Mwalimu Nyerere na Mkapa wamepumzika kwa amani, kwanini Magufuli haachwi apumzike kwa amani?

..kwasababu alikuwa fisadi, laghai, mbaguzi, na mkatili.
Kwa ufisadi na ukatili hakuna aliyemfikia mkapa. Ukituliza akili utaona hakuna rais aliyeua watanzania wengi na kusababisha wakimbizi wengi kama mkapa, ndugu zetu wa Pemba ni mashahidi kwa hili.

Hakuna kipindi mali za taifa hili zimeibiwa kwa kiwango cha kutisha kama kipindi cha mkapa.
 

..moja kati ya wizi / ufisadi mkubwa ktk awamu ya Mkapa ilikuwa uuzwaji wa nyumba za serikali kwa bei ya kutupa. Na msimamizi na mtekelezaji wa wizi huo alikuwa Magufuli.

..ni kweli wakati wa Mkapa waliuawa Waunguja na Wapemba idadi yao inaweza kufikia 60. Idadi hiyo inabishaniwa baina ya serikali na chama cha Cuf.

..Kutokana na mauaji na vurugu kuna wananchi walilazimika kwenda ukimbizini Mombasa na Somalia.

..Lakini Mkapa anaweza kutetewa kwamba mauaji yale yalitokea akiwa nje ya nchi, hivyo huenda hakutoa amri wananchi wale wauwawe.

..Pia Mkapa aliunda Tume ya Uchunguzi ili kubaini kilichotokea. Kwasababu tukio hilo baya lilitokea mara moja tunaweza kusema ilikuwa bahati mbaya, halikuwa limepangwa.

..Tatizo la Magufuli lilikuwa kufanya mambo ya kikatili kwa miaka 6 aliyokuwa madarakani. Na kwa bahati mbaya hakujiweka mbali na mambo hayo ya hovyo. Wanasiasa waliokuwa wakikamatwa walikuwa wanaambiwa ilikuwa ni "amri kutoka juu."

..Pia Magufuli alitengeneza makundi ya kizandiki kusifia na kuhalalisha mambo ya kikatili yaliyokuwa yakifanyika. Yaani kulikuwa na magenge yaliyokuwa yaki-indoctrinate jamii kwamba ushenzi na ukatili ni mambo ya kuonea fahari.
 
Ufisadi unaouona kwa mkapa ni uuzwaji nyumba za serikali tu kwa kuwa ulimhusisha Magufuli; kuuzwa kwa NBC, ununuzi wa rada kwa bei isiyo halisi, kuwapa kandarasi wageni kuendesha TANESCO bila kufuata taratibu na uchafu mwingine mwingi hutaki kuuangalia sijui kwa sababu zipi.

Utetezi wa mkapa kuwa nje ya nchi wakati wapemba wanauawa na kukimbia nchi ni mwepesi sana, labda uniambie baada ya hiyo tume aliyounda ni nani waliwajibishwa.

Nafahamu mkapa alioa kwenu, lakini hiyo isikupofushe.
 
kumbe unauliza swala halafu unajijibu mwenyewe.kazi kweli kweli.mm nilidhani unahitaji majibu!
 
kumbe unauliza swala halafu unajijibu mwenyewe.kazi kweli kweli.mm nilidhani unahitaji majibu!
Nimetoa mtazamo wangu embu toa na wewe mtazamo wako.
 
FURAHA YA MTU DUNI MASIKINI NI KUONA TAJIRI AKIUMIZWA BILA KUONA KUWA TAJIRI HUYO NDIYO MUAJIRI WAKE KWA MAFUTA YA KUPIKIA ANAYOYAUZA!
 
Vipi wale waliozzamishwa baharini huko Zanzibar 2001?
 
Hawa wanaomsema ni watu ambao walikuwa wakifaidika na ufisadi. Hivyo wana hasira kwasababu magufuri alionyesha uwezo na kuwaprove wrong kuwa maisha ya watanzania na umasikini unaowaandama si asili yao wala si matokeo ya uhalisia bali ni kundi au makundi ya watu yanawahujumu na kuwafanya kuwa duni miaka yote.

Kama magufuri kwa miaka mitano , mtu m'moja bila msaada wa makundi ya hawa wezi ameweza kukimbiza uchumi na kuanza kuadjust maeneo tata je wangepatikana watu wa aina yake 200,000 tu serikalini hii Tanzania ingeanza kuwa kama Uchina.

Sasa hawa mamburula unaona hata sasa wamekazana kupiga vijembe tu ila ukiwaambia mbona yanayoendelea na maovu tupu mbona hamkemei, wanakaa kimya.

Wapumbavu sana hawa takataka.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Wa kupimwa akili wewe..!!
 
Viongozi wetu wakuu waliokwisha kutangulia kama Mwalimu Nyerere na Mkapa wanaonekana “kupumzika kwa amani”, l


Unao uhakika gani kwamba huko walipo wamepumzika kwa amani??
 
Magufuri ni Mtu mwingine hao uliowataja hakuna wa kumfananisha nae mzee,Nyerere alitupotezea muda tu hatukuwa tayari kujitawala,Mkapa vitu vyote alivyokuta baada ya utawala wa mwinyi alikuja kuuzaa tu na kuturudisha nyuma kiuchumi.
Jpm alikuwa anapambana kuleta mambo mapya na kuondoa wale waliobaki kuitafuna nchi....Sema ndo hivyo walimchomoa Fuse RIP mzee
 
Magu Jiwe ilikuwa ukitoa maoni yaliyo tofauti na yake unakiona cha mtema kuni, hakukuwa na uhuru wa kuwa na mtazamo tofauti na wake katika jambo lolote.
 

..sijasema kwamba ufisadi pekee uliotokea ktk awamu ya Mkapa ni uuzwaji wa nyumba za serikali nchi nzima kwa bei ya kutupa.

..kulikuwa na ufisadi mwingine mkubwa-mkubwa kama ulivyoelezea ktk post zako za awali na hapo juu.

..kuhusu mauaji ya waandamanaji wa Unguja na Pemba ni ukweli usiopingika kwamba tukio lilitokea wakati Mkapa akiwa nje ya nchi.

..yeye atabeba lawama kama RAISI wa nchi, lakini sio kwa uzito uleule kama mauaji hayo yangetokea akiwa nchini.

..kwa upande mwingine, je, unaweza kusema kwamba Mkapa au watendaji wake walipanga njama kuuwa waandamanaji wa Pemba na Unguja?

..matukio mabaya yaliyotokea ktk utawala wa Magufuli yanaonyesha kulikuwa na njama za kuyapanga na kuyatekeleza.

..Ben Saanane kupotea, Lissu kupigwa risasi,Sugu kufungwa, Lijualikali kufungwa, Mbowe, Msigwa, Halima Mdee, etc etc yote ni mipango na njama zilizosukwa na kutekelezwa. Na kwa kiwango kikubwa inaelekea kulikuwa na baraka za Magufuli.

..Mazungumzo ya MARIDHIANO yamepelekea kuachiliwa huru kwa wanachama wa Chadema zaidi ya 400 waliotiwa magerezani au mahabusu kwa uonevu na hila na serikali ya Magufuli.

..Je, ukisoma taarifa kama hizo huoni kwamba Magufuli alikuwa mtawala katili zaidi kulinganisha na watangulizi wake?

NB:

..Sina kumbukumbu ya watu waliochukuliwa hatua za Raisi Mkapa kwa kuhusika na mauaji ya Pemba na Unguja.

..Pia siamini kama Ripoti ya Tume ya Brig.Gen.Hashim Mbita ilitenda haki kwa waathirika wa mauaji yale.
 
Tuliza domo lako, wewe sumesema humwamini Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…