JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,114
- 3,541
Morning friends!
Basi, mwaka mmoja Mwalimu alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara. Jioni ya siku ya kwanza baada ya shughuli za mchana kutwa akarudi kupumzika pale Shangani, Ikulu ndogo. Akiwa chumbani kwake akashangaa kuona binti maridadi sana anapanga panga vitu. Mara arekebishe hiki mara asogeze kile, Nyerere ikabidi amuulize, Mbona hivyo? Basi binti yule akamjibu kuwa yeye ametumwa na mkuu wa Mkoa aje kumsaidia Mwalimu kuusindikiza usiku asiwe mpweke.
Mwalimu akamuuliza yule binti kwani Mkuu wa Mkoa hajui Mwalimu ni Mkatoliki? Na kwamba Mkatoliki anakiapo cha mke mmoja? Binti akabaki kimyaa. Mwalimu akamwita mkuu wa mkoa akamuuliza, Hujui kuwa mimi ni Mkatoliki? Mkuu wa mkoa akajibu, nafahamu.
Mwalimu akamhoji swali jingine. Toka lini Mkatoliki aliye shika nadhiri akafanya haya?
Mkuu wa Mkoa akakaa kimyaa. Mwalimu akamwambia mrudishe binti huyu nyumbani kwao. Kisha wewe tangulia Dar es salaam. Mkuu wa mkoa akapata mtihani. Akatumbuliwa, ingawa baadae aliteuliwa tena kushika nyadhifa kadhaa serikalini.
Kisa cha pili, Mwalimu alikuwa na kawaida ya kuwaandaa viongozi kabla ya kuwateua.
Siku moja majira ya kiangazi Katibu tarafa mkoani alipata barua ikimtaka afike Ikulu tarehe iliyo pangwa. Yule bwana akaogopa sana kuitwa Ikulu kwa Nyerere.
Basi, akamtafuta rafikie wa karibu akamwambia kuhusu wito ule.
Rafiki yake akamwambia usikute wabaya wako wamemwambia Nyerere unafanya biashara ya meno ya tembo. Yule afisa tarafa akasema, inawezekana! Dunia hii imejaa watu wabaya sana.
Siku ikawadia! Akafika Ikulu. Zamu yake ilipo fika akaingia ndani. Baada ya salamu huku anatetemeka akamwambia Mwalimu;
Mwalimu Dunia hii imejaa watu wabaya sana. Mimi sijawahi kufanya biashara ya meno ya tembo hata siku moja! Sijawahi.
Nyerere akamtazamaa kisha akamwambia haya nenda nje, kapumzike kwenye kiti.
Wakati anatoka wenzake wakamuuliza umepewa kuwa mkuu wa Wilaya gani? Maana ndicho walicho itiwa!!! Losalalee akajisemea mwenyewe kumbe nimeharibu mambo kwa haraka zangu.
Akarudi Iringa kuendelea na utarafa wake.
Kisa cha tatu, hiki kilimkuta aliye kuwa Waziri wa Elimu na Mkuu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe. Nitawaletea siku nyingine.
Kwenye siasa kuna visa na vijimambo!!