Mwalimu wa field aliyesambaza picha za watoto wamekaa chini kufukuzwa (uhaba wa madawati)

Mwalimu wa field aliyesambaza picha za watoto wamekaa chini kufukuzwa (uhaba wa madawati)

Mwalimu aliyesambaza picha hizi kufukuzwa

JUMATANO , 8TH FEB , 2023

NA MWANDISHI WETU

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Wakili Triphonia Kisiga, amesema Mwalimu wa kujitolea katika shule ya sekondari Sinde, Evarist Chonya, aliyesambaza picha za uongo za wanafunzi wakiwa wamekaa chini amesimamishwa na kwamba kwa kuwa sio mwajiriwa atafukuzwa kabisa.

Picha hizo zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikielezwa kuwa wanafunzi hao wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo na kuibua taharuki kwa jamii.

Imeelezwa kuwa mwishoni mwa wiki madawati yote ya shule hiyo yalitolewa nje ya vyumba kwa ajili ya kuyaandika majina ya wanafunzi ili kila mwanafunzi awe na dawati lake ambalo atakuwa analitumia na kulitunza mpaka atakapohitimu kidato cha nne.

Na kwamba wakati shughuli hiyo ikiendelea mwalimu huyo aliwarejesha darasani baadhi ya wanafunzi na kuwaamuru wakae chini kisha akawapiga picha kwa nia ambayo haijulikani.

Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Anathalia Luwungo amesema shule hiyo ina wanafunzi 1300 kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ambao wote wanakaa kwenye madawati na hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye anakaa chini kama ambavyo picha hizo zinaeleza.

View attachment 2510742View attachment 2510743
Nashindwa kuelewa, kosa lake ni nini haswa?
 
Kimsingi si vizuri kumuanua muajiri wako madhaifu yake. Wanaofanya hivyo ni makachero waliotumwa au kujituma kupekuapekua udhaifu, hala kuna wale walimu wanafiki, unaadhibu mwanafunzi yeye anarekodi video na kuisambaza, walimu wa hivi huenda wana kazi zingine wanazotumwa. Mi niadhibu mwanafunzi mtovu wa nidhamu halafu mwalimu mwenzangu anirekodi, hiyo simu nitaipasuapasua, sitaki unafiki
 
Hakuna mtoto atadahiriwa pasipo mzazi kulipia/changia dawati. Hilo ni hitaji la lazima kwa mwanafunzi wa sekondari.
Huyo mwalimu wa kujitolea alifanya kitendo hicho kwa maksudi tu ili apate cha kupost kwenye mitandao ya kijamii.
 
Kwenye hz shule za serikali kuna watoto ni wajasiri huwez amini,unashangaa dogo anakuletea zawadi wakati wa jioni

aJabu ni kuwa,mwalimu mpya wa kiume huwa anaanza kuwa karibu na wanafunz wa kike haraka kuliko wa kiume
🤣🤣🤣Ndo ivo
 
DSM kuna shule ya sekondari wanafunzi wamekisa madawati wanakaa chini sembuse huko Mbeya.
Kuna uongo ktk taarifa hii.
 
Back
Top Bottom