tenanzinyo
Member
- Dec 28, 2012
- 64
- 23
Wadau wa historia habari zenu? naombeni msaada kuna habari nimewahi kuisikia zamani kidogo inamhusu Mwalimu Nyerere kipindi hicho akiwa Rais wa Tz na mwanasiasa mkongwe Bi Thabita Siwale waziri wa zamani wa elimu na utamaduni!
Hbr yenyewe ipo hivi huyu bi Thabita Siwale chanzo cha yeye kuteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Waziri wa Elimu miaka hiyo ni ujasiri wa kipekee aliounyesha akiwa mkuu wa shule sekondari maarufu mkoani Tabora(jina nimelisahau) kwa kuumpa adhabu ya kurudi nyumbani kwa muda(sunspension)mtoto Mwalimu Nyerere aliyekuwa akisoma katika shule hiyo na kumuamuru siku ya kurudi shule aje na mzazi wake ili hali akijua kabisa mzazi wake ni rais wa nchi mwalimu Nyerere!
Aidha inasemekana baada ya kumpa adhabu hiyo watu wengi walianza kumtisha Bi Thabita kuwa atafukuzwa kazi kwa kumrudisha nyumbani mtoto wa Rais.
Baada ya adhabu kwisha yule mtoto alirudi shuleni akiwa na mzazi wake kama alivyoamriwa katika barua aliyopewa wakati wakurudishwa nyumbani Walimu na hata Bi Tabitha walistaajabu walipomwona yule mtoto kaja na Mwalimu Nyerere,wenyewe walimu na Bi Tabitha walitegemea mwalimu Nyerere angemtuma mwakilishi kutokana majukumu na hadhi yake ya urais wa nchi.
Baada ya kumwona Nyerere inasemekana mama Tabitha na staff nzima walichanganyikiwa wakajua sasa mwisho wao ndiyo umefika wa kufukuzwa kazi,lkn mwalimu Nyerere aliwatoa wasiwasi na kuwambia wasiwe na hofu yoyote yeye pale hajaja kama Rais wa nchi bali amekuja kama mzazi wa mtoto,baada ya hapo kengele ya paredi ikangongwa wanafunzi wakakusanyika wote yakaelezwa yale makosa ya mtoto wa Nyerere akaamriwa kuchapwa viboko na mwisho wa siku akaruhusiwa kuendelea na masomo,mwalimu Nyerere akarudi zake Dar es Salam.
Nasikia baada ya muda BiThabita badala ya kufukuzwa kazi akateuliwa kuwa waziri elimu kwa ushujaa aliounyesha!Maswali ya kujiuliza je kwa sasa hivi ni mkuu gani wa shule anaweza kumfukuza mtoto wa rais Shule achilia mbali watoto wa wabunge,mkuu wa wilaya au mkoa,waziri au hata wakurugenzi tu?
Kwa hakika Bi thabita alionyesha ushujaa wa hali ya juu sana!Kwa kizazi cha sasa tuna hitaji aina ya viongozi km Bi Tabitha Siwale ambao wanaweza kufanya maamuzi magumu bila kujali hadhi ya mtu!