Mwalimu wa field aliyesambaza picha za watoto wamekaa chini kufukuzwa (uhaba wa madawati)

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
Mwalimu aliyesambaza picha hizi kufukuzwa

JUMATANO , 8TH FEB , 2023

NA MWANDISHI WETU

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Wakili Triphonia Kisiga, amesema Mwalimu wa kujitolea katika shule ya sekondari Sinde, Evarist Chonya, aliyesambaza picha za uongo za wanafunzi wakiwa wamekaa chini amesimamishwa na kwamba kwa kuwa sio mwajiriwa atafukuzwa kabisa.

Picha hizo zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikielezwa kuwa wanafunzi hao wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo na kuibua taharuki kwa jamii.

Imeelezwa kuwa mwishoni mwa wiki madawati yote ya shule hiyo yalitolewa nje ya vyumba kwa ajili ya kuyaandika majina ya wanafunzi ili kila mwanafunzi awe na dawati lake ambalo atakuwa analitumia na kulitunza mpaka atakapohitimu kidato cha nne.

Na kwamba wakati shughuli hiyo ikiendelea mwalimu huyo aliwarejesha darasani baadhi ya wanafunzi na kuwaamuru wakae chini kisha akawapiga picha kwa nia ambayo haijulikani.

Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Anathalia Luwungo amesema shule hiyo ina wanafunzi 1300 kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ambao wote wanakaa kwenye madawati na hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye anakaa chini kama ambavyo picha hizo zinaeleza.

kufukuzwa.jpg
hali halisi.jpg
 
Hayo mambo ya upungufu wa Madawati wachagga huwa wanayasikia tu kwenye redioni, kwani walishazoea kujitolea kumaliza kero ndogo ndogo kama Vyoo mashuleni, madawati, Vitanda Mahospitalini Matengenezo ya kawaida kwa barabara zao za vijijini nk.

Halafu anatokea mtu huko kusema eti Kilimanjaro inabebwa, Shame!!!
 
Mwalimu aliyesambaza picha hizi kufukuzwa

JUMATANO , 8TH FEB , 2023

NA MWANDISHI WETU

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Wakili Triphonia Kisiga, amesema Mwalimu wa kujitolea katika shule ya sekondari Sinde, Evarist Chonya, aliyesambaza picha za uongo za wanafunzi wakiwa wamekaa chini amesimamishwa na kwamba kwa kuwa sio mwajiriwa atafukuzwa kabisa.

Picha hizo zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikielezwa kuwa wanafunzi hao wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo na kuibua taharuki kwa jamii.

Imeelezwa kuwa mwishoni mwa wiki madawati yote ya shule hiyo yalitolewa nje ya vyumba kwa ajili ya kuyaandika majina ya wanafunzi ili kila mwanafunzi awe na dawati lake ambalo atakuwa analitumia na kulitunza mpaka atakapohitimu kidato cha nne.

Na kwamba wakati shughuli hiyo ikiendelea mwalimu huyo aliwarejesha darasani baadhi ya wanafunzi na kuwaamuru wakae chini kisha akawapiga picha kwa nia ambayo haijulikani.

Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Anathalia Luwungo amesema shule hiyo ina wanafunzi 1300 kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ambao wote wanakaa kwenye madawati na hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye anakaa chini kama ambavyo picha hizo zinaeleza.

View attachment 2510742View attachment 2510743
Huyu mwana angeendelea tu kula vitoto vya kinyaki huko hayo mambo mengine angeachana nayo tu
 
Hayo mambo ya upungufu wa Madawati wachagga huwa wanayasikia tu redioni, kwani walishazoea kujitolea kumaliza kero ndogo ndogo kama Vyoo mashuleni, madawati, Vitanda Mahospitalini nk
Halafu anatokea mtu huko kusema eti Kilimanjaro inabebwa, Shame!!!
wapare bwanaa!!!

mkuu huo ukabila wako unaingiaje kwenye mada sensitive kama hii?
 
Back
Top Bottom