Mwalimu Nyerere vs Thabita Siwale

Mwalimu Nyerere vs Thabita Siwale

tenanzinyo

Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
64
Reaction score
23
Wadau wa historia habari zenu? naombeni msaada kuna habari nimewahi kuisikia zamani kidogo inamhusu Mwalimu Nyerere kipindi hicho akiwa Rais wa Tz na mwanasiasa mkongwe Bi Thabita Siwale waziri wa zamani wa elimu na utamaduni!

Hbr yenyewe ipo hivi huyu bi Thabita Siwale chanzo cha yeye kuteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Waziri wa Elimu miaka hiyo ni ujasiri wa kipekee aliounyesha akiwa mkuu wa shule sekondari maarufu mkoani Tabora(jina nimelisahau) kwa kuumpa adhabu ya kurudi nyumbani kwa muda(sunspension)mtoto Mwalimu Nyerere aliyekuwa akisoma katika shule hiyo na kumuamuru siku ya kurudi shule aje na mzazi wake ili hali akijua kabisa mzazi wake ni rais wa nchi mwalimu Nyerere!

Aidha inasemekana baada ya kumpa adhabu hiyo watu wengi walianza kumtisha Bi Thabita kuwa atafukuzwa kazi kwa kumrudisha nyumbani mtoto wa Rais.

Baada ya adhabu kwisha yule mtoto alirudi shuleni akiwa na mzazi wake kama alivyoamriwa katika barua aliyopewa wakati wakurudishwa nyumbani Walimu na hata Bi Tabitha walistaajabu walipomwona yule mtoto kaja na Mwalimu Nyerere,wenyewe walimu na Bi Tabitha walitegemea mwalimu Nyerere angemtuma mwakilishi kutokana majukumu na hadhi yake ya urais wa nchi.

Baada ya kumwona Nyerere inasemekana mama Tabitha na staff nzima walichanganyikiwa wakajua sasa mwisho wao ndiyo umefika wa kufukuzwa kazi,lkn mwalimu Nyerere aliwatoa wasiwasi na kuwambia wasiwe na hofu yoyote yeye pale hajaja kama Rais wa nchi bali amekuja kama mzazi wa mtoto,baada ya hapo kengele ya paredi ikangongwa wanafunzi wakakusanyika wote yakaelezwa yale makosa ya mtoto wa Nyerere akaamriwa kuchapwa viboko na mwisho wa siku akaruhusiwa kuendelea na masomo,mwalimu Nyerere akarudi zake Dar es Salam.

Nasikia baada ya muda BiThabita badala ya kufukuzwa kazi akateuliwa kuwa waziri elimu kwa ushujaa aliounyesha!Maswali ya kujiuliza je kwa sasa hivi ni mkuu gani wa shule anaweza kumfukuza mtoto wa rais Shule achilia mbali watoto wa wabunge,mkuu wa wilaya au mkoa,waziri au hata wakurugenzi tu?

Kwa hakika Bi thabita alionyesha ushujaa wa hali ya juu sana!Kwa kizazi cha sasa tuna hitaji aina ya viongozi km Bi Tabitha Siwale ambao wanaweza kufanya maamuzi magumu bila kujali hadhi ya mtu!
 
MwanaJF mimi ninakubaliana na wewe kwa 95% kuwa watanzani wa sasa wengi wao hawajiamini katika mahamuzi mazito kama alivyofanya Bi Tabitha.

Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa naye Bi Tabitha hakutegemea kuwa mtoto wa Nyerere siku ya kurejea shule atakuja na baba yake ambaye ni Rais wa nchi "kama ulivyoeleza kuwa walimu walitegemea kwamba mtoto atapewa mwakilishi wa baba" kwahiyo hii ilitokea kama miujiza kwao, hawakutegemea, ndiyo maana walimu walishangaa kumuona Nyerere ameongozana na mtoto wake.

Mimi kwangu naona ni jambo la kawaidi sana kwa mzazi kama Nyerere kufanya kitendo kama hicho.

Uzuri wa Nyerere alikuwa hapuuzii kitu, hata kikiwa kidogo namna gani, lazima alikuwa anafanya ufatiliaji na kujua hitimisho lake.

Na huyu Bi Tabitha kupewe uwaziri' nadhani si kwamba kwa sababu ya kumfukuza mtoto wa Rais wa nchi! na kumuagiza mtoto aje na baba yake baada ya adhabu yake kumalizika.

Yawezekani ni utendaji wake wakazi' nakumbuka wakati huo shule zilikuwa chache sana kwahiyo wakuu wa shule walikuwa wanajulikana mpaka ngazi za juu katika wizara kwa uchapaji kazi. Kwahiyo Bi Tabitha yawezeka alikuwa anajulika kwa Nyerere hata kabla ya jambo hilo.

Sioni kama ni jambo la kusangaza kwa wakati huo.
 
Hii story imevulugwa kidogo, ninavyojua mimi mtoto wa Nyerere aliyewahi kufukuzwa shule ni John ambae alikuwa anasoma Mazengo DODOMA wakati huo ikiitwa Illiance.

Kwa uhakika kabisa headmaster aliyemtimua shule mtoto huyo alikuwa anaitwa Mr. Kamuzola ambae baadae aliteuliwa na Nyerere huyo huyo kuwa RDD Dodoma mwaka 1972 wakati wa centralization.

Thabita Siwale aliibukia chuo cha ualimu Korogwe kule alikutana na Waziri mmoja wa elimu alikuwa mhuni mhuni hivi aliitwa Chediel Mgonja waliwaki kupishana na Siwale kwa ajili ya mambo yake ya ufsika(waziri) wakati huo mambo hayakuwa magumu kama ilivyo sasa ilikuwa ni kawaida kabisa Principal kumtafutia kitowewo waziri hata kama ni mwanachuo na mkuu wa chuo kuneemeka privilege fulani toka kwa waziri.

Haya Siwale aliyakataa kabisa, labda msimamo huu ulimfikia Mzee Julius kwani waziri huyo hakudumu. Sikumbuki kama Siwale alipata ubunge wa kuteuliwa, ila nadhani aliteuliwa maana enzi hizo viti maalum vilikuwa bado kuanzishwa, basi alipopata ubunge akawa ni waziri wa elimu.

Habari zinasema baada ya kuwaa waziri mama huyu akawa anacheza rafu sana mambo ya kiunyumba na mzee Siwale kila mala mzee akimhitaji basi alikuwa anamjibu kwamba amechoka na kwamba uwaziri wa elimu siyo mchezo, basi Mzee Siwale akatoa malalamiko kwa Nyerere ikabidi naye amwondoe kwenye nafasi hiyo ili amhudumie vizuri Mzee Siwale.

Chaguzi zilizofuata hakufua dafu alijaribu ubunge wa Afrika Mashariki pia hakufua dafu,akanzisha NGO yake akaiita WAT( women Advancement Trust) ofisi zake ziko Kinondoni barabarani kabisa nadhani ni Kawawa road .

Uliyeandika Tread hii nenda pale kinondoni utamkuta huyu mama akupe ukweli zaidi toka mdomoni mwake.
 
Sawa kabisa ebaeban! Tabitha alipewa uwaziri kwa sababu ya ujasuri wake. Si unajua yule ni Mnyakyusa?

Ila alikija kukosana na Nyerere baada Tabitha kuanza kumdharau mumewe. Kwa vile tu alikuwa waziri!
 
Okay yote kwa yote hapa tunachojifunza ni namna mwalimu alivyokuwa mweledi na mtu asiyependelea upande wake hata awe mke au mtoto. Iko stori nyingine ya mtoto wake mwingine aliyekuwa akisoma Old MOshi. kuna siku mtoto alikataa kula chakula kwa janja janja kama kuumwa hivi. Mtoto alitaka apewe special diet. Mwalimu alipojulishwa akasema huyo mtoto apewe hicho chakula alichokataa na aachwe atakula tu muda ukifika. mtoto alikaa weee mwisho njaa ilipomzidi alikila kile chakula na hakurudia tena suala lile.
 
Sawa kabisa ebaeban! Tabitha alipewa uwaziri kwa sababu ya ujasuri wake. Si unajua yule ni Mnyakyusa?

Ila alikija kukosana na Nyerere baada Tabitha kuanza kumdharau mumewe. Kwa vile tu alikuwa waziri!

Ni kweli kabisa anamdharau sana mumewe. Huyu anasali kwa mwingira na anatoa sadaka ya mamilioni huku mumewe akiwa anakaa tu nyumbani hana hata senti tano. kwa kifupi ni mama mwenye roho mbaya sana hastaili kusifiwa hata kidogo. Yaani mzee siwale anaishi kama msukule wakati mkewe anaishi kama milionea.
 
Wapi Andrew Nyerere atupe version yake?

Hii habari sijaisikia. Hili jambo naona ni distraction.Huyu Thabita Siwale sikuifuatilia sana career yake. I was too youmg at that time to be preoccupied with politics. Halafu hakuna mtoto wa Mwalimu ambaye amesoma Tabora.
Maoni yangu ni kwamba walimu wanaowabughudhi watoto wa viongozi,I hate them with perfect hatred. Hao watoto wa Wabunge,watoto wa Katibu Kata,mimi kaka yao. Tabia ya kuwaita vibaka,walevi,teja,na kuwafanyia fujo,ikomeshwe mara moja. I ask that they should be left in peace.
 
Andrew.

Mind.

I could have provided a sympathetic ear - not that you need one- had your case needed a just, or even equanimous treatment.

But a lot of people would look at your scantily detailed response, with the best intent, and still garner a perfect case for a divisive, classic, haves against have nots, us against them, brahmis against dalits, age old dichotomy that Mwalimu stood against and Mwalimu in the particular sense of the thread stood against, mind the case invoking, Mwalimu against mwalimu.

Surely you can make a better case devoid of that simplified old age dichotomy characterization.

Where is that case?
 
Hii habari sijaisikia. Hili jambo naona ni distraction.Huyu Thabita Siwale sikuifuatilia sana career yake. I was too youmg at that time to be preoccupied with politics. Halafu hakuna mtoto wa Mwalimu ambaye amesoma Tabora.
Maoni yangu ni kwamba walimu wanaowabughudhi watoto wa viongozi,I hate them with perfect hatred. Hao watoto wa Wabunge,watoto wa Katibu Kata,mimi kaka yao. Tabia ya kuwaita vibaka,walevi,teja,na kuwafanyia fujo,ikomeshwe mara moja. I ask that they should be left in peace.
Mie nilisikia huyo mtoto alikuwa anasoma Korogwe Girls na Mama Siwale alikuwa mkuu pale wakati huo
 
Ndio waziri pekee ambaye rekodi yake haijavunjwa mpaka leo alikaa wizara ya elimu karibu miaka kumi alikuwa pia waziri wa ardhi alikosa uwaziri baada ya kuingia Raisi Mwinyi
 
Okay yote kwa yote hapa tunachojifunza ni namna mwalimu alivyokuwa mweledi na mtu asiyependelea upande wake hata awe mke au mtoto.
Juzi juzi, wakati wa uzinduzi wa bodi ya udhamini ya kuwaenzi waasisi wa taifa, Mwalimu na Karume, nilipata fursa ya kuongea na binti Nyerere kwa jina la Rose, alisema Mwalimu was a very loving father, ndiye aliyemfudisha Rose kupika chai!, japo alikuwa hatembezi bakora kwa watoto wa kike, ila kwenzi zilitembea kwa makosa ya kijinga jinga!.
Pasco.
 
Hii habari sijaisikia. Hili jambo naona ni distraction.Huyu Thabita Siwale sikuifuatilia sana career yake. I was too youmg at that time to be preoccupied with politics. Halafu hakuna mtoto wa Mwalimu ambaye amesoma Tabora.
Maoni yangu ni kwamba walimu wanaowabughudhi watoto wa viongozi,I hate them with perfect hatred. Hao watoto wa Wabunge,watoto wa Katibu Kata,mimi kaka yao. Tabia ya kuwaita vibaka,walevi,teja,na kuwafanyia fujo,ikomeshwe mara moja. I ask that they should be left in peace.

Mmmh..!!! I have a million reasons to doubt about your upstairs.
 
Back
Top Bottom