Viongozi wetu wakuu waliokwisha kutangulia kama Mwalimu Nyerere na Mkapa wanaonekana “kupumzika kwa amani”, lakini yupo mmoja wao John Magufuli anayeonekana kutoachwa “apumzike kwa amani”. Je, Kuna nini nyuma ya jambo hili la kihistoria?
Kwa mtazamo wangu Nyerere na Mkapa (kwa kiwango kikubwa) waliwaachia watu uhuru wa kusema na kutoa maoni yao kupitia vyombo vya habari na mikusanyiko mbalimbali, ila uhuru huu ulikosekana wakati wa utawala wa Magufuli.
Kinachotokea sasa ni watu kutumia uhuru wao wa kujieleza ulioporwa enzi za Magufuli na hivyo kumfanya Magufuli kutopumzika hadi watu watakapomaliza kusema.