Mwalimu Nyerere na Mkapa wamepumzika kwa amani, kwanini Magufuli haachwi apumzike kwa amani?

Mwalimu Nyerere na Mkapa wamepumzika kwa amani, kwanini Magufuli haachwi apumzike kwa amani?

..sijasema kwamba ufisadi pekee uliotokea ktk awamu ya Mkapa ni uuzwaji wa nyumba za serikali nchi nzima kwa bei ya kutupa.

..kulikuwa na ufisadi mwingine mkubwa-mkubwa kama ulivyoelezea ktk post zako za awali na hapo juu.

..kuhusu mauaji ya waandamanaji wa Unguja na Pemba ni ukweli usiopingika kwamba tukio lilitokea wakati Mkapa akiwa nje ya nchi.

..yeye atabeba lawama kama RAISI wa nchi, lakini sio kwa uzito uleule kama mauaji hayo yangetokea akiwa nchini.

..kwa upande mwingine, je, unaweza kusema kwamba Mkapa au watendaji wake walipanga njama kuuwa waandamanaji wa Pemba na Unguja?

..matukio mabaya yaliyotokea ktk utawala wa Magufuli yanaonyesha kulikuwa na njama za kuyapanga na kuyatekeleza.

..Ben Saanane kupotea, Lissu kupigwa risasi,Sugu kufungwa, Lijualikali kufungwa, Mbowe, Msigwa, Halima Mdee, etc etc yote ni mipango na njama zilizosukwa na kutekelezwa. Na kwa kiwango kikubwa inaelekea kulikuwa na baraka za Magufuli.

..Mazungumzo ya MARIDHIANO yamepelekea kuachiliwa huru kwa wanachama wa Chadema zaidi ya 400 waliotiwa magerezani au mahabusu kwa uonevu na hila na serikali ya Magufuli.

..Je, ukisoma taarifa kama hizo huoni kwamba Magufuli alikuwa mtawala katili zaidi kulinganisha na watangulizi wake?

NB:

..Sina kumbukumbu ya watu waliochukuliwa hatua za Raisi Mkapa kwa kuhusika na mauaji ya Pemba na Unguja.

..Pia siamini kama Ripoti ya Tume ya Brig.Gen.Hashim Mbita ilitenda haki kwa waathirika wa mauaji yale.
Nimekuelewa mkuu.
 
Hao uliowataja hawana kundi la kuwatetea mitandaon maan, waliyofanya hayahitaj watetezi!! NB; Kama kuna mazuri kafanya mtu je kuna haja ya kuwepo kikundi cha kumtetea ama la!
Uwezo wako wakufikiri ni mdogo saana jitafakari..
 
Viongozi wetu wakuu waliokwisha kutangulia kama Mwalimu Nyerere na Mkapa wanaonekana “kupumzika kwa amani”, lakini yupo mmoja wao John Magufuli anayeonekana kutoachwa “apumzike kwa amani”. Je, Kuna nini nyuma ya jambo hili la kihistoria?

Kwa mtazamo wangu Nyerere na Mkapa (kwa kiwango kikubwa) waliwaachia watu uhuru wa kusema na kutoa maoni yao kupitia vyombo vya habari na mikusanyiko mbalimbali, ila uhuru huu ulikosekana wakati wa utawala wa Magufuli.

Kinachotokea sasa ni watu kutumia uhuru wao wa kujieleza ulioporwa enzi za Magufuli na hivyo kumfanya Magufuli kutopumzika hadi watu watakapomaliza kusema.
MATESO ALIYOWATENDEA WATANZANIA WENZAKE NDIYO YANAMFANYA ASIPUMZIKE
 
Back
Top Bottom