUU yaliyo laini matamu.
3: Urefu wake humsaidia Twiga kumuona adui( Simba chui duma fisi mbweha mbwa mwitu) hata adui awe km 2. Hii humsaidia Twiga kujihami mapema kwa kutoa viashiria kwa familia yake.
4: Twiga sio mgomvi sio mtata sio mshari. Hana majivuno.
Hizo Ni sifa za nembo yetu ya Taifa.
 
Mkuu yapo mambo mengi yaliyoandikwa kwenye Biblia,maovu na mema.Kwa mfano imeandikwa kwamba Mfalme Suleiman alioa masuria mia saba,lakini hii haina maana kwamba na sisi tuwe na mitala.Biblia imeandika pia kwamba Musa aliua,lakini hii haina maana kwamba na sisi tuue;Ibrahim alimuoa mjakazi wake,lakini hii haina maana kwamba na sisi tuoe wajakazi wetu;Mfalme Daudi alizini na kuoa mke wa jemadari wake,lakini hii haina maana kwamba na sisi tufanye hivyo nk.nk..Haya yaliandikwa ili kutuonya sisi,so kama tunaona hayako katika mpango wa Mungu,hatuna budi kuyaacha,haijalishi kama yalitumiwa zamani au laa.

Mwisho tusisahau kwamba zipo kwa mfano rangi(nyekundu na nyeusi),wanyama,
ndege kama tai au hata mimea ambayo adui anapenda kuitumia kwa malengo yake.Kwa mfano kama wewe unaji associate na rangi nyekundu au nyeusi,Shetani anaweza kuitumia hiyo kama conduit kuku-posses na kukushambulia,hasa kama huko vizuri kiroho,kwa hiyo ni lazima tuwe makini sana,everything we do must be properly calculated,as individuals or as a nation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…