Mwalimu wa field aliyesambaza picha za watoto wamekaa chini kufukuzwa (uhaba wa madawati)

Mwalimu aliyesambaza picha hizi kufukuzwa

JUMATANO , 8TH FEB , 2023

NA MWANDISHI WETU

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Wakili Triphonia Kisiga, amesema Mwalimu wa kujitolea katika shule ya sekondari Sinde, Evarist Chonya, aliyesambaza picha za uongo za wanafunzi wakiwa wamekaa chini amesimamishwa na kwamba kwa kuwa sio mwajiriwa atafukuzwa kabisa.

Picha hizo zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikielezwa kuwa wanafunzi hao wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo na kuibua taharuki kwa jamii.

Imeelezwa kuwa mwishoni mwa wiki madawati yote ya shule hiyo yalitolewa nje ya vyumba kwa ajili ya kuyaandika majina ya wanafunzi ili kila mwanafunzi awe na dawati lake ambalo atakuwa analitumia na kulitunza mpaka atakapohitimu kidato cha nne.

Na kwamba wakati shughuli hiyo ikiendelea mwalimu huyo aliwarejesha darasani baadhi ya wanafunzi na kuwaamuru wakae chini kisha akawapiga picha kwa nia ambayo haijulikani.

Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Anathalia Luwungo amesema shule hiyo ina wanafunzi 1300 kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ambao wote wanakaa kwenye madawati na hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye anakaa chini kama ambavyo picha hizo zinaeleza.

View attachment 2510742View attachment 2510743
Nmeielewa JEANS ya madoa doa ya mwalimu, Dah! Bila kuwepo somo la MAADILI nchi hii itakuwa ngumu mno. Walimu kizazi kipya kazi ipo
 
Mbona hawajatatua tatizo mambo ya madawati na vyumba vya hovyo hivyo utadhani sio shule wao wanaona sawa madirisha hayana kitu chochote utadhani milango huyo Mwanasheria wa wawapi anakua kilaza hivyo...
 
Imeelezwa kuwa mwishoni mwa wiki madawati yote ya shule hiyo yalitolewa nje ya vyumba kwa ajili ya kuyaandika majina ya wanafunzi ili kila mwanafunzi awe na dawati lake ambalo atakuwa analitumia na kulitunza mpaka atakapohitimu kidato cha nne.
Hayangeweza kuandikiwa humohumo darasani?
 
Upumbavu ni mzigo mkubwa sana kwanini wasingempa tuzo kwa ajili ya kufichua uozo badala yake wanamfukuza, SHAME yaani badala aliyeonyesha panapovuja ashukuriwe ili pazibwe matokeo yake anaadabishwa, fisiemuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu imechoka sana inahitaji kupumzika hii ni AIBU
 
Binafsi

Nampongeza Mwalimu KWA kazi nzuri!

Kupitia yeye wanafunzi wamepata madawati japo ni ya mchongo coz sekondari hawatumii madawati kama hayo bali ni viti na meza!

Walimu kama huyo kijana aliepost Ndio wazalendo na anapaswa apewe ajira haraka Sana!!

Namshauri mkurugenzi amuajiri Mwalimu huyo KWA ushujaaa na uzalendo wake!

Taifa linajengwa na wenye kuthubutu na sio waoga!!

Mungu ibariki Tanzania NCHI yetu tuipendayo Sana
 
Mwalimu aliyesambaza picha hizi kufukuzwa

JUMATANO , 8TH FEB , 2023

NA MWANDISHI WETU

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Wakili Triphonia Kisiga, amesema Mwalimu wa kujitolea katika shule ya sekondari Sinde, Evarist Chonya, aliyesambaza picha za uongo za wanafunzi wakiwa wamekaa chini amesimamishwa na kwamba kwa kuwa sio mwajiriwa atafukuzwa kabisa.

Picha hizo zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikielezwa kuwa wanafunzi hao wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo na kuibua taharuki kwa jamii.

Imeelezwa kuwa mwishoni mwa wiki madawati yote ya shule hiyo yalitolewa nje ya vyumba kwa ajili ya kuyaandika majina ya wanafunzi ili kila mwanafunzi awe na dawati lake ambalo atakuwa analitumia na kulitunza mpaka atakapohitimu kidato cha nne.

Na kwamba wakati shughuli hiyo ikiendelea mwalimu huyo aliwarejesha darasani baadhi ya wanafunzi na kuwaamuru wakae chini kisha akawapiga picha kwa nia ambayo haijulikani.

Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Anathalia Luwungo amesema shule hiyo ina wanafunzi 1300 kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ambao wote wanakaa kwenye madawati na hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye anakaa chini kama ambavyo picha hizo zinaeleza.

View attachment 2510742View attachment 2510743
Mbona maandishi ni ya zamani na madawati yenyewe sii mapya,kwanini yatolewe nje na kuandikwa leo,,🤔 Tafakari chukua hatua 🏃🏃
 
Back
Top Bottom